Madamboss
Member
- Sep 7, 2021
- 5
- 193
Jeshi la kujenga taifa (JKT) ni moja ya chombo kilichoundwa tarehe 10 Jul, 1963 baada ya nchi yetu kupata uhuru. Lengo kuu ni kuelimisha, kudumisha uzalendo, maadili na nidhamu ya vijana na kuwafanya wawe raia wanaopenda kutumikia na kuiilinda nchi yao.
Mara baada ya kumaliza kidato cha sita, sheria ya nchi huwataka wahitimu wajiunge na JKT kwa muda wa miezi mitatu. Kuna kambi maalumu ambazo zimetengwa katika mikoa mbalimbali kwa ajili ya kufanikisha hili zoezi kwa mfano JKT Maramba iliyopo Tanga, JKT Mtabila ya Kigoma na JKT Itaka ya Songwe.
Zifuatazo ni baadhi ya faida ambazo zitapatikana iwapo vijana wataishi kwa muda kwenye jamii halisi wanapoenda kwenye mafunzo yao ya JKT.
Vijana kupata muda wa kutosha na mazingira mazuri ya kutafakari taaluma wanaoenda kusomea katika elimu ya juu. Wahitimu wa kidato cha sita kwa kawaida humaliza elimu hiyo mwezi wa tano na kuanza chuo mwaka huo huo kwenye mwezi wa tisa/kumi. Ndani ya muda huu mchache, kwa mujibu wa sheria wanaochaguliwa wanatakiwa wakaudhurie mafunzo ya JKT. Ingekuwa ni vyema zaidi ikiwa vijana hawa wakafanya maamuzi haya ya msingi wakiwa katika jamii. Ili wajue changamoto zilizopo katika jamii na wawe na utayari kipindi wanapomaliza elimu ya chuo kurudi kufanya kazi katika mazingira haya ili kuleta mabadiliko na maendeleo. Kwa mfano mzuri, kumekuwa na wimbi kubwa la watumishi kama vile waalimu na wahudumu wa afya kutokuishi katika mazingira ya kazi wanapopangiwa maeneo ya mbali na miji. Ilikuepuka haya ni bora vijana wakaone mazingira halisi yaliyopo kabla hawajaenda kusoma elimu ya juu.
Kuwa sehemu ya jamii kutawaisaidia vijana kuwafumbua macho kuhusiana na maisha wanayoyaishi watu wengine na kutambua fursa ndani ya nchi yetu. Baadhi ya vijana kwa sehemu yote ya maisha yao wameishi kwenye miji mikubwa ya Tanzania kama Dar es Salaam na Mwanza. Uwepo wa programu hii ndani ya mafunzo yao itawasaidia vijana kutambua fursa zilizopo kutokana na maeneo tofauti hapa nchini Tanzania. Ni ukweli uliowazi kwamba kila eneo linakuja na fursa zake. Kwahiyo ni vyema wahitimu wa kidato cha sita wakitambua rasiliamali tulizobarikiwa kama nchi na wakaanza kuwa na mawazo ya namna ipi bora ya kuzitumia kwa manufaa binafsi na ya nchi. Na wanapoelekea vyuoni wakahusishe elimu yao na rasiliamali zilizopo.
Kufahamu tamaduni za makabila mbalimbali. Tanzania imebarikiwa zaidi ya makabila 200 ambayo yana mila na desturi tofauti tofauti. Na hizi tamaduni ni urithi wetu ambao hatupaswi kuupotezea bali kuulinda na kuhakikisha vizazi vijavyo vinafahamu asili yetu. Vijana walio JKT wakifahamu kuhusu tamaduni zetu ni hatua mojawapo kwenye kuusambaza na kudumisha. Utamaduni unajumuisha lugha, chakula, ngoma, mila, mavazi na mengineyo. Ni kwa bahati mbaya kati ya makabila 200 ni machache sana ambayo yanajulikana. Hii inamaanisha kwamba baada ya vizazi kadhaa kupita makabila haya yatapotea pamoja na tamaduni husika. Hivyo basi ni muhimu kuchukua hatua mapema ilikuhakikisha tunalinda utamaduni ambao ni tunu ya nchi yetu.
Faida nyingine itakayopatikana kutokana na wahitimu wa kidato cha sita kuishi kwenye jamii ni maendeleo ya kijamii kutokana na utatuzi wa changamoto ndogo ndogo. Kwa ngazi ya elimu ya elimu walionayo hawa vijana ni rasiliamali kubwa ambayo ikitumika vyema kuna baadhi ya masuala yatapatiwa utatuzi. Kwa mfano, kuwasaidia waalimu mashuleni kwa kuwaongezea ujuzi wanafunzi wa shule ya msingi na hata wa sekondari au hata kujihusisha na miradi mingine ya maendeleo iliyoanzishwa sehemu mbalimbali. Na kizuri zaidi kwa namna nyingine hii itamuongeza kijana uzoefu katika nyanja mbalimbali.
Pia kuwapa motisha wanafunzi ambao wapo katika ngazi za chini za elimu kuongeza jitihada na kuamini katika ndoto zao. Kuna watoto wanaishi kwenye mazingira magumu ambayo wanakosa mtu wa kumtazamia. Na kutokana na changamoto za hapa na pale wanakosa kuona umuhimu wa kusoma. Watoto wengi kwa namna hii hupoteza mwelekeo wa maisha. Uwepo wa wahitimu wa kidato cha sita itasaidia kuwapa motisha watoto wadogo kwenye safari ya elimu. Na hii programu ikiwekewa mfumo mzuri ulioendelevu itakuwa ni vizuri kwa wanafunzi wanapomaliza elimu ya msingi hasahasa kutoka kaya zisizo na kipato kikubwa kuwa "linked up" na wanafunzi waliowatangulia kwenye suala la elimu. Hii itajenga utaifa na vijana wataishi kwenye misingi bora huku wakipambana kwa kuona mifano hai ya watu waliofanikiwa.
Naamini programu hii itasaidia kuunda viongozi ambao wanauchungu wa kutaka kuleta maendeleo mkubwa katika nchi yetu. Hii ni kwa sababu watakuwa wameyaishi maisha ya Mtanzania mwenye kipato cha chini. Ni vigumu kwa kiongozi ambaye anapokea changamoto kwa kuelezwa kuwa na msukumo mkubwa wa kutaka mabadiliko kama yule ambaye ameishi kwenye jamii na kufahamu wananchi wanataka kitu gani. JKT ni chombo mojawapo ambacho kinatumika vizuri ilikuwaanda vijana ambao ni viongozi wajao wa taifa letu. Hadi kufikia sasa kuna viongozi wengi wamepita huku na huo ni uthibitisho tosha wa umuhimu wa hiki chombo. Hivyo basi ni vyema kijana wa Kitanzania akapandikizwa hasira ya kutaka maendeleo akiwa mdogo kwa kupitia chombo kama JKT.
Kwahiyo iwapo serikali itaongeza hii programu kwenye muda wa mafunzo wa JKT, manufaa mengi yatapatikana. Na katika yote tutaendeleza sera ya baba wa taifa ya ujamaa. Lakini pia kila kijana anayepata fursa ya kujiunga na JKT atarudi mtaani akiwa na hadithi yake ya namna ya kuleta mabadiliko (stories of change).

Upvote
196