SoC01 Wahitimu wa Vyuo na Maisha ya utafutaji Mtaani

SoC01 Wahitimu wa Vyuo na Maisha ya utafutaji Mtaani

Stories of Change - 2021 Competition

Theb

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2019
Posts
3,927
Reaction score
7,276
Habari zenu wana Jamii Forums, hususani jukwaa hili la "Stories of Change". Ni tumaini langu wote ni wazima.

Andiko hili litaangazia maisha ya vijana wahitimu wa vyuo waliotegemea kuajiriwa na hali imekua tofauti na matarajio yao. Mwanzo, nitaelezea maisha ya mtaani, changamoto zinazo wakabili na vipi watatue hizo changamoto, Pili, nitaelezea fursa zisizohitaji mitaji na zenye kuhitaji mitaji. Tatu, nitaelezea mchango wa serikali na sekta binafsi katika kuwasaidia vijana kupata ajira na kujiajiri. Mwisho, nitamalizia kwa kutoa ushauri wangu katika kuwawezesha vijana wahitimu kujikwamua.

Maisha ya mtaani katika jamii zetu karibia kote yana mfanano kwa asilimia kubwa. Kuanzia ngazi ya familia za wahitimu walio wengi zinafanana kiuchumi, kitamaduni na hata kimalengo. Familia nyingi katika jamii zetu Tanzania tunasoma ili tuajiriwe na sio kujiajiri kwa waliowengi, hali iliyopo kwa sasa imeenda kinyume na malengo na matarijio ya vijana waliokuwa wanasoma na wanaoendelea kusoma mashuleni mpaka vyuoni.

CHANGAMOTO ZINAZO WAKABILI VIJANA WAHITIMU KATIKA UTAFUTAJI.

1. Kushindwa kujiamini na kushindwa kuikubali hali halisi iliyopo. Wengi wameshindwa kujiamini na kufikiria nje ya kitu walichosomea na kuanza kitu kipya ina wawia ngumu.

2. Mazingira yanayo wazunguka wahitimu, jamii ina wapa wakati mgumu kwa kuwahukumu kuwa wamesoma bure, elimu yao haina faida. Hili sio sawa.

3. Ukosefu wa muunganiko baina ya wahitimu na waliotangulia kwenye utafutaji, hapa unakuta wahitimu hawana muunganiko na waliotangulia kwenye utafutaji mitaani.

4. Ukosefu wa mitaji, hususani kwenye biashara au fursa zinazohitaji mitaji.

5. Kukosa uelewa katika utafutaji wenyewe. Kutozijua fursa au kutozitambua biashara na majira yake. Maana kila biashara ina majira yake.

6. Kuchagua kazi. Baadhi ya wahitimu hii changamoto kubwa kwao. Hawako tayari kubeba hata mizigo wanaona aibu au wanaona haiba yao hawastahili kubeba mizigo.

7. Mfumo na mitaala ya elimu nchini haikidhi dhumuni la kujiajiri kwa sababu imejikita katika nadharia zaidi na sio hali halisi katika kujiajiri.

JINSI YA KUPAMBANA NA HIZO CHANGAMOTO:-

1. Wazazi wasaidie watoto wao kuchagua fani zitakazo wawezesha kujiajiri pindi watakapo hitimu vyuoni.

2. Kujikubali, kujitambua na kujichanganya na watafutaji wengine mitaani bila kuwaza au kujutia muda uliopoteza shuleni na vyuoni.

3. Kukubali hali halisi hususani kuwa tayari kwa kazi yoyote bila kuchagua kazi. Mfano baadhi ya wahitimu ni ngumu kufanya kazi kama kuuza mkaa au kununua chupa za plastiki zilizotumika kwa kuhofia taaluma yake au watu watamuonaje.

4. Kuzitambua fursa na kuwa tayari kupambana nazo maana utafutaji mtaani ni ushindani.

5. Kufanya uchunguzi wa biashara unayotaka kwenda kuanzisha, hapa itahitaji kutafiti kwa kile unachotaka kufanya mtaani.

6. Kupunguza matumizi yale yasiyo muhimu. Kuwa na matumizi sahihi ya fedha. Mfano waache unywaji wa pombe, kubet, uvutaji wa sigara au ulevi wowote na anasa zingine zinazo hitaji pesa.

7. Kufanya uchaguzi sahihi wa kile unachoweza kukifanya mtaani na sio kufuata mkumbo. Fanya unachokipenda na unachokiweza

8. Usisahau kutunza kile unachokipata hata kama kidogo. (Bandu bandu humaliza gogo)

FURSA ZINAZOWEZA KUSAIDIA WAHITIMU KATIKA UTAFUTAJI MTAANI

1. Fursa zisizo hitaji mitaji na zisizo hitaji mitaji mikubwa sana. (Hizi kwa ajili ya kuanza kujipatia mitaji kidogo kidogo)

(i) Vibarua viwandani
Kwa wale wahitimu waliopo mijini kuna viwanda, vipo vibarua vya kutwa na wale wanaolipwa kwa wiki viwandani. Kuna kubeba mizigo viwandani kupakia na kupakua mizigo inayoingia na inayotoka na kazi zingine kulingana na kiwanda husika.

(ii) Fursa kwenye standi za mabasi ya abiria
Pia kwenye standi za mabasi kuna baadhi ya fursa zisizohitaji mitaji au zinazohitaji mitaji midogo. Mfano kubeba mizigo ya abiria kuwa wakala wa kukata tiketi na kuunza bidhaa ndogo ndogo kama karanga maji, juisi na matunda.

(iii) Kununua plastiki na kwenda kuziuza
Hapa kuna hii fursa ya kununua plastiki na kwenda kuuza mfano kilo moja unanunua kuanzia 300 hadi 400 na kuuza iliyosagwa ni kuanzia 800 hadi 1200 isiyo sagwa ni 800 bei ya kuuza. Hii ni fursa japo inadharauliwa.

(iv) Kuwa dalali wa mazao shambani au magari ya kusafirisha mizigo au dalali wa nyumba na viwanja
Haihitaji mtaji kwenye kuanza uaminifu wako na kujua chimbo za unachofanya ndio mtaji wako.

(v) Kuanzisha twisheni (tuition) mtaani kwenu
Hii pia saa zingine haihitaji mtaji itahitaji tu utayari wako na uwepo wa wanafunzi wanaosoma na kuitangaza. Japo maeneo mengine hii haina nafasi maana muitiko unakua mdogo hasa vijijini.

(vi) Kubeba mizigo kwenye masoko kupakua na kupakia mazao na bidhaa mbalimbali
Tunaweza kuidharau lakini ni fursa ukibeba mizigo 25 yenye kulipwa 1000 kila mzigo kwa siku una shilingi 25000. Haitaki mtu mwenye aibu na usharobaro.

(v). Kipaji kiwe cha uandishi, uimbaji, ususi, uchoraji, na michezo
Kipaji pia ni fursa kubwa tena isiyo hitaji mtaji ila inahitaji utayari wako kujituma na ubunifu zaidi na uvumilivu uliomithilika.

(vi). Kuwa saidia fundi ujenzi, fundi wa kuchomelea dirisha na mageti, fundi randa nk,

Kusaidia fundi atakulipa kidogo itategemea na kazi iliyopo hapo unajifunza ufundi, kujiandaa kuwa fundi ili ujitegemee. Mfano saidia fundi ujenzi hulipwa sio chini ya 10,000/= kwa siku.

(vii). Kuuza mahindi ya kuchoma na ya kuchemsha.
Hii hususani sehemu zenye mikusanyiko, stand za mabasi, barabarani na kwenye vyombo vya usafiri hususani mabasi.


2. Fursa zinazohitaji mitaji mikubwa au ya kiasi. Nitataja baadhi na ambazo ni rahisi kuzitambua kama ifuatavyo:-

(i). Kununua mazao mashambani na kuleta mjini kwenye masoko
Hapa kuna mahindi, viazi aina zote, mchele mboga mboga kutoka mashambani kuleta mijini. Kikubwa kufanya tathmini vizuri.

(ii). Umachinga wa kuuza vitu mtaani kando ya barabara au kutembeza au kutengeneza banda lako sehemu inayoonekana kwa wateja

(iii). Kilimo, uvuvi na ufugaji

Kilimo kinahitaji uwe na shamba, mbegu, pembejeo za kilimo mbolea na dawa za kupulizia kuua vijidudu hatarishi kwa mazao nacho kilimo kitategemea na aina ya mazao unayolima.

Ufugaji
Mfano wa kuku lazima uwe na mtaji wa kununua kuku, pumba, uduvi na mifupa.

(iv). Udereva boda boda au bajaji
Huu nao utahitaji uwe na mtaji au upate ya mtu. Mfano bado boda hakosi kupata 25000 hadi 30000 kwa siku.

(v). Kuanzisha saloon zote za kunyoa nywele na kusuka nywele
Hapa kwa wanaume na kwa wanawake kuna kunyoa na kusuka hivyo sehemu uliyopo ikiwa na uhitaji hii ni fursa.

(vi). Huduma ya kutuma pesa kwa njia za simu.
Kuanzisha M pesa, airtel money, tigo pesa na halopesa.

(vii). Kuanzisha mgahawa, mama ntilie au ukaangaji wa chipsi na kuchoma mishkaki.

(viii). Kununua na kuuza vyuma chakavu. Hii pia ni fursa inayolipa vizuri ni jambo la kufanya uchunguzi na kuthubutu.


MCHANGO WA SERIKALI PAMOJA NA SEKTA BINAFSI KATIKA KUWASAIDIA WAHITIMU.

1. Kuwapa motisha, semina na muongozo wa namna ya kuanza ujasiriamali.

2. Kuwapatia mikopo yenye riba nafuu au isiyo na riba kabisa.(walemavu wapewe kipaumbele).
Serikali na sekta binafsi kupitia benki na taasisi zingine za kifedha watoe mikopo kwa wahitimu. Pia familia zenye uwezo ziwawezeshe vijana wao waliohitimu.

3. Mazingira wezeshi kwa watafutaji wanaoanza kutafuta mtaani. Hapa kuwaondolea kodi kandamizi. Kuboresha miundo mbinu zaidi mijini na vijijini itasaidia usafirishaji wa bidhaa.

4. Serikali itengeneze mahusiano mazuri na mataifa mengine. Itasaidi kutanua soko la nje kwenye ajira na bidhaa au mazao yatakayo zalishwa nchini.

5. Serikali na sekta binafsi zinapaswa kwa pamoja kuwaamini vijana na kuondoa kigezo cha uzoefu katika kuwapatia kazi/ajira.

6. Serikali na sekta binafsi ziwashirikishe vijana katika juhudi za kuwainua iwe mikopo au semina za kiujasiriamali.

7. Mfumo wa elimu uboreshwe hususani mitaala. Elimu itolewe kwa vitendo na ijikite katika kuwaandaa kujitegemea/kujiajiri.

8. Wazazi, jamii, serikali na mashirika binafsi kwa pamoja watambue na kudhamini karama au vipaji vya wanafunzi toka wakiwa wadogo na kuvisimamia kwa lengo la kujiajiri baadae.

9. Wahitimu wote wenye ulemavu wapatiwe kazi serikalini na mashirika binafsi moja kwa moja. Mfano ajira za mwaka 2021 ualimu na afya serikali haikuwaacha nyuma hili liendelee kila wakati.

10.Kuwe na uwazi katika masuala ya ajira. Iwe za serikali mpaka mashirika binafsi.

11. Ukabila, rushwa, umaeneo na udini viepukwe katika kuwapatia vijana ajira.

12. Waliofikia umri wa kustaafu wasiruhusiwe kuendelea kufanya kazi.

13. Uwepo mgawanyo wa kazi.
Ili mtu mmoja asifanye kazi zaidi ya kituo kimoja.

USHAURI WANGU KWA VIJANA WAHITIMU KATIKA UTAFUTAJI
Ushauri wangu kwa vijana wasaka tonge wahanga wa ajira na vijana woote watafutaji kwa ujumla napenda kutoa ushauri kama ifuatavyo:-

(i). Uvumilivu kwenye hizo fursa tunazoenda kuanzisha maana nako pia tutakutana na changamoto ila tusivunjike moyo na tusikate tamaa mapambano yaendelee.

(ii). Tuzijue hizo fursa na kutambua majira ya hizo fursa itasaidia kutambua muda gani muafaka wa kuanza tusikurupuke kuna kuanguka pia.

(iii). Kama unamtaji usianze na pesa yote ya mtaji maana hauna uhakika 100% kuwa itaenda sawa hivyo kujipanga kwa hilo ni muhimu.

(iv). Kupata ushauri kwa waliofanikiwa ni muhimu itakuongezea maarifa kwa yale usiyo yajua.

(v). Usimuamini kila mtu katika utafutaji wako wengine watakukwamisha. Mfano wanao kopa ni sumu kwako unaeanza utafutaji.

(vi). Tambua hitaji la jamii ikizungukayo. Kama jamii inataka mahindi wapelekee mahindi na sio mchele.

(vii). Ishi vizuri na watu na waheshimu watu kwa imani zao makabila yao na rangi zao. Kuwa na lugha nzuri.

(viii). Zingatia usafi kwenye ofisi yako kuwa na mpangilio mzuri pia toa huduma iliyo bora sio bora huduma.

(ix). Muhimu na la kukumbukwa kila unapopata kidogo kitunze kadri kinavyo kua kiwekeze kitaleta zaidi.

(X). Fanya shughuli halali, kuwa muaminifu, uadilifu ni muhimu na kufuata sheria za nchi yetu katika utafutaji.
 
Upvote 1.6K
MTAPOTEANA WENGINE WANAONDOKA NA BUMU HUKO CHANGAMOTO ZOTE HAWANA.... MAANA WANAPOKEA BUMU KILA MWEZI
Sawa boom ni kwa ajili ya matumizi ya kila cku. Na boom.sio.mshahara ndugu. Na sio wahitimu wote wanaopata boom. Wapo wahitimu wa certificate , diploma na degree ambao hawana boom.

Kwa ujumla boom sio.mshahara bali matumizi sahihi ndio yanayozingatiwa. Mwanachuo akiweza kujibana itamsaidia kukikwamua. Wapo wanaolea ndugu na kusomesha wadogo zao kwa hilo hilo boom hivyo tuongee kilichopo hapa. Fungua uzi unaoelezea matumizi.ya boom
 
BUMU HUGEUKA KUWA MSHAHARA TAFUTA TAARIFA UTAJUA TU

Boom sio mshahara mzee baba. Na story za boom zitoe hapa huu uzi ni kwa ajili ya wahitimu wote mzee umeuelewa au bado..?
 
HILO TATIZO LAKO WENZAKO WAKIHITIMU WANAPATA ALLOWANCE KAMA ILIVYO BOOM LABDA KAMA ULIKUWEPO CHUONI KWA AJILI YA KLUVUNJIWA MAHUSIANO WATU WANAKULA ALLOWANCE ZAO BILA KELELE MAANA KUNA GADAFI
Tunaongea habari za kujiajiri hapa wewe unaleta habari za boom. Umeuelewa uzi mkuu..? Rudia kusoma tena.??
 
WEWE UNAWAZA KUJIAJIRI WENZAKO WANAWAZA KUPATA HELA ZA KUPOTEZA SIKU MZEE BABA VP? KUFIKILIA WATU NI UGONJWA SIKU HIZI CORONA HAFADHARI TANZANIA KUNA ULAYA - OSTABAY MFANO PAMOJA NA WATU WA KUTAFUTA TAARIFA....

BADO TUNATAFUTA MAANA YA KAZI NDIO MAANA ELEWA HUYU KIONGOZI WENU/WETU UKIPENDA

Mkuu kale ukalale hujaelewa nilichoandika naona unajibu vitu tofauti tofauti huu uzi umetumia kiswahili chepesi nakuona sio muelewa kaurudie kuusoma vzr mkuu maana unaandika vitu havieleweki vinajipanda juu juu mara gadafi mara corona mara heueleweki. I'm sorry[emoji1317] nashukrani kwa mchango wako hapa
 
HAYEEE ULIZANI KAZI KUELEWA TUNASOMA ILA TUFANYEJE KAMA KUNA NJAAA WAHITIMU TUNAENDA KUPATA ALLOWANCE NA KUTULIA NYUMBANI KUWAZA KIONGOZI KAONGEA NINI
Andiko lina husu kuleta mabadiliko ya kimaendeleo kwenye jamii zetu wewe unataka kutuambia tukaa tu nyumbani tutapigaje hatua..? Huwezi kupata ikiwa hutafuti. Fikra zako zinahitaji ujifunze na uondoe hiyo hali ya kuamini porojo za kuletewa allowance kitu ambacho maongea huyo ndugai na hakipo katika utekelezaji na hakiwezi kutekelezwa. Amka acha kuendelea kuwaza mambo ambayo ni ya kusadikika
 
HIYO VITA NI YA UJERUMANI ITASHIA KWA SULTANI
usipo kubali kujifunza kamwe huwezi kujifunza.
Na usipoamka kutafuta sahau kuhusu kufanikiwa iwe kwa kitu chochote. Ushauri na usemalo ni kitu kibovu kuwaaminisha wahitimu. Lazima watu watafute maana maisha ni mapambano.
 
Hakika mimi pia muhitimu na mhanga wa hili la ajira ila napambana na kila nafasi ninayoipata nishauza mkaa kwa kuajiriwa na mtu. Waty wanaojua nimehitimu chuo walikua wananishangaa lakini sijawahi.kuogopa hilo

Sent using Jamii Forums mobile app
Hebu toa mwanga zaidi kwa wengine...hiyo biashara ya mkaa unaifanya kwa ubora kiasi gani tofauti na ambaye hajasoma?

Maana yangu ni kwamba elimu uliyonayo umeitumiaje kuboresha maisha yako kwa chochote ufanyacho?
 
Hebu toa mwanga zaidi kwa wengine...hiyo biashara ya mkaa unaifanya kwa ubora kiasi gani tofauti na ambaye hajasoma?

Maana yangu ni kwamba elimu uliyonayo umeitumiaje kuboresha maisha yako kwa chochote ufanyacho?
Vzr ilikua ni.ofisi ya mtu analeta mimi nauza yaani kama ananikopesha mzigo. Bei ya kushusha 3400 inaweza kuzidi na kuchanga sasa inaweza kufikia hata 4000, 4200, itategemea na uhutaji na aina ya mkaa na ubora wake ni kazi iliyoniwezesha kujikimu mjini hapa maana ndio ilikua inanipatia kila senti ninayotumia kuanzia kula kulipa kodi kuvaa na majukumu mengine

Faida ipo na ukiwa sehemu yenye mzunguko mzuri gunia inakuletea mpaka saa zingine 10000 faida hivo ukiwa na uhakika wawateja wakuuza gunia 4 kwa siku afu makisio tu ya chini iwe faida kila gunia 6000 kwa 4 una jumla ya 24000 toa kula na usafiri unauhakika wakuweka 15000 per day hapo huja jikwamua kweli..?
 
Serikali inatakiwa kuwekeza nguvu kubwa kwa vijana hasa wale wahitimu wa kada mbali mbali kwa kuwaandalia mazingira wezeshi pindi wanapomaliza masomo yao, iwe kwa kuwapatia mitaji au kuwapa ajira, serikalini ama sekta binafsi
 
Serikali inatakiwa kuwekeza nguvu kubwa kwa vijana hasa wale wahitimu wa kada mbali mbali kwa kuwaandalia mazingira wezeshi pindi wanapomaliza masomo yao, iwe kwa kuwapatia mitaji au kuwapa ajira, serikalini ama sekta binafsi
Kweli. Serikali na sekta binafsi zina hitajika kwa pamoja kuwapatia vijana wahitimu mikopo na kuwapa semina za kujua namna ya kujiajiri.
 
Kweli. Serikali na sekta binafsi zina hitajika kwa pamoja kuwapatia vijana wahitimu mikopo na kuwapa semina za kujua namna ya kujiajiri.
Kabisa vinginevo tutaendelea kuwa na rundo kubwa la vijana wasiokua na ajira
 
Back
Top Bottom