SoC01 Wahitimu wa Vyuo na Maisha ya utafutaji Mtaani

Stories of Change - 2021 Competition

Theb

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2019
Posts
3,927
Reaction score
7,276
Habari zenu wana Jamii Forums, hususani jukwaa hili la "Stories of Change". Ni tumaini langu wote ni wazima.

Andiko hili litaangazia maisha ya vijana wahitimu wa vyuo waliotegemea kuajiriwa na hali imekua tofauti na matarajio yao. Mwanzo, nitaelezea maisha ya mtaani, changamoto zinazo wakabili na vipi watatue hizo changamoto, Pili, nitaelezea fursa zisizohitaji mitaji na zenye kuhitaji mitaji. Tatu, nitaelezea mchango wa serikali na sekta binafsi katika kuwasaidia vijana kupata ajira na kujiajiri. Mwisho, nitamalizia kwa kutoa ushauri wangu katika kuwawezesha vijana wahitimu kujikwamua.

Maisha ya mtaani katika jamii zetu karibia kote yana mfanano kwa asilimia kubwa. Kuanzia ngazi ya familia za wahitimu walio wengi zinafanana kiuchumi, kitamaduni na hata kimalengo. Familia nyingi katika jamii zetu Tanzania tunasoma ili tuajiriwe na sio kujiajiri kwa waliowengi, hali iliyopo kwa sasa imeenda kinyume na malengo na matarijio ya vijana waliokuwa wanasoma na wanaoendelea kusoma mashuleni mpaka vyuoni.

CHANGAMOTO ZINAZO WAKABILI VIJANA WAHITIMU KATIKA UTAFUTAJI.

1. Kushindwa kujiamini na kushindwa kuikubali hali halisi iliyopo. Wengi wameshindwa kujiamini na kufikiria nje ya kitu walichosomea na kuanza kitu kipya ina wawia ngumu.

2. Mazingira yanayo wazunguka wahitimu, jamii ina wapa wakati mgumu kwa kuwahukumu kuwa wamesoma bure, elimu yao haina faida. Hili sio sawa.

3. Ukosefu wa muunganiko baina ya wahitimu na waliotangulia kwenye utafutaji, hapa unakuta wahitimu hawana muunganiko na waliotangulia kwenye utafutaji mitaani.

4. Ukosefu wa mitaji, hususani kwenye biashara au fursa zinazohitaji mitaji.

5. Kukosa uelewa katika utafutaji wenyewe. Kutozijua fursa au kutozitambua biashara na majira yake. Maana kila biashara ina majira yake.

6. Kuchagua kazi. Baadhi ya wahitimu hii changamoto kubwa kwao. Hawako tayari kubeba hata mizigo wanaona aibu au wanaona haiba yao hawastahili kubeba mizigo.

7. Mfumo na mitaala ya elimu nchini haikidhi dhumuni la kujiajiri kwa sababu imejikita katika nadharia zaidi na sio hali halisi katika kujiajiri.

JINSI YA KUPAMBANA NA HIZO CHANGAMOTO:-

1. Wazazi wasaidie watoto wao kuchagua fani zitakazo wawezesha kujiajiri pindi watakapo hitimu vyuoni.

2. Kujikubali, kujitambua na kujichanganya na watafutaji wengine mitaani bila kuwaza au kujutia muda uliopoteza shuleni na vyuoni.

3. Kukubali hali halisi hususani kuwa tayari kwa kazi yoyote bila kuchagua kazi. Mfano baadhi ya wahitimu ni ngumu kufanya kazi kama kuuza mkaa au kununua chupa za plastiki zilizotumika kwa kuhofia taaluma yake au watu watamuonaje.

4. Kuzitambua fursa na kuwa tayari kupambana nazo maana utafutaji mtaani ni ushindani.

5. Kufanya uchunguzi wa biashara unayotaka kwenda kuanzisha, hapa itahitaji kutafiti kwa kile unachotaka kufanya mtaani.

6. Kupunguza matumizi yale yasiyo muhimu. Kuwa na matumizi sahihi ya fedha. Mfano waache unywaji wa pombe, kubet, uvutaji wa sigara au ulevi wowote na anasa zingine zinazo hitaji pesa.

7. Kufanya uchaguzi sahihi wa kile unachoweza kukifanya mtaani na sio kufuata mkumbo. Fanya unachokipenda na unachokiweza

8. Usisahau kutunza kile unachokipata hata kama kidogo. (Bandu bandu humaliza gogo)

FURSA ZINAZOWEZA KUSAIDIA WAHITIMU KATIKA UTAFUTAJI MTAANI

1. Fursa zisizo hitaji mitaji na zisizo hitaji mitaji mikubwa sana. (Hizi kwa ajili ya kuanza kujipatia mitaji kidogo kidogo)

(i) Vibarua viwandani
Kwa wale wahitimu waliopo mijini kuna viwanda, vipo vibarua vya kutwa na wale wanaolipwa kwa wiki viwandani. Kuna kubeba mizigo viwandani kupakia na kupakua mizigo inayoingia na inayotoka na kazi zingine kulingana na kiwanda husika.

(ii) Fursa kwenye standi za mabasi ya abiria
Pia kwenye standi za mabasi kuna baadhi ya fursa zisizohitaji mitaji au zinazohitaji mitaji midogo. Mfano kubeba mizigo ya abiria kuwa wakala wa kukata tiketi na kuunza bidhaa ndogo ndogo kama karanga maji, juisi na matunda.

(iii) Kununua plastiki na kwenda kuziuza
Hapa kuna hii fursa ya kununua plastiki na kwenda kuuza mfano kilo moja unanunua kuanzia 300 hadi 400 na kuuza iliyosagwa ni kuanzia 800 hadi 1200 isiyo sagwa ni 800 bei ya kuuza. Hii ni fursa japo inadharauliwa.

(iv) Kuwa dalali wa mazao shambani au magari ya kusafirisha mizigo au dalali wa nyumba na viwanja
Haihitaji mtaji kwenye kuanza uaminifu wako na kujua chimbo za unachofanya ndio mtaji wako.

(v) Kuanzisha twisheni (tuition) mtaani kwenu
Hii pia saa zingine haihitaji mtaji itahitaji tu utayari wako na uwepo wa wanafunzi wanaosoma na kuitangaza. Japo maeneo mengine hii haina nafasi maana muitiko unakua mdogo hasa vijijini.

(vi) Kubeba mizigo kwenye masoko kupakua na kupakia mazao na bidhaa mbalimbali
Tunaweza kuidharau lakini ni fursa ukibeba mizigo 25 yenye kulipwa 1000 kila mzigo kwa siku una shilingi 25000. Haitaki mtu mwenye aibu na usharobaro.

(v). Kipaji kiwe cha uandishi, uimbaji, ususi, uchoraji, na michezo
Kipaji pia ni fursa kubwa tena isiyo hitaji mtaji ila inahitaji utayari wako kujituma na ubunifu zaidi na uvumilivu uliomithilika.

(vi). Kuwa saidia fundi ujenzi, fundi wa kuchomelea dirisha na mageti, fundi randa nk,

Kusaidia fundi atakulipa kidogo itategemea na kazi iliyopo hapo unajifunza ufundi, kujiandaa kuwa fundi ili ujitegemee. Mfano saidia fundi ujenzi hulipwa sio chini ya 10,000/= kwa siku.

(vii). Kuuza mahindi ya kuchoma na ya kuchemsha.
Hii hususani sehemu zenye mikusanyiko, stand za mabasi, barabarani na kwenye vyombo vya usafiri hususani mabasi.

2. Fursa zinazohitaji mitaji mikubwa au ya kiasi. Nitataja baadhi na ambazo ni rahisi kuzitambua kama ifuatavyo:-

(i). Kununua mazao mashambani na kuleta mjini kwenye masoko
Hapa kuna mahindi, viazi aina zote, mchele mboga mboga kutoka mashambani kuleta mijini. Kikubwa kufanya tathmini vizuri.

(ii). Umachinga wa kuuza vitu mtaani kando ya barabara au kutembeza au kutengeneza banda lako sehemu inayoonekana kwa wateja

(iii). Kilimo, uvuvi na ufugaji

Kilimo kinahitaji uwe na shamba, mbegu, pembejeo za kilimo mbolea na dawa za kupulizia kuua vijidudu hatarishi kwa mazao nacho kilimo kitategemea na aina ya mazao unayolima.

Ufugaji
Mfano wa kuku lazima uwe na mtaji wa kununua kuku, pumba, uduvi na mifupa.

(iv). Udereva boda boda au bajaji
Huu nao utahitaji uwe na mtaji au upate ya mtu. Mfano bado boda hakosi kupata 25000 hadi 30000 kwa siku.

(v). Kuanzisha saloon zote za kunyoa nywele na kusuka nywele
Hapa kwa wanaume na kwa wanawake kuna kunyoa na kusuka hivyo sehemu uliyopo ikiwa na uhitaji hii ni fursa.

(vi). Huduma ya kutuma pesa kwa njia za simu.
Kuanzisha M pesa, airtel money, tigo pesa na halopesa.

(vii). Kuanzisha mgahawa, mama ntilie au ukaangaji wa chipsi na kuchoma mishkaki.

(viii). Kununua na kuuza vyuma chakavu. Hii pia ni fursa inayolipa vizuri ni jambo la kufanya uchunguzi na kuthubutu.

MCHANGO WA SERIKALI PAMOJA NA SEKTA BINAFSI KATIKA KUWASAIDIA WAHITIMU.

1. Kuwapa motisha, semina na muongozo wa namna ya kuanza ujasiriamali.

2. Kuwapatia mikopo yenye riba nafuu au isiyo na riba kabisa.(walemavu wapewe kipaumbele).
Serikali na sekta binafsi kupitia benki na taasisi zingine za kifedha watoe mikopo kwa wahitimu. Pia familia zenye uwezo ziwawezeshe vijana wao waliohitimu.

3. Mazingira wezeshi kwa watafutaji wanaoanza kutafuta mtaani. Hapa kuwaondolea kodi kandamizi. Kuboresha miundo mbinu zaidi mijini na vijijini itasaidia usafirishaji wa bidhaa.

4. Serikali itengeneze mahusiano mazuri na mataifa mengine. Itasaidi kutanua soko la nje kwenye ajira na bidhaa au mazao yatakayo zalishwa nchini.

5. Serikali na sekta binafsi zinapaswa kwa pamoja kuwaamini vijana na kuondoa kigezo cha uzoefu katika kuwapatia kazi/ajira.

6. Serikali na sekta binafsi ziwashirikishe vijana katika juhudi za kuwainua iwe mikopo au semina za kiujasiriamali.

7. Mfumo wa elimu uboreshwe hususani mitaala. Elimu itolewe kwa vitendo na ijikite katika kuwaandaa kujitegemea/kujiajiri.

8. Wazazi, jamii, serikali na mashirika binafsi kwa pamoja watambue na kudhamini karama au vipaji vya wanafunzi toka wakiwa wadogo na kuvisimamia kwa lengo la kujiajiri baadae.

9. Wahitimu wote wenye ulemavu wapatiwe kazi serikalini na mashirika binafsi moja kwa moja. Mfano ajira za mwaka 2021 ualimu na afya serikali haikuwaacha nyuma hili liendelee kila wakati.

10.Kuwe na uwazi katika masuala ya ajira. Iwe za serikali mpaka mashirika binafsi.

11. Ukabila, rushwa, umaeneo na udini viepukwe katika kuwapatia vijana ajira.

12. Waliofikia umri wa kustaafu wasiruhusiwe kuendelea kufanya kazi.

13. Uwepo mgawanyo wa kazi.
Ili mtu mmoja asifanye kazi zaidi ya kituo kimoja.

USHAURI WANGU KWA VIJANA WAHITIMU KATIKA UTAFUTAJI
Ushauri wangu kwa vijana wasaka tonge wahanga wa ajira na vijana woote watafutaji kwa ujumla napenda kutoa ushauri kama ifuatavyo:-

(i). Uvumilivu kwenye hizo fursa tunazoenda kuanzisha maana nako pia tutakutana na changamoto ila tusivunjike moyo na tusikate tamaa mapambano yaendelee.

(ii). Tuzijue hizo fursa na kutambua majira ya hizo fursa itasaidia kutambua muda gani muafaka wa kuanza tusikurupuke kuna kuanguka pia.

(iii). Kama unamtaji usianze na pesa yote ya mtaji maana hauna uhakika 100% kuwa itaenda sawa hivyo kujipanga kwa hilo ni muhimu.

(iv). Kupata ushauri kwa waliofanikiwa ni muhimu itakuongezea maarifa kwa yale usiyo yajua.

(v). Usimuamini kila mtu katika utafutaji wako wengine watakukwamisha. Mfano wanao kopa ni sumu kwako unaeanza utafutaji.

(vi). Tambua hitaji la jamii ikizungukayo. Kama jamii inataka mahindi wapelekee mahindi na sio mchele.

(vii). Ishi vizuri na watu na waheshimu watu kwa imani zao makabila yao na rangi zao. Kuwa na lugha nzuri.

(viii). Zingatia usafi kwenye ofisi yako kuwa na mpangilio mzuri pia toa huduma iliyo bora sio bora huduma.

(ix). Muhimu na la kukumbukwa kila unapopata kidogo kitunze kadri kinavyo kua kiwekeze kitaleta zaidi.

(X). Fanya shughuli halali, kuwa muaminifu, uadilifu ni muhimu na kufuata sheria za nchi yetu katika utafutaji.
 
Upvote 1.6K
Kazi ngumu ndio yenye hela, ukitaka kilimo chepesi ni mchicha lkn ni nani aliwahi kutajilika kwa kuuza mchicha.
Watu wanatafuta pakuanzia mchicha ukiulima vzr na ukawa na uhakika wa soko mbona unapiga hatua mkuu. Tembea ujionee mengi. Masoko kama ya miji mikubwa kama dar es salaam mchicha unauzika saana tu na unalimwa saana mabustanini
 
Kazi ngumu ndio yenye hela, ukitaka kilimo chepesi ni mchicha lkn ni nani aliwahi kutajilika kwa kuuza mchicha.
Upo sawa ndugu, maana yangu ilikuwa ni kwamba watu wasije wakadhani kupata kg moja ya vannila ni rahisi kama kupata kg moja ya mahindi au mpunga.
 
Mkuu tuelezee hapa kuwa je hiyo vanilla kuikusanya kg 1 inakuaje kuaje kwa ujumla tupe fununu zakueleweka kuhusu vanilla.
 
Upo sawa ndugu, maana yangu ilikuwa ni kwamba watu wasije wakadhani kupata kg moja ya vannila ni rahisi kama kupata kg moja ya mahindi au mpunga.
Kazi ngumu ndio yenye hela, ukitaka kilimo chepesi ni mchicha lkn ni nani aliwahi kutajilika kwa kuuza mchicha.
NIMEINGIA MTANDAONI NIMEWALETEA HII HAPA MAELEZO YA NAMNA YA KULIMA VANILA NI KAZI NZITO SIO KIDOGO. kwa kuanza utafutaji simshauri mtu aanze hii inataka una chanzo.kingine cha kipato

KILIMO BORA CHA VANNILA :

UTANGULIZI

Zao la vanilla ni moja ya zao la viungo ambalo asili yake ni Kusini Mashariki ya Mexico na sehemu nyingine za Amerika ya Kati. Vanilla hulimwa katika nchi mbalimbali duniani. Nchi zinazolima kwa wingi ni pamoja na Madagascar, Comoro, Tahiti, Uganda, India na nchi nyingine za Amerika ya Kati.

Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazolima vanilla katika Afrika. Zao hili lilianza kuingia nchini kutoka Uganda mnamo mwaka 1954 kupitia kwa mkulima mmoja wa kijiji cha Kiilima wilaya ya Bukoba Vijijini. Vanilla imeanza kulimwa kibiashara hasa katika mkoa wa Kagera mwaka wa 1992.

Katika mkoa wa Kagera, kilimo cha Vanilla kimehamasishwa zaidi na Chama cha Maendeleo Ya Wakulima kinachofahamika kama MAYAWA. Chama hiki kimekuwa kikihimiza uzalishaji na usindikaji wa Vanilla ambayo huuzwa kupitia kampuni zilizopo Uganda.

Mmea wa Vanilla huzaa maharage (mapodo) ambayo hukaushwa kwa njia maalum inayowezesha kupatikana kwa Kemikali inayoitwa Vanillini. Kemikali hiyo hutumika katika kuongeza ladha na harufu nzuri kwenye vyakula na vinywaji mbalimbali. Pia hutumika katika viwanda vinvyotengeneza Vipodozi na Dawa za matibabu ya binadamu.

Kwa matumizi ya kawaida, Vanilla huweza kutumika katika vinywaji kama Chai, Maziwa na kama kiungo kwenye mapishi ya Vyakula mbalimbali.

Maeneo mengine ya Tanzania yanayoweza kulima zao la vanilla ni pamoja na wilaya za Mbeya Vijijini, Tukuyu, Morogoro Vijijini, Mvomero, Muheza, Arumeru na Ukerewe.

UMBILE LA MMEA NA MAZINGIRA YANAYOFAA

Mmea wa Vanilla upo katika familia ya Okidi (Orchidaceae) ambayo ina generazipatazo 700. Kati ya hizo, genera moja itwaayo vanilla ndio yenye umuhimu wa kiuchumi. Genera ya Vanilla ina aina au jamii zipatazo 110, kati ya hizo ni mbili ambazo huzalishwa kibiashara. Aina hizo ni Bourbon ya nchini Mexico na Tahitian ya visiwa vya Tahiti.

Mmea wa Vanilla ni rando teke linalotambaa ambalo ni la kudumu. Mmea huu hukua na kutambaa katika mti mwingine hadi kufikia urefu wa mita 10 hadi 15 na zaidi kutegemea na mazingira.

MIZIZI

Mizizi ya mmea huu ni mirefu ina rangi nyeupe, myembamba yenye kipenyo cha milimita mbili. Mizizi hutokea kwenye fundo la shina lililo ndani ya udongo na hutambaa sambamba na tabaka la udongo wenye rutuba. Pia hutokea katika vifundo vya shina sambamba na majani ambayo hujishikiza katika miti ya kuegemea.

SHINA

Shina la vanilla lina rangi ya kijani, refu lenye vifundo na kipenyo cha sentimeta moja hadi mbili. Nafasi kati ya fundo na fundo ni sentimita tano (5) hadi 15.

MAJANI

Majani yana rangi ya kijani iliyokolea, yenye umbile la bapa, lenye ncha, nene na kubwa. Huota kwa kupishana katika shina, yana urefu wa sentimita nane hadi 25 na upana wa sentimita mbili hadi nane, na yana rangi ya kijani iliyokolea.

MAUA

Maua yana rangi mchanganyiko wa kijani na njano na kipenyo cha sentimita 10. Huota katika vifungu vyenye maua kati ya 18 hadi 30.

MATUNDA

Matunda yana umbile la podo la harage lenye rangi ya kijani likiwa changa. Hubadilika kuwa rangi ya njano, hatimaye kahawia kadri linavyokomaa. Podo lina urefu wa sentmeta 10 hadi 25, kipenyo cha sentimeta nane hadi 15 na lina mbegu ndogo sana ambazo huonekana linapokomaa.

MAZINGIRA YANAYOFAA KATIKA UZALISHAJI WA ZAO LA VANILLA

Mmea wa vanilla una asili ya msituni hivyo huhitaji kuoteshwa katika sehemu yenye kivuli na mvua ya kutosha. Ili zao hili liweze kukua vizuri linahitaji mazingira yafuatayo:

MVUA

Mmea wa Vanilla huhitaji kiasi cha mvua cha milimita 1250 hadi 2500 kwa mwaka. Pia zao hili huhitaji kipindi cha miezi mawili cha ukame ili kuweza kusisisimka na kutoa vitumba vya maua.

JOTO

Zao hili hustawi vizuri katika maeneo yenye nyuzi joto 20 hadi 30 za Sentigredi. Pia huweza kustahimili nyuzi joto 32 za Sentigredi. Lakini hukua vizuri zaidi katika kiwango cha nyuzi joto 27 za Sentigredi.

MWINUKO

Zao hili hustawi vizuri katika maeneo yenye mwinuko wa mita 0 hadi 600 kutoka usawa wa bahari. Pia hustawi katika maeneo yenye mwinuko unaofikia mita 1500 katika nchi za joto (tropiki).

UDONGO

Mmea wa vanilla una mizizi ambayo hutambaa katika sehemu ya juu ya udongo. Hivyo, huhitaji udongo mwepesi wa tifutifu, wenye rutuba ya kutosha na usiotuamisha maji.

MWANGA

Mmea wa vanilla huathirika kwa jua na husababisha kuungua kwa majani, hivyo huhitaji kivuli cha asilimia 50 hadi 75 ili uweze kukua vizuri. Kivuli kinaweza kupatikana kwa kupanda miti au kwa kutengenezwa kitaalamu.

UZALISHAJI WA ZAO LA VANILA

Vanilla huzalishwa kwa kupandikiza marando moja kwa moja shambani au kwa kukuzwa kwanza kwenye kitalu na baadaye kupandikizwa shambani. Kabla ya kupanda inatakiwa kuzingatia yafuatayo:

UCHAGUZI WA SHAMBA

Shamba la kupanda vanilla inafaa liwe mahali pasipo na upepo mkali ili kuepuka kuanguka kwa miti ya kuegemea na kukatika kwa mimea. Ni muhimu kupanda miti ya kuzuia upepo ikiwa mahali hapo pana upepo mkali. Shamba hilo pia liwe na udongo usiotuamisha maji, mwepesi na ambao unaruhusu mizizi kupenya kwa urahisi.

Aidha, shamba lisiwe na magugu mabaya (kwa mfano kwekwe/sangare) ambayo hulazimu kutumia jembe mara kwa mara wakati wa palizi. Kutumia jembe huweza kusababisha kukatika au kuharibu mizizi na kuhatarisha ukuaji wa mmea.

UTAYARISHAJI WA SHAMBA

Utayarishaji wa shamba huhusisha shughuli mbalimbali kama vile usafishaji wa shamba, utayarishaji wa mashimo na uwekaji wa mbolea.

KUSAFISHA SHAMBA

Shamba lisafishwe kwa kulima, kungíoa visiki, magugu mabaya na kutifua hadi kina kisichopungua sentimita 30.

KUTAYARISHA MASHIMO

Mashimo yatayarishwe miezi miwili hadi mitatu sambamba na usafishaji wa shamba. Yawe na kina cha sentimita 30 na upana wa sentimita 60 hadi 90. Nafasi kati ya mstari na mstari iwe mita mbili na nusu hadi mita tatu na kati ya shimo na shimo iwe mita moja na nusu hadi mbili. Udongo wa juu utengwe na ule wa chini.

UWEKAJI WA MBOLEA

Mbolea za asili kama mboji, vunde au samadi ichanganywe vema na udongo wa juu na kujazwa kwenye shimo kwa kipimo cha debe moja hadi mbili kwa kila shimo.

MIFUMO YA UPANDAJI

Zao la vanilla huweza kupandwa shambani kwa kutumia mifumo mikuu mitatu ifuatayo:

(i) VANILLA PEKEE

Mfumo huu unahusisha upandaji wa mmea wa vanilla na miti ya kuegemea tu ambayo hutoa kivuli kwa mimea.

(ii) VANILLA NA MIGOMBA

Mfumo huu unawezesha kuotesha vanilla katika shamba la migomba, ambapo rando hupandwa pamoja na mti wa kuegemea ndani ya shamba la migomba. Na hivyo kukuwezesha kufanya kilimo cha migomba na vanilla katika shamba moja kwa wakati mmoja

(iii) VANILLA NA MITI YA KIVULI

Katika mfumo huu vanilla huoteshwa katika shamba la miti ya kivuli, ambapo mmea hupandwa na miti ya kuegemea katikati ya miti ya kivuli.

Kumbuka: Mfumo wa pili na wa tatu unapendekezwa zaidi kutokana na matokeo yake mazuri.

UPANDAJI WA MITI YA KUEGEMEA (MIEGA)

Miti ya kuegemea hupandwa miezi miwili hadi mitatu kabla ya kupanda rando la vanilla ili iweze kuchipua, kutoa kivuli na kuwa na uwezo wa kuhimili mimea.

(i) SIFA ZA MIEGA

Miti inayofaa kutumika kwa kuegemea iwe na sifa zifuatazo:

Uwezo wa kukua haraka bila kuathiri mmea wa vanilla.Uwezo wa kutoa kivuli kinachofaa.Uwezo wa kuchipua haraka inapopunguzwa.Uwezo wa kuchipua matawi kwa chini ili kupandishia marando kwa urahisi.Uwezekano wa kuoteshwa kwa urahisi.

Miti yenye sifa hizo ni pamoja na mibono (Jatropha carcus) na Gilirisidia. Miti mingine inayoweza kutumika kwa kivuli na kuegemea ni pamoja na Erythrina spp na Bauhania spp.

(ii) KUPANDA MIEGA YA MIBONO

Miti inayotumika zaidi katika mashamba ya vanilla ni jamii ya Jatropha. Miti hii huoteshwa kwa kutumia mbegu au kipande cha tawi kwa umbali wa sentimita 30 kutoka katika shimo la kupandia vanilla. Tawi la mbono lenye urefu wa sentimita 120 hadi 150 hupandwa katika kina cha sentimita10 hadi 15.

UPANDAJI WA VANILLA

Mmea wa vanilla hupandwa mwanzoni mwa msimu wa mvua ili kuhakikisha upatikanaji wa unyevu ardhini. Hupandwa kwa kutumia rando lenye urefu wa kati ya sentimita 100 hadi 150 (futi tatu na nusu hadi tano) kutoka kwenye mmea unaokuwa vizuri, usio na magonjwa na wenye pingili ndefu. Rando lenye sifa hizo hukua haraka na kutoa maua mapema (miaka 2). Rando fupi halikui haraka na huchukua muda mrefu kutoa maua (miaka 2 hadi 3).

KUTAYARISHA MARANDO

Kata rando kwa kutumia kisu kikali kwa kufuata vipimo (sentimita 100 hadi 150).Ondoa majani matatu hadi matano katika sehemu ya chini ya rando itayofukiwa kwenye udongo.Ning’iniza rando lililokatwa kwenye kivuli kwa muda wa siku saba hadi 10 kabla ya kupanda ili kupunguza utomvu na kulipa nguvu ya kuchipua na kuhimili hali ya shambani.

JINSI YA KUPANDA

Upandaji wa vanilla hufanywa kwa kutumia hatua zifuatazo:

Andaa nyasi kavu (matandazo) ambazo zitatumika mara baada ya kupanda.Tengeneza kifereji chenye kina cha sentimita 10 hadi 12 katikati ya shimo lenye mbolea lililokwisha tengenezwa.Laza sehemu ya rando iliyotolewa majani katika kifereji hicho, acha sehemu yenye majani juu ya ardhi.Fukia rando kwenye kifereji kwa udongo na gandamiza taratibu ili lishikamane na udongo.Funga sehemu ya juu ya rando kwa kutumia kamba katika umbile la nane kwenye mti wa kuegemea.Weka matandazo kuzunguka kila shina lililopandwa.

KUMBUKA:

Utaratibu huu wa kupanda hutumika katika aina zote za mifumo ya kuzalisha vanilla, na hutofautiana kwa nafasi za upandaji kati ya mfumo mmoja na mwingine.Shamba la vanilla pekee katika miaka ya mwanzoni, huweza kuchanganywa katikati ya mistari na mazao mengine ya muda mfupi kama mazao ya jamii ya mikunde.

UTUNZAJI WA SHAMBA

Vanilla huhitaji kutunzwa vizuri ili iweze kukua vizuri na kutoa mavuno yenye ubora wa hali ya juu. Huduma muhimu katika uzalishaji wa vanilla ni kama ifuatavyo:

KUTENGENEZA KIVULI

Mmea wa vanilla huhitaji kivuli ili uweze kukua vizuri. Hivyo ni muhimu kupanda miti ya kivuli kabla ya kustawisha vanilla. Katika ukuaji wake kuanzia inapopandwa hadi inapokaribia kutoa maua huhitaji kivuli cha kutosha kinachoweza kuzuia jua kali na kuruhusu mwanga (asilimia 60 hadi 70).

Kipindi cha kusisimua kivuli kipunguzwe zaidi na kufikia asilimia 55 hadi 50. Kivuli kitengenezwe kwa kupunguza matawi ya miti ya miega na ya kivuli ili kupata kivuli kinachofaa.

Kumbuka: Kivuli kizito huathiri ukuaji wa mmea.

KUWEKA MATANDAZO

Utandazaji wa nyasi ni muhimu katika shamba la vanila kutokana na tabia ya ukuaji wa mizizi ambayo huota katika kina cha sentimita 5 hadi 10, hivyo huhitaji kulindwa isiharibiwe. Matandazo yawekwe kuzunguka mashina ya mimea ili kuhifadhi unyevu, kuzuia uotaji wa magugu, na kulinda mizizi isiharibiwe wakati wa palizi.

Kumbuka: Matandazo yawe makavu na yasiwe na mbegu za magugu.

PALIZI

Palizi hufanyika wakati wowote magugu yanapoota shambani. Inashauriwa kufanya palizi kabla ya mvua kunyesha ili mmea uweze kutumia maji ya mvua ipasavyo. Palizi ifanyike wakati wowote magugu yanapoota shambani, kwa kungíoa magugu kutumia mikono ili kuepuka kujeruhi mizizi jembe linapotumika.

KUNING’INIZA MARANDO

Mmea wa vanilla uliokua vizuri huota matawi (marando) mengi na marefu. Marando hayo huelekezwa kwenye matawi ya miti ya kuegemea na kuningíinizwa. Rando linapofikia urefu wa sentimita 150 hadi 180 liningíinizwe katika matawi ya miega ili liendelee kukua kuelekea chini. Endapo kuna upepo mkali, marando yafungwe kwenye miega kwa muda ili yasivunjike.

KULISHA MARANDO

Kulisha marando ni kitendo cha kufukia ardhini sehemu ya kipande cha rando ili kiweze kutoa mizizi na kuongeza nguvu ya kuchukua chakula kutoka kwenye udongo. Kazi hii hufanywa baada ya rando lililoningíinizwa kurefuka sana kiasi cha kutambaa ardhini, katika hatua hii mmea huweza kuwa na umri wa miezi sita hadi tisa kutegemea na utunzaji.

Jinsi ya Kulisha

Ondoa majani matatu hadi manne kwenye rando lililoingíinizwa na kurefuka sana.Fukia kwenye udongo, karibu na shina sehemu iliyoondolewa majani.Weka matandazo katika sehemu iliyofukiwa ili kuhifadhi unyevu.Funga sehemu ya juu ya rando katika mti wa kuegemea ili liendelee kukua.Marando mawili hadi mitatu yalishwe kwa wakati mmoja na mengine yaachwe kwa ajili ya kutoa maua na kupata marando ya kupanda.

Kumbuka: Kulisha kufanyike wakati wa mvua ili marando yaweze kutoa mizizi kwa urahisi. Kazi hii irudiwe kila wakati ili rando mama litakapokatika machipukizi yake yaendelea kukua.

KUSISIMUA

Kusisimua ni kitendo cha kuufanya mmea kuwa katika hali ya kuweza kutoa maua. Kitendo hiki kifanywe wakati mmea ukiwa umefikia umri wa mwaka 1 na nusu au zaidi, na hufanywa wakati wa kiangazi ili kuepuka kupata matawi mengi badala ya vitumba vya maua. Mmea usiosisimuliwa hautoi maua au hutoa maua machache na kusisimua mapema kunaweza kuuchosha mmea.

JINSI YA KUSISIMUA

Chagua matawi matatu hadi matano yanayoningíinia. Kusisimua matawi mengi kunaweza kuudhoofisha mmea au kuzaa maharage madogo.Kata ncha ya rando ili kuwezesha vitumba vya maua kukua na kuwa tayari kufunguka au kutoa maua.

Ukataji wa ncha huweza kufanyika kama ifuatavyo:

Kukata ncha ndogo (mdomo wa rando) kwa mkono. Hii hufanyika kwa rando fupi linaloningínia.Kukata rando kwa kisu kikali, kwa rando linaloningínia ambalo halijafikia urefu wa kupanda.Kukata rando kwa kisu kikali kwa rando refu linaloningíinia (lenye urefu wa kuweza kupandwa, sentimita100-150).

UCHAVUSHAJI

Ni kitendo cha kuunganisha chavua kutoka katika sehemu dume ya ua na kuweka katika sehemu jike ya ua, hufanyika baada ya maua kuchanua.

UCHANUAJI WA MAUA

Mmea wa Vanilla hutoa maua miezi miwili hadi mitatu baada ya kusisimuliwa. Maua huchanua kwa kipindi cha masaa matatu hadi manne kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa saba mchana kwa muda wa miezi miwili hadi mitatu kutegemea unyevu uliopo kwenye udongo na kiwango cha Jua.

Ua huchanua kwa muda huo na hudondoka baada ya siku 1 ikiwa halikupata chavua. Hivyo ni muhimu uchavushaji ufanyike kwa haraka na kwa uangalifu mkubwa.

JINSI YA KUCHAVUSHA

Mmea wa vanilla, ili uweze kutoa matunda inabidi uchavushwe. Ua la vanilla kwa kawaida huchavushwa na nyuki jamii ya melapona ambao hawapo hapa nchini. Nyuki hao hupatikana Mexico na katika nchi nyingine za Amerika ya Kati. Hivyo uchavushaji hufanywa kwa mikono kwani umbile la ua haliruhusu nyuki wa aina nyingine kufanya uchavushaji.

UCHAVUSHAJI HUFANYWA KWA KUFUATA HATUA ZIFUATAZO:

Gawa petali ya ua la vanilla katika sehemu mbili kwa kutumia pini, sindano, au mwiba. Hakikisha vifaa hivyo ni safi.Kunjua sehemu jike ya ua (stigima) kwa kuelekea juu ili kuwezesha kulala sambamba kwenye sehemu dume ya ua (stameni).Unganisha stameni na stigima na kubana taratibu kwa dole gumba kwa nusu dakika ili kuruhusu chavua kuingia kwenye stigima.

Ua lililochavushwa vizuri, hubaki likiningíinia kwenye kikonyo chake. Ikiwa uchavushaji haukufanikiwa, ua hudondoka baada ya siku moja au mbili. Kiasi cha maua au mapodo nane hadi 12 yaachwe katika kila kitumba. Aidha vitumba vinne hadi nane viruhusiwe kukua katika kila rando na visizidi 20 kwa mmea.

Ndugu yangu mkulima hivi ndivyo vanilla inavyolimwa, ni shughuri nzito sana lakini inalipa sana, kama ilivyo kawaida: mvumilivu hula mbivu. Sasa badilishana nasi uzoefu wako wa kilimo hiki kwa ku-coment hapa chini huku ukisubiri muendelezo wa kilimo cha vanilla.

Chanzo cha maelezo haya ni Swahili Blog
 
KILIMO-BORA-CHA-VANNILA-400x194.jpg
na picha ya Vanilla hii hapa
Chanzo cha picha Swahili blog
 
Mimi binafsi nimetembelea hadi ofisi za hawa MAYAWA pale Bukoba mjini kushuhudia jinsi wanavyofanya processing ya vanilla. Aisee ni tedious process! Kilimo chake sifahamu but bila shaka sio kifahisi
 
Kwa wanao anza kutafuta mitaji hiki kilimo wala hawawezi kwa kweli wakiache kwanza wasake mitaji wa kijikwamua ndipo wajihusishe na hiki kilimo.

Mkuu kwa hapo unaposema wananunua kilo bei gani mkuu?.?
 
Mkuu ni dhahiri kuwa wahitimu wengi wapo selective sana ktk kazi za kufanya...
Wengi wanawish wapate kazi znazoendana na taaluma zao, jambo ambalo si sawa coz dunia kwa sasa inazunguka kwa kasi kubwa sana, so kuipata kazi ya taaluma husika n mtihani.

Zaidi ni kujiongeza ktk kufumikia fursa zinazotuzunguka.....
Uvuvi ni moja ya sekta isiyohitaj mtaji mkuuuuubwa kuanza kufanya kaz bt wengi huichukulia kuwa n ya local people.
Ila tuliopo humu tunajua tunachokipata.

Nijitolee mfano mimi....
Niko na biashara tatu ( duka la nguo za kiume, duka ka viatu vya kiume na saluni 2 za kike) na zote zipo active, bt nimeona fursa ktk uvuvi, cjakubali hii fursa inipite..... Nafanya biashara ya nyavu na pia navua samaki.
Point yangu kubwa ni kutokubali fursa ikupite..... Mambo ya kusubir kupata kazi ya taaluma uloioata kwa theory sio mchongo kwa dunia ya karne hii.
View attachment 1902245
FB_IMG_1629467984413.jpg
View attachment 1902246
 
View attachment 1902245View attachment 1902247View attachment 1902246
Shukran mkuu kwa uzoefu wako na ushauri wako una hamasisha kweli. Tuzidi kupeana uekewa wa fursa zinazotuzunguka maana kila sehemu ina fursa zake japo mara nyingi zinafanana kwa kuangalia jeografia ya sehemu husika na maendeleo pia ya hiyo sehemu
 
Bado Tanzania inatoa idadi ndogo sana ya wahitimu wa vyuo vikuu ukilinganisha na nchi Jirani kama Kenya na Uganda.
Hivyo Serikali yetu bado inaweza kukabiliana na tatizo la ajira kwa wahitimu wa vyuo.
Endapo Serikali yetu itaweka na kusimamia mikakati madhubuti ktk maeneo uliyo yataja hakika tatizo la ajira litadhitiwa kwa kiwango kikubwa sana.
Mfano;
Serikali iliweka mkakati wa kujenga viwanda vikubwa na vidogo ktk kila Mkoa na Wilaya nchini., endapo mkakati huu utasimamiwa kikamilifu naamini tatizo la ukosefu wa ajira litadhibitiwa kwa 90%.

Serikali ianzishe utaratibu wa kutoa ajira za mikataba ya muda mfupi hii itasaidia kwa wahitimu angalu kupata kianzio, anaweza kupata mtaji kisha akajiajiri mwenyewe.
 
Bado Tanzania inatoa idadi ndogo sana ya wahitimu wa vyuo vikuu ukilinganisha na nchi Jirani kama Kenya na Uganda.
Hivyo Serikali yetu bado inaweza kukabiliana na tatizo la ajira kwa wahitimu wa vyuo.
Endapo Serikali yetu itaweka na kusimamia mikakati madhubuti ktk maeneo uliyo yataja hakika tatizo la ajira litadhitiwa kwa kiwango kikubwa sana.
Mfano;
Serikali iliweka mkakati wa kujenga viwanda vikubwa na vidogo ktk kila Mkoa na Wilaya nchini., endapo mkakati huu utasimamiwa kikamilifu naamini tatizo la ukosefu wa ajira litadhibitiwa kwa 90%.

Serikali ianzishe utaratibu wa kutoa ajira za mikataba, hii itasaidia kwa wahitimu angalu kupata kianzio, anaweza kupata mtaji kisha akajiajiri mwenyewe.
[emoji1319][emoji1319] shukran mkuu kwa mawazo uzoefu na uelewa wako uliojaa ukweli asilimia kubwa umeongezea jambo zuri na linapopaswa pia kutekelezwa zaidi. [emoji1317][emoji1303]
 
Back
Top Bottom