A
Anonymous
Guest
Wahitimu wa Kozi ya Basic Driving katika chuo cha IFDC kilichopo Ikwiriri, Wilaya ya Rufiji, Mkoa wa Pwani. Chuo hiki kilianzishwa kwa juhudi za Mbunge na Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa, na kinatambulika na VETA.
Changamoto yangu ni kwamba tangu tumalize kozi hiyo, takribani miezi saba imepita bila kupata vyeti vyetu. Tunapowauliza uongozi, tunaambiwa vyeti vinatengenezwa, lakini muda umekuwa mrefu bila kupata ufumbuzi. Hata wahitimu waliotutangulia walikumbana na changamoto kama hii.
Kupitia JamiiForums, tunaomba msaada wa kufikisha hoja hii kwa wahusika ili vyeti vyetu vitolewe kwa wakati, kwani kuchelewa huko kunatukwamisha kuendelea na hatua zinazofuata za maisha na taaluma yetu.