A
Anonymous
Guest
Sisi wanafunzi na wahitimu wa programu za Technical Education in Engineering (Civil, Electrical na Mechanical) katika Mbeya University of Science and Technology (MUST), tunakabiliwa na changamoto kubwa ya kutotambuliwa kitaaluma ipasavyo.
Hali hii imesababisha ugumu wa kuomba na kupata ajira nyingi za uhandisi, licha ya kusoma kwa muda wa miaka minne na kujifunza masomo mengi yanayofanana kwa kiasi kikubwa na yale ya programu za “pure engineering”.
Kutokana na changamoto hiyo, wahitimu wengi wanashindwa kuajiriwa katika taasisi za uhandisi kwa sababu hawawezi kusajiliwa na ERB (Engineers Registration Board). Aidha, wanapojaribu kutafuta ajira katika taasisi za mafunzo ya ufundi, hukumbana pia na vikwazo vinavyowafanya washindwe kupata nafasi za kazi zinazolingana na taaluma zao. Matokeo yake ni kuwa wahitimu wa programu hizi wanajikuta hawana fursa za ajira zilizo wazi na zinazoendana na ujuzi walioupata chuoni.
Pamoja na kuwepo kwa changamoto hizi kwa kipindi cha zaidi ya miaka minne, chuo kimeendelea kudahili idadi kubwa ya wanafunzi kila mwaka bila kuwepo kwa suluhisho la kudumu kuhusu mustakabali wa wahitimu wa programu hizi. Juhudi mbalimbali za kufuatilia na kutafuta ufumbuzi zimefanyika, lakini hadi sasa hazijazaa matunda yanayotarajiwa.
Hivyo basi, tunaomba kwa heshima mamlaka husika, ikiwemo vyombo vya serikali na taasisi zinazohusika na usajili wa wahandisi, kulifanyia kazi suala hili kwa haraka ili wahitimu wa programu hizi watambulike ipasavyo na kupata fursa za ajira zinazostahili. Aidha, tunaomba MUST pia itafute suluhisho la kudumu la changamoto hii kabla ya kuendelea kudahili wanafunzi wengi katika programu husika.
“Elimu inayotolewa inapaswa kuendana na fursa za ajira na utambuzi wa kitaaluma ili kulinda maslahi ya wanafunzi na maendeleo ya taifa.”