SoC02 Wahitimu wa Ualimu wajitolee kufidia uhaba wa Walimu, na wenye kigezo hiko wapewe kipaumbele cha ajira

SoC02 Wahitimu wa Ualimu wajitolee kufidia uhaba wa Walimu, na wenye kigezo hiko wapewe kipaumbele cha ajira

Stories of Change - 2022 Competition

Mrope11

Member
Joined
Jul 18, 2022
Posts
13
Reaction score
3
Uhaba wa walimu.

Ripoti ya takwimu muhimu za Tanzania ya mwaka 2019 iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu inaonesha shule mbalimbali za Msingi za serikali inaonesha kuwa mwaka 2018 shule za serikali zilikuwa na walimu 191771 ila kwa mwaka uliofuata wa 2019 walipungua hadi walimu 188336 kabla ya kushuka zaidi hadi walimu 182002 mwaka 2020 ambapo ni upungufu wa walimu 9769.

Kwa takwimu za wanafunzi na walimu wa shule za serikali waliokuwepo kwa mwaka 2019 ni sawa na kusema mwalimu mmoja alikuwa anafundisha wanafunzi 56 katika darasa ambapo ni juu ya wastani unaopendekezwa na serikali wa mwalimu mmoja kufundisha wanafunzi 45.



Sababu za Upungufu wa walimu

- Udahili wa wanafunzi katika shule za Msingi za serikali na binafsi Tanzania bara umekuwa ukiongezeka kila mwaka tangu mwaka 2016,ripoti hiyo inaeleza kuwa kwa mwaka 2019 wanafunzi million 10.6 waliandikishwa katika shule za msingi ikilinganishwa na wanafunzi million 8.3 walioandikishwa mwaka 2015.Katika hao wanafunzi million 10.6 walioandikishwa mwaka 2019 asilimia 96 wanatoka katika shule za umma na hii inatajwa kuchangiwa na sera ya elimu bila malipo na ongezeko la uandikishwaji wa wanafunzi limeshindwa na kuendana na uhitaji wa walimu hivyo kupelekea uchache wa walimu kutokana na idadi ya wanafunzi waliopo.

-Sera ya elimu na mafunzo ya ufundi ya mwaka 2014 iliyotolewa na wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia inataja sababu ya kupungua kwa idadi ya walimu ni kupanuka kwa sekta nyingine zenye maslahi mazuri,baadhi ya walimu wamekuwa wakiacha kazi ya ualimu na kujiunga na sekta ambazo zinavutia kimaslahi na kimazingira.

-Mwaka 2017 wakati idadi ya walimu ikiendelea kupungua ndio kipindi ambacho serikali iliendesha zoezi la uhakiki wa watumishi wa umma nchi nzima,ambapo walimu 3655 walibainika kuwa na vyeti vya kughushi na kupoteza sifa ya kuwa watumishi wa umma.

-Ripoti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (nbs) inaonesha kuwa mwaka 2019 kulikuwa na vyuo vya ualimu 88 vilivyopungua kutoka vyuo 137 vilivyokuwepo mwaka 2018 kutokana na kufungwa kwa vyuo 49 vilivyokuwa vinamilikiwa na watu binafsi hivyo tutakubaliana kwamba uzalishaji wa walimu hapo huenda ukawa umepungua.


Tatizo la ajira nchini Tanzania.

Suala la changamoto ya ajira sio tu kwa walimu bali hata katika nyanja nyingine na suala hilo halikuanza leo hivyo serikali kwa muda mrefu imeonekana kukosa suluhu ya kudumu,mfano ripoti ya tume ya taifa ya takwimu kupitia utafiti wake wa nguvu kazi nchini uliofanyika mwaka 2014 iligundua kwamba ,jumla ya wahitimu 65614 hawakuwa wamejiajiri wala kuajiriwa kwenye sekta yoyote ya ajiri mwaka huo.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2016 inaonesha kwamba kila mwaka vijana 700,000 nchini Tanzania wanahitimu masomo katika ngazi mbalimbali za elimu ambapo ni fursa 40,000 tu ndio huwa ajira za moja kwa moja hii ikimaanisha kwamba ni asilimia 6 tu ya vijana ndio ambao wanapata kazi rasmi.


Athari za uhaba wa walimu.

-
Kupata wahitimu wasiokidhi sifa na vigezo.Mfano ripoti ya shirika lisilo la kiserikali la Haki Elimu yam waka 2012 ilionesha wanafunzi 5200 waliojiunga na kidato cha kwanza mwaka huo walikuwa hawajui kusoma wala kuandika,Pia kupitia Ukaguzi uliofanywa na Wizara ya Elimu katika shule 6,831 za msingi mwaka 2015/16 umebaini kuwepo kwa wanafunzi 10,273 wasiojuajua kusoma wala kuandika.

Hii inamaanisha tunaweza kuzalisha vijana ambao watakosa sifa za kuweza kuajiriwa kwa sababu wanafunzi watashindwa kumaliza syllabus kutokana na idadi ya walimu iliyopo au walimu wanaweza kufundisha juu juu kwa maana ya bora liende ambapo mwishowe mwanafunzi anaweza asinufaike sana


Nini kifanyike?

-Kwanza serikali iweke kigezo cha uzoefu wa kazi kwa walimu kabla ya kuajiriwa awe amefundisha angalau mwaka mmoja hususani katika shule za serikali,hii itafanya walimu wote wanaotoka v yuoni kwenda kuongeza nguvu na kupunguza uhaba wa walimu.

-Dhana ya elimu bure iangaliwe upya,kwani awali kuzuiwa kwa michango mashuleni ilipelekea wazazi wengine kutoa visingizio pale wanapotakiwa kuchangia walimu wa ziada na wao wamekuwa wakijibu bila tabu,”Elimu Bure”

-Walimu waboreshewe maslahi na kutengenezewa mazingira mazuri ya kazi, hii itawapeleka walimu wapate moyo na kuongeza jitihada katika kufundisha na kizazi kinachoinukia kitatamani nao wasomee fani hiyo,ila kama akikua akikuta walimu masikini wataona hiyo kazi haiwafai kwa siku zijazo,maana bila hivyo itapalekea miaka mingi ijayo kada hiyo ikaja kuwa na upungufu wa watu.

-Serikali iajiri kulingana na,idadi ya walimu wanaoacha,na wanaostaafu.

-Kuwekwe kodi maalumu ambayo itakatwa kutoka kwa wabunge kwa ajili ya mfuko maalumu wa walimu,mfuko ambao utasaidia kuajiri walimu wapya,maslahi yao pamoja na uboreshaji wa miundombinu mingine.
 
Upvote 1
kaa kwakutulia ww, Elimu ni biashara Amnaga biashara yahivyo imagine zaidi ya mil20 umewekeza mpaka chuo then ukafanye kaz bure!!😳
anyway ukajitolee ww &wenzako
 
Hili nakupinga kwa 100%. Mtu ajitolee bure wote wakijitolea utawaajiri kwa pamoja.? Na watu wanamipango yao wengine wanafamilia watazileaje ikiwa wanajitolea bure.? Kwangu mimi hili ni BIG NO
 
Hili nakupinga kwa 100%. Mtu ajitolee bure wote wakijitolea utawaajiri kwa pamoja.? Na watu wanamipango yao wengine wanafamilia watazileaje ikiwa wanajitolea bure.? Kwangu mimi hili ni BIG NO

kaa kwakutulia ww, Elimu ni biashara Amnaga biashara yahivyo imagine zaidi ya mil20 umewekeza mpaka chuo then ukafanye kaz bure!!😳
anyway ukajitolee ww &wenzako
''Of course akili na elimu vinatofautiana'' EINSTEIN Ila mifumo ya ajira inataka uzoefu labda kama hujawahi kufanya interview ya kazi hadi ila unaposubiri ajira unatafuta expreience ya kazi,kama utajitolea au utajishikiza sehemu ni wewe tu,ajira za karibu hata zila za muda mfupi mfano kusimamia uchaguzi na sensa wamechukua watu wanaojitolea,tukisema ajira ni neno pana sana,kuna za muda mfupi na mrefu,sasa inategemea na wewe hiyo mill 20 ulisomea nini
 
Hili nakupinga kwa 100%. Mtu ajitolee bure wote wakijitolea utawaajiri kwa pamoja.? Na watu wanamipango yao wengine wanafamilia watazileaje ikiwa wanajitolea bure.? Kwangu mimi hili ni BIG NO
Sijui umesoma heading tu,au unafikiria nitashinda,maana waswahili nanyi,lengo langu sio tu kushinda bali ku create awareness kwenye jambo lenye human interest kwa wananchi.Kama ulishawahi kufanya interview ya kazi unaulizwa uzoefu sasa sijui kwako mwenzetu ila wahitimu wengi wnapomaliza wametakiwa kufanya kazi kutafuta uzoefu kwa sababu kuna watu wana mwaka wa 5 sasa nyumbani taaluma kama mwalimu akiwa nje kwa miaka 6 anapoteza sifa,naruhusu kupinga lakini ni haki yako.
 
Yani kwangu Mimi kujitoleà kwa kazi ya ualimu hicho ni kipengele. Sikusoma bure.

Kama ñi taàluma kupotea acha ipotee kabisà
 
Back
Top Bottom