SoC01 Wahitimu wa Vyuo na Maisha ya utafutaji Mtaani

SoC01 Wahitimu wa Vyuo na Maisha ya utafutaji Mtaani

Stories of Change - 2021 Competition

Theb

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2019
Posts
3,927
Reaction score
7,276
Habari zenu wana Jamii Forums, hususani jukwaa hili la "Stories of Change". Ni tumaini langu wote ni wazima.

Andiko hili litaangazia maisha ya vijana wahitimu wa vyuo waliotegemea kuajiriwa na hali imekua tofauti na matarajio yao. Mwanzo, nitaelezea maisha ya mtaani, changamoto zinazo wakabili na vipi watatue hizo changamoto, Pili, nitaelezea fursa zisizohitaji mitaji na zenye kuhitaji mitaji. Tatu, nitaelezea mchango wa serikali na sekta binafsi katika kuwasaidia vijana kupata ajira na kujiajiri. Mwisho, nitamalizia kwa kutoa ushauri wangu katika kuwawezesha vijana wahitimu kujikwamua.

Maisha ya mtaani katika jamii zetu karibia kote yana mfanano kwa asilimia kubwa. Kuanzia ngazi ya familia za wahitimu walio wengi zinafanana kiuchumi, kitamaduni na hata kimalengo. Familia nyingi katika jamii zetu Tanzania tunasoma ili tuajiriwe na sio kujiajiri kwa waliowengi, hali iliyopo kwa sasa imeenda kinyume na malengo na matarijio ya vijana waliokuwa wanasoma na wanaoendelea kusoma mashuleni mpaka vyuoni.

CHANGAMOTO ZINAZO WAKABILI VIJANA WAHITIMU KATIKA UTAFUTAJI.

1. Kushindwa kujiamini na kushindwa kuikubali hali halisi iliyopo. Wengi wameshindwa kujiamini na kufikiria nje ya kitu walichosomea na kuanza kitu kipya ina wawia ngumu.

2. Mazingira yanayo wazunguka wahitimu, jamii ina wapa wakati mgumu kwa kuwahukumu kuwa wamesoma bure, elimu yao haina faida. Hili sio sawa.

3. Ukosefu wa muunganiko baina ya wahitimu na waliotangulia kwenye utafutaji, hapa unakuta wahitimu hawana muunganiko na waliotangulia kwenye utafutaji mitaani.

4. Ukosefu wa mitaji, hususani kwenye biashara au fursa zinazohitaji mitaji.

5. Kukosa uelewa katika utafutaji wenyewe. Kutozijua fursa au kutozitambua biashara na majira yake. Maana kila biashara ina majira yake.

6. Kuchagua kazi. Baadhi ya wahitimu hii changamoto kubwa kwao. Hawako tayari kubeba hata mizigo wanaona aibu au wanaona haiba yao hawastahili kubeba mizigo.

7. Mfumo na mitaala ya elimu nchini haikidhi dhumuni la kujiajiri kwa sababu imejikita katika nadharia zaidi na sio hali halisi katika kujiajiri.

JINSI YA KUPAMBANA NA HIZO CHANGAMOTO:-

1. Wazazi wasaidie watoto wao kuchagua fani zitakazo wawezesha kujiajiri pindi watakapo hitimu vyuoni.

2. Kujikubali, kujitambua na kujichanganya na watafutaji wengine mitaani bila kuwaza au kujutia muda uliopoteza shuleni na vyuoni.

3. Kukubali hali halisi hususani kuwa tayari kwa kazi yoyote bila kuchagua kazi. Mfano baadhi ya wahitimu ni ngumu kufanya kazi kama kuuza mkaa au kununua chupa za plastiki zilizotumika kwa kuhofia taaluma yake au watu watamuonaje.

4. Kuzitambua fursa na kuwa tayari kupambana nazo maana utafutaji mtaani ni ushindani.

5. Kufanya uchunguzi wa biashara unayotaka kwenda kuanzisha, hapa itahitaji kutafiti kwa kile unachotaka kufanya mtaani.

6. Kupunguza matumizi yale yasiyo muhimu. Kuwa na matumizi sahihi ya fedha. Mfano waache unywaji wa pombe, kubet, uvutaji wa sigara au ulevi wowote na anasa zingine zinazo hitaji pesa.

7. Kufanya uchaguzi sahihi wa kile unachoweza kukifanya mtaani na sio kufuata mkumbo. Fanya unachokipenda na unachokiweza

8. Usisahau kutunza kile unachokipata hata kama kidogo. (Bandu bandu humaliza gogo)

FURSA ZINAZOWEZA KUSAIDIA WAHITIMU KATIKA UTAFUTAJI MTAANI

1. Fursa zisizo hitaji mitaji na zisizo hitaji mitaji mikubwa sana. (Hizi kwa ajili ya kuanza kujipatia mitaji kidogo kidogo)

(i) Vibarua viwandani
Kwa wale wahitimu waliopo mijini kuna viwanda, vipo vibarua vya kutwa na wale wanaolipwa kwa wiki viwandani. Kuna kubeba mizigo viwandani kupakia na kupakua mizigo inayoingia na inayotoka na kazi zingine kulingana na kiwanda husika.

(ii) Fursa kwenye standi za mabasi ya abiria
Pia kwenye standi za mabasi kuna baadhi ya fursa zisizohitaji mitaji au zinazohitaji mitaji midogo. Mfano kubeba mizigo ya abiria kuwa wakala wa kukata tiketi na kuunza bidhaa ndogo ndogo kama karanga maji, juisi na matunda.

(iii) Kununua plastiki na kwenda kuziuza
Hapa kuna hii fursa ya kununua plastiki na kwenda kuuza mfano kilo moja unanunua kuanzia 300 hadi 400 na kuuza iliyosagwa ni kuanzia 800 hadi 1200 isiyo sagwa ni 800 bei ya kuuza. Hii ni fursa japo inadharauliwa.

(iv) Kuwa dalali wa mazao shambani au magari ya kusafirisha mizigo au dalali wa nyumba na viwanja
Haihitaji mtaji kwenye kuanza uaminifu wako na kujua chimbo za unachofanya ndio mtaji wako.

(v) Kuanzisha twisheni (tuition) mtaani kwenu
Hii pia saa zingine haihitaji mtaji itahitaji tu utayari wako na uwepo wa wanafunzi wanaosoma na kuitangaza. Japo maeneo mengine hii haina nafasi maana muitiko unakua mdogo hasa vijijini.

(vi) Kubeba mizigo kwenye masoko kupakua na kupakia mazao na bidhaa mbalimbali
Tunaweza kuidharau lakini ni fursa ukibeba mizigo 25 yenye kulipwa 1000 kila mzigo kwa siku una shilingi 25000. Haitaki mtu mwenye aibu na usharobaro.

(v). Kipaji kiwe cha uandishi, uimbaji, ususi, uchoraji, na michezo
Kipaji pia ni fursa kubwa tena isiyo hitaji mtaji ila inahitaji utayari wako kujituma na ubunifu zaidi na uvumilivu uliomithilika.

(vi). Kuwa saidia fundi ujenzi, fundi wa kuchomelea dirisha na mageti, fundi randa nk,

Kusaidia fundi atakulipa kidogo itategemea na kazi iliyopo hapo unajifunza ufundi, kujiandaa kuwa fundi ili ujitegemee. Mfano saidia fundi ujenzi hulipwa sio chini ya 10,000/= kwa siku.

(vii). Kuuza mahindi ya kuchoma na ya kuchemsha.
Hii hususani sehemu zenye mikusanyiko, stand za mabasi, barabarani na kwenye vyombo vya usafiri hususani mabasi.

2. Fursa zinazohitaji mitaji mikubwa au ya kiasi. Nitataja baadhi na ambazo ni rahisi kuzitambua kama ifuatavyo:-

(i). Kununua mazao mashambani na kuleta mjini kwenye masoko
Hapa kuna mahindi, viazi aina zote, mchele mboga mboga kutoka mashambani kuleta mijini. Kikubwa kufanya tathmini vizuri.

(ii). Umachinga wa kuuza vitu mtaani kando ya barabara au kutembeza au kutengeneza banda lako sehemu inayoonekana kwa wateja

(iii). Kilimo, uvuvi na ufugaji

Kilimo kinahitaji uwe na shamba, mbegu, pembejeo za kilimo mbolea na dawa za kupulizia kuua vijidudu hatarishi kwa mazao nacho kilimo kitategemea na aina ya mazao unayolima.

Ufugaji
Mfano wa kuku lazima uwe na mtaji wa kununua kuku, pumba, uduvi na mifupa.

(iv). Udereva boda boda au bajaji
Huu nao utahitaji uwe na mtaji au upate ya mtu. Mfano bado boda hakosi kupata 25000 hadi 30000 kwa siku.

(v). Kuanzisha saloon zote za kunyoa nywele na kusuka nywele
Hapa kwa wanaume na kwa wanawake kuna kunyoa na kusuka hivyo sehemu uliyopo ikiwa na uhitaji hii ni fursa.

(vi). Huduma ya kutuma pesa kwa njia za simu.
Kuanzisha M pesa, airtel money, tigo pesa na halopesa.

(vii). Kuanzisha mgahawa, mama ntilie au ukaangaji wa chipsi na kuchoma mishkaki.

(viii). Kununua na kuuza vyuma chakavu. Hii pia ni fursa inayolipa vizuri ni jambo la kufanya uchunguzi na kuthubutu.

MCHANGO WA SERIKALI PAMOJA NA SEKTA BINAFSI KATIKA KUWASAIDIA WAHITIMU.

1. Kuwapa motisha, semina na muongozo wa namna ya kuanza ujasiriamali.

2. Kuwapatia mikopo yenye riba nafuu au isiyo na riba kabisa.(walemavu wapewe kipaumbele).
Serikali na sekta binafsi kupitia benki na taasisi zingine za kifedha watoe mikopo kwa wahitimu. Pia familia zenye uwezo ziwawezeshe vijana wao waliohitimu.

3. Mazingira wezeshi kwa watafutaji wanaoanza kutafuta mtaani. Hapa kuwaondolea kodi kandamizi. Kuboresha miundo mbinu zaidi mijini na vijijini itasaidia usafirishaji wa bidhaa.

4. Serikali itengeneze mahusiano mazuri na mataifa mengine. Itasaidi kutanua soko la nje kwenye ajira na bidhaa au mazao yatakayo zalishwa nchini.

5. Serikali na sekta binafsi zinapaswa kwa pamoja kuwaamini vijana na kuondoa kigezo cha uzoefu katika kuwapatia kazi/ajira.

6. Serikali na sekta binafsi ziwashirikishe vijana katika juhudi za kuwainua iwe mikopo au semina za kiujasiriamali.

7. Mfumo wa elimu uboreshwe hususani mitaala. Elimu itolewe kwa vitendo na ijikite katika kuwaandaa kujitegemea/kujiajiri.

8. Wazazi, jamii, serikali na mashirika binafsi kwa pamoja watambue na kudhamini karama au vipaji vya wanafunzi toka wakiwa wadogo na kuvisimamia kwa lengo la kujiajiri baadae.

9. Wahitimu wote wenye ulemavu wapatiwe kazi serikalini na mashirika binafsi moja kwa moja. Mfano ajira za mwaka 2021 ualimu na afya serikali haikuwaacha nyuma hili liendelee kila wakati.

10.Kuwe na uwazi katika masuala ya ajira. Iwe za serikali mpaka mashirika binafsi.

11. Ukabila, rushwa, umaeneo na udini viepukwe katika kuwapatia vijana ajira.

12. Waliofikia umri wa kustaafu wasiruhusiwe kuendelea kufanya kazi.

13. Uwepo mgawanyo wa kazi.
Ili mtu mmoja asifanye kazi zaidi ya kituo kimoja.

USHAURI WANGU KWA VIJANA WAHITIMU KATIKA UTAFUTAJI
Ushauri wangu kwa vijana wasaka tonge wahanga wa ajira na vijana woote watafutaji kwa ujumla napenda kutoa ushauri kama ifuatavyo:-

(i). Uvumilivu kwenye hizo fursa tunazoenda kuanzisha maana nako pia tutakutana na changamoto ila tusivunjike moyo na tusikate tamaa mapambano yaendelee.

(ii). Tuzijue hizo fursa na kutambua majira ya hizo fursa itasaidia kutambua muda gani muafaka wa kuanza tusikurupuke kuna kuanguka pia.

(iii). Kama unamtaji usianze na pesa yote ya mtaji maana hauna uhakika 100% kuwa itaenda sawa hivyo kujipanga kwa hilo ni muhimu.

(iv). Kupata ushauri kwa waliofanikiwa ni muhimu itakuongezea maarifa kwa yale usiyo yajua.

(v). Usimuamini kila mtu katika utafutaji wako wengine watakukwamisha. Mfano wanao kopa ni sumu kwako unaeanza utafutaji.

(vi). Tambua hitaji la jamii ikizungukayo. Kama jamii inataka mahindi wapelekee mahindi na sio mchele.

(vii). Ishi vizuri na watu na waheshimu watu kwa imani zao makabila yao na rangi zao. Kuwa na lugha nzuri.

(viii). Zingatia usafi kwenye ofisi yako kuwa na mpangilio mzuri pia toa huduma iliyo bora sio bora huduma.

(ix). Muhimu na la kukumbukwa kila unapopata kidogo kitunze kadri kinavyo kua kiwekeze kitaleta zaidi.

(X). Fanya shughuli halali, kuwa muaminifu, uadilifu ni muhimu na kufuata sheria za nchi yetu katika utafutaji.
 
Upvote 1.6K
Kilo 1 ya Vanila ni tsh 1.2mln mavuno ni baada ya miezi 6 piga hesabu halafu linganisha na kuokota chupa kaa chizi.
Hiyo pia ni fursa hatuwezi woote tukaangukia kwenye fursa moja na nchi yoote haina hali ya hewa sawa kuna maeneo hilo zao halikui. Angalia andiko vizuri na kama umelisoma lote kilimo ni moja wapo ya fursa niliyoiorodhesha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kilo 1 ya Vanila ni tsh 1.2mln mavuno ni baada ya miezi 6 piga hesabu halafu linganisha na kuokota chupa kaa chizi.
Na ni vema kama ungedadavua hapa ili kila mtu atakaye pita atambue kuwa hiyo vanila inakulia mazingira gani, mtaji, hatua za kuandaa shamba na kuitunza mpaka inakua tayari. Mkuu tunaomba uelezee jinsi ya kulima vanila

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Elimu Yetu tuliyorithi toka kwa wakoloni ndio tatizo , kipindi hicho watu walisoma ili wakasaidie kazi za ofisini kwa sababu wanataaluma walikua wachache sana, sasa tatizo ni kwamba watu tumeongezeka ajira hakuna inasikitisha kijana wa kitanzania anamaliza chuo akiwa na 27 yrs na hajui akirudi mtaani atafanya nini!
Ni kweli kabsa. Ndio maana andiko langu nimejaribu kuonesha baadhhi ya fursa zilizopo mtani. Ambazo mtu yoyote anaweza kujichanganya na atakayoona ana iweza na inalipa kulingana na uhitaji wa sehemu alipo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Elimu yetu inamfanya kijana awe muoga na asijiamini leo hii kiukweli tunahitaji kuwekeza kwenye ujuzi zaidi kuliko kwenye hizo theory wanazofundishwa huko mashuleni,
Talent based education tuitilie mkazo na zaidi elimu iendane na mazingira hali ni mbaya na inasikitisha, kijana alieishia darasa la saba akaenda gereji au aliishia formfour akaenda gereji na akajifunza umeme wa magari tu kamwe wewe na degree yako unakuja kurudi tayari keshajenga na anamiradi kadhaa inaingiza kipato cha uhakika na hakupoteza muda wake vyuoni na asilimia kubwa mambo unayosoma vyuoni kiukweli ni machache sana utayatumia kwenye maisha halisi
Umenena vyema mkuu. Ndio maana ya andiko hili. Na ni moja ya mapendekezo kuwa serikali iufanyie mfumo wa elimu na mitaala yake maboresho ili iweze kuwaandaa wahitimu vizuri katika kiweza kujikwamua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wahitimunwakianza kubeba mizigo stend na kupiga debe, amini shule watoto wataacha kusoma ni bora wakakeshe gym tu sasa.

Hivi huwa mnaangalia impact ya haya mawazo yenu kwa kizazi kijacho kweli?, Napinga daima graduate kufanya hizo kazi seriously graduate akaanze kuwa kuli stendi?, Acha utani Mkuu hizo sio kazi na ndio ukweli.

Labda kama hatuji kwanini tuna wasomi wa elimu za juu nchini, kifupi hawa ndio usukani wa nchi sasa fikiria usukani ukaanze kubeba mizigo stend tutafika wapi miaka 30 ijayo.

Bora kulima, kufuga, biashara zenye tija, vipaji na mambo yenye tija sio kuwa kuli Mkuu.
 
Hiyo kubeba mzgo wewe unaona haiwezekani ila mtafutaji anaetafuta kamtaji hapaswi kuchagua kazi. Hicho kilimo au fursa yoyote inahitaji mtaji sasa asipo fanya kazi hata kama ni hizi za kubeba mizigo au kumfanyia mtu yoyote kazi kama hakuna wakumapatia mtaji atafanyaje ili apate mtaji wa kuanzia..? Kilimo kina taka mtaji maana kama hauna shamba utakodi shamba na uandae shamba na utafute mbegu na mbolea bado mazao yanavyokua kuna palizi kuna kunyunyizia dawa na mbolea za kukuzia. Hivyo hapo nimeoinisha vitu vinavyotaka mtaji na visivyo hitaji mitaji sijui unaweza kurudia kuusoma tena huu uzi.

Na toa wazo au mbadala unaoona wewe utasaidia kupata kujikwamua. Maana shida ni pakuanzia ndipo tunapojaribu kupaelezea. Kuna mhitimu kwao hawana shamba na hana wa kumpa mtaji afanye nini. Afu kazi ya kubeba mzigo usiidharau nenda masokoni mijini afu jichanganye na waulize watu walianzia wapi kupata mitaji. Utakuja kuelewa nacho ongelea kama utajaribu kufikiria vizuri. Mfano mbebaji wa mizigo sokoni anayebeba viloba 30 kwa siku kuwapelekea wateja analipwa tuseme kila kiloba 1000 itategemea na umbali ina weza kuzidi au kupungua jumlisha mara 30 inaleta bei gani tufanye kakodi toroli toa 5000 ya toroli na kula 5000 toka ahsubuhi mpaka usiku anabakiwa na bei gani. Kwa mwezi.afanya hivyo mara hata siku 25 au 22 tu ana shilingi ngapi..?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na ni vema kama ungedadavua hapa ili kila mtu atakaye pita atambue kuwa hiyo vanila inakulia mazingira gani, mtaji, hatua za kuandaa shamba na kuitunza mpaka inakua tayari. Mkuu tunaomba uelezee jinsi ya kulima vanila

Sent using Jamii Forums mobile app
Headline inatosha mkuu ukitaka utafuniwe kila kitu hiyo vanila itakushinda
 
Ingefaa ukatoa maelezo ya hilo zao kwa uzoefu wako.

Sent using Jamii Forums mobile app

Vanilla ni zao ambalo sokoni lipo juu sana, maana ni zaomuhimu kwa bidhaa za viwandani ikiwamo dawa ya meno, vanilla kwa Tanzania hulimwa zaidi mikoa ya kagera wilaya za muleba na kuerwa lakini pia njombe wameanza kulima na soko lake zuri liko Comoro kama sijasahau na waganda Nununua Tanzania na kupeleka ufaransa
 
Vizuri na inapendeza kwa kutoa ushirikiano ili kila atakaepitia hapa aone hiyo fursa. Naona hilo zao linakulia ukanda wa ubaridi nadhani acha nitafuatilia nijue kuwa lina limwaje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kama unania utatafta vyazo vyenye uhakika kuliko kutegemea jf, au nenda wizaran watakupa kila kitu mkuu
Sawa lakini hapa tupo jamii forum tupo kwa ajili ya kujuzana ukiwa una jua kitu ni bora kukiwasilisha hapa maana kila mtu atakaye ona atapata kitu kipya labda kitamsaidia kuweza kukifwatilia na kukitambua kwa undani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo kubeba mzgo wewe unaona haiwezekani ila mtafutaji anaetafuta kamtaji hapaswi kuchagua kazi. Hicho kilimo au fursa yoyote inahitaji mtaji sasa asipo fanya kazi hata kama ni hizi za kubeba mizigo au kumfanyia mtu yoyote kazi kama hakuna wakumapatia mtaji atafanyaje ili apate mtaji wa kuanzia..? Kilimo kina taka mtaji maana kama hauna shamba utakodi shamba na uandae shamba na utafute mbegu na mbolea bado mazao yanavyokua kuna palizi kuna kunyunyizia dawa na mbolea za kukuzia. Hivyo hapo nimeoinisha vitu vinavyotaka mtaji na visivyo hitaji mitaji sijui unaweza kurudia kuusoma tena huu uzi.

Na toa wazo au mbadala unaoona wewe utasaidia kupata kujikwamua. Maana shida ni pakuanzia ndipo tunapojaribu kupaelezea. Kuna mhitimu kwao hawana shamba na hana wa kumpa mtaji afanye nini. Afu kazi ya kubeba mzigo usiidharau nenda masokoni mijini afu jichanganye na waulize watu walianzia wapi kupata mitaji. Utakuja kuelewa nacho ongelea kama utajaribu kufikiria vizuri. Mfano mbebaji wa mizigo sokoni anayebeba viloba 30 kwa siku kuwapelekea wateja analipwa tuseme kila kiloba 1000 itategemea na umbali ina weza kuzidi au kupungua jumlisha mara 30 inaleta bei gani tufanye kakodi toroli toa 5000 ya toroli na kula 5000 toka ahsubuhi mpaka usiku anabakiwa na bei gani. Kwa mwezi.afanya hivyo mara hata siku 25 au 22 tu ana shilingi ngapi..?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu pakuanzia ni serikali iondoe kigezo cha kikundi ili kupewa mkopo wa halmashauri, hichi kigezo ni kizuizi kikubwa sana kwa vijana.

Ubaya hili haliongelewi ndio maana limebaki kuwepo, ila nguvu ikiwekwa hapo kwenye sharti la kikunfi ili kupewa mkopo litolewe itaondoa swali la mtaji utatoka wapi, then mambo mengine pia yatatatulika kwenye ishu ya kujiajiri.

Kazi ni kazi ila sharti iwe kazi yenye tija, na tunapohamasisha kazi fulani fulanibtuangalie na matokeo yake mbeleni. Tusiwe waongo kazi zisizo na tija ni kazi zinazoua kizazi na taifa.

Unaweza kupata pesa nyingi sana kwenye hizi kazi ila utatumia pesa nyingi ili kuifanya tu hiyo kazi, utalewa sana kisa stress, utafanya starehe kisa mateso na lawama hazitakuwa mbali na wewe pia. Sio rahisi hizo kazi zina gharama yake kubwa sana.

Ni bora kutuliza akili kuwa na mkakati na kufuata pesa ya halmashauri ili upate mtaji. Kuna vitu kama taifa tunategemea vifanywe na wasomi na huo ni ukweli.

Taifa haliwezi tegemea wasomi wake wabuni mradi wa kuwa makuli, aise hii ni hatari sana, miaka 10 ijayo hali itakuwaje sasa?, Tufikiri upya Mkuu.
 
Wazo zuri lakini ni kitu kinachokuwa na ugumu kwa mataifa yetu haya kuwawezesha wahitimu wote kwa kuwapa mtaji. Ni jambo la kuamua wewe kama wewe vipi uutafute mtaji. Kila kazi inalipa ikiwa na mzunguko mzuri. Serikali haijawawezesha wahitimu wasubirie mpaka lini kuwezeshwa ikiwa miaka ina kimbia. Hizo hela za halmashauri kuzipata ni taratibu ambazo sijazijua vizuri. Ila yote ya yote kuelekezana na kupashana namna ya kupata pa kuanzia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom