A
Anonymous
Guest
Sisi ni wahitimu wa mafunzo ya udereva kutoka Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Ikwiriri, kilichopo Wilaya ya Rufiji, Mkoa wa Pwani.
Tunahitimu mafunzo mwezi Aprili 2026 na kufaulu vizuri. Tayari tumepatiwa vyeti vya kuhitimu, lakini tunapokwenda TRA kwa ajili ya kupata leseni za udereva, tunaambiwa kuwa chuo chetu hakipo kwenye mfumo.
Tumejaribu mara kadhaa kuwasiliana na uongozi wa chuo ili kutatua changamoto hii, lakini tumekuwa tukipewa ahadi kwamba suala hilo litashughulikiwa na chuo kitawekwa kwenye mfumo. Hata hivyo, hadi sasa hakuna hatua iliyochukuliwa na bado hatujapata leseni zetu.
Tangu Aprili 2026 hadi sasa, tumeshindwa kupata leseni licha ya kuwa tumemaliza mafunzo na kufaulu. Hali hii imekwamisha mipango yetu mingi, hasa kwa wale waliokuwa wanategemea leseni hizi kupata ajira na kuanza shughuli za kujikwamua kiuchumi.
Tunaomba mamlaka husika zitusaidie kulifuatilia na kulitatua suala hili haraka, ili juhudi na muda tuliowekeza katika mafunzo zisiwe bure na tuweze kutumia taaluma yetu kujenga maisha yetu.
Mhitimu wa Mafunzo ya Udereva,
Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Ikwiriri.
Ahsante.