SoC01 Wahitimu wa Vyuo na Maisha ya utafutaji Mtaani

SoC01 Wahitimu wa Vyuo na Maisha ya utafutaji Mtaani

Stories of Change - 2021 Competition

Theb

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2019
Posts
3,927
Reaction score
7,276
Habari zenu wana Jamii Forums, hususani jukwaa hili la "Stories of Change". Ni tumaini langu wote ni wazima.

Andiko hili litaangazia maisha ya vijana wahitimu wa vyuo waliotegemea kuajiriwa na hali imekua tofauti na matarajio yao. Mwanzo, nitaelezea maisha ya mtaani, changamoto zinazo wakabili na vipi watatue hizo changamoto, Pili, nitaelezea fursa zisizohitaji mitaji na zenye kuhitaji mitaji. Tatu, nitaelezea mchango wa serikali na sekta binafsi katika kuwasaidia vijana kupata ajira na kujiajiri. Mwisho, nitamalizia kwa kutoa ushauri wangu katika kuwawezesha vijana wahitimu kujikwamua.

Maisha ya mtaani katika jamii zetu karibia kote yana mfanano kwa asilimia kubwa. Kuanzia ngazi ya familia za wahitimu walio wengi zinafanana kiuchumi, kitamaduni na hata kimalengo. Familia nyingi katika jamii zetu Tanzania tunasoma ili tuajiriwe na sio kujiajiri kwa waliowengi, hali iliyopo kwa sasa imeenda kinyume na malengo na matarijio ya vijana waliokuwa wanasoma na wanaoendelea kusoma mashuleni mpaka vyuoni.

CHANGAMOTO ZINAZO WAKABILI VIJANA WAHITIMU KATIKA UTAFUTAJI.

1. Kushindwa kujiamini na kushindwa kuikubali hali halisi iliyopo. Wengi wameshindwa kujiamini na kufikiria nje ya kitu walichosomea na kuanza kitu kipya ina wawia ngumu.

2. Mazingira yanayo wazunguka wahitimu, jamii ina wapa wakati mgumu kwa kuwahukumu kuwa wamesoma bure, elimu yao haina faida. Hili sio sawa.

3. Ukosefu wa muunganiko baina ya wahitimu na waliotangulia kwenye utafutaji, hapa unakuta wahitimu hawana muunganiko na waliotangulia kwenye utafutaji mitaani.

4. Ukosefu wa mitaji, hususani kwenye biashara au fursa zinazohitaji mitaji.

5. Kukosa uelewa katika utafutaji wenyewe. Kutozijua fursa au kutozitambua biashara na majira yake. Maana kila biashara ina majira yake.

6. Kuchagua kazi. Baadhi ya wahitimu hii changamoto kubwa kwao. Hawako tayari kubeba hata mizigo wanaona aibu au wanaona haiba yao hawastahili kubeba mizigo.

7. Mfumo na mitaala ya elimu nchini haikidhi dhumuni la kujiajiri kwa sababu imejikita katika nadharia zaidi na sio hali halisi katika kujiajiri.

JINSI YA KUPAMBANA NA HIZO CHANGAMOTO:-

1. Wazazi wasaidie watoto wao kuchagua fani zitakazo wawezesha kujiajiri pindi watakapo hitimu vyuoni.

2. Kujikubali, kujitambua na kujichanganya na watafutaji wengine mitaani bila kuwaza au kujutia muda uliopoteza shuleni na vyuoni.

3. Kukubali hali halisi hususani kuwa tayari kwa kazi yoyote bila kuchagua kazi. Mfano baadhi ya wahitimu ni ngumu kufanya kazi kama kuuza mkaa au kununua chupa za plastiki zilizotumika kwa kuhofia taaluma yake au watu watamuonaje.

4. Kuzitambua fursa na kuwa tayari kupambana nazo maana utafutaji mtaani ni ushindani.

5. Kufanya uchunguzi wa biashara unayotaka kwenda kuanzisha, hapa itahitaji kutafiti kwa kile unachotaka kufanya mtaani.

6. Kupunguza matumizi yale yasiyo muhimu. Kuwa na matumizi sahihi ya fedha. Mfano waache unywaji wa pombe, kubet, uvutaji wa sigara au ulevi wowote na anasa zingine zinazo hitaji pesa.

7. Kufanya uchaguzi sahihi wa kile unachoweza kukifanya mtaani na sio kufuata mkumbo. Fanya unachokipenda na unachokiweza

8. Usisahau kutunza kile unachokipata hata kama kidogo. (Bandu bandu humaliza gogo)

FURSA ZINAZOWEZA KUSAIDIA WAHITIMU KATIKA UTAFUTAJI MTAANI

1. Fursa zisizo hitaji mitaji na zisizo hitaji mitaji mikubwa sana. (Hizi kwa ajili ya kuanza kujipatia mitaji kidogo kidogo)

(i) Vibarua viwandani
Kwa wale wahitimu waliopo mijini kuna viwanda, vipo vibarua vya kutwa na wale wanaolipwa kwa wiki viwandani. Kuna kubeba mizigo viwandani kupakia na kupakua mizigo inayoingia na inayotoka na kazi zingine kulingana na kiwanda husika.

(ii) Fursa kwenye standi za mabasi ya abiria
Pia kwenye standi za mabasi kuna baadhi ya fursa zisizohitaji mitaji au zinazohitaji mitaji midogo. Mfano kubeba mizigo ya abiria kuwa wakala wa kukata tiketi na kuunza bidhaa ndogo ndogo kama karanga maji, juisi na matunda.

(iii) Kununua plastiki na kwenda kuziuza
Hapa kuna hii fursa ya kununua plastiki na kwenda kuuza mfano kilo moja unanunua kuanzia 300 hadi 400 na kuuza iliyosagwa ni kuanzia 800 hadi 1200 isiyo sagwa ni 800 bei ya kuuza. Hii ni fursa japo inadharauliwa.

(iv) Kuwa dalali wa mazao shambani au magari ya kusafirisha mizigo au dalali wa nyumba na viwanja
Haihitaji mtaji kwenye kuanza uaminifu wako na kujua chimbo za unachofanya ndio mtaji wako.

(v) Kuanzisha twisheni (tuition) mtaani kwenu
Hii pia saa zingine haihitaji mtaji itahitaji tu utayari wako na uwepo wa wanafunzi wanaosoma na kuitangaza. Japo maeneo mengine hii haina nafasi maana muitiko unakua mdogo hasa vijijini.

(vi) Kubeba mizigo kwenye masoko kupakua na kupakia mazao na bidhaa mbalimbali
Tunaweza kuidharau lakini ni fursa ukibeba mizigo 25 yenye kulipwa 1000 kila mzigo kwa siku una shilingi 25000. Haitaki mtu mwenye aibu na usharobaro.

(v). Kipaji kiwe cha uandishi, uimbaji, ususi, uchoraji, na michezo
Kipaji pia ni fursa kubwa tena isiyo hitaji mtaji ila inahitaji utayari wako kujituma na ubunifu zaidi na uvumilivu uliomithilika.

(vi). Kuwa saidia fundi ujenzi, fundi wa kuchomelea dirisha na mageti, fundi randa nk,

Kusaidia fundi atakulipa kidogo itategemea na kazi iliyopo hapo unajifunza ufundi, kujiandaa kuwa fundi ili ujitegemee. Mfano saidia fundi ujenzi hulipwa sio chini ya 10,000/= kwa siku.

(vii). Kuuza mahindi ya kuchoma na ya kuchemsha.
Hii hususani sehemu zenye mikusanyiko, stand za mabasi, barabarani na kwenye vyombo vya usafiri hususani mabasi.

2. Fursa zinazohitaji mitaji mikubwa au ya kiasi. Nitataja baadhi na ambazo ni rahisi kuzitambua kama ifuatavyo:-

(i). Kununua mazao mashambani na kuleta mjini kwenye masoko
Hapa kuna mahindi, viazi aina zote, mchele mboga mboga kutoka mashambani kuleta mijini. Kikubwa kufanya tathmini vizuri.

(ii). Umachinga wa kuuza vitu mtaani kando ya barabara au kutembeza au kutengeneza banda lako sehemu inayoonekana kwa wateja

(iii). Kilimo, uvuvi na ufugaji

Kilimo kinahitaji uwe na shamba, mbegu, pembejeo za kilimo mbolea na dawa za kupulizia kuua vijidudu hatarishi kwa mazao nacho kilimo kitategemea na aina ya mazao unayolima.

Ufugaji
Mfano wa kuku lazima uwe na mtaji wa kununua kuku, pumba, uduvi na mifupa.

(iv). Udereva boda boda au bajaji
Huu nao utahitaji uwe na mtaji au upate ya mtu. Mfano bado boda hakosi kupata 25000 hadi 30000 kwa siku.

(v). Kuanzisha saloon zote za kunyoa nywele na kusuka nywele
Hapa kwa wanaume na kwa wanawake kuna kunyoa na kusuka hivyo sehemu uliyopo ikiwa na uhitaji hii ni fursa.

(vi). Huduma ya kutuma pesa kwa njia za simu.
Kuanzisha M pesa, airtel money, tigo pesa na halopesa.

(vii). Kuanzisha mgahawa, mama ntilie au ukaangaji wa chipsi na kuchoma mishkaki.

(viii). Kununua na kuuza vyuma chakavu. Hii pia ni fursa inayolipa vizuri ni jambo la kufanya uchunguzi na kuthubutu.

MCHANGO WA SERIKALI PAMOJA NA SEKTA BINAFSI KATIKA KUWASAIDIA WAHITIMU.

1. Kuwapa motisha, semina na muongozo wa namna ya kuanza ujasiriamali.

2. Kuwapatia mikopo yenye riba nafuu au isiyo na riba kabisa.(walemavu wapewe kipaumbele).
Serikali na sekta binafsi kupitia benki na taasisi zingine za kifedha watoe mikopo kwa wahitimu. Pia familia zenye uwezo ziwawezeshe vijana wao waliohitimu.

3. Mazingira wezeshi kwa watafutaji wanaoanza kutafuta mtaani. Hapa kuwaondolea kodi kandamizi. Kuboresha miundo mbinu zaidi mijini na vijijini itasaidia usafirishaji wa bidhaa.

4. Serikali itengeneze mahusiano mazuri na mataifa mengine. Itasaidi kutanua soko la nje kwenye ajira na bidhaa au mazao yatakayo zalishwa nchini.

5. Serikali na sekta binafsi zinapaswa kwa pamoja kuwaamini vijana na kuondoa kigezo cha uzoefu katika kuwapatia kazi/ajira.

6. Serikali na sekta binafsi ziwashirikishe vijana katika juhudi za kuwainua iwe mikopo au semina za kiujasiriamali.

7. Mfumo wa elimu uboreshwe hususani mitaala. Elimu itolewe kwa vitendo na ijikite katika kuwaandaa kujitegemea/kujiajiri.

8. Wazazi, jamii, serikali na mashirika binafsi kwa pamoja watambue na kudhamini karama au vipaji vya wanafunzi toka wakiwa wadogo na kuvisimamia kwa lengo la kujiajiri baadae.

9. Wahitimu wote wenye ulemavu wapatiwe kazi serikalini na mashirika binafsi moja kwa moja. Mfano ajira za mwaka 2021 ualimu na afya serikali haikuwaacha nyuma hili liendelee kila wakati.

10.Kuwe na uwazi katika masuala ya ajira. Iwe za serikali mpaka mashirika binafsi.

11. Ukabila, rushwa, umaeneo na udini viepukwe katika kuwapatia vijana ajira.

12. Waliofikia umri wa kustaafu wasiruhusiwe kuendelea kufanya kazi.

13. Uwepo mgawanyo wa kazi.
Ili mtu mmoja asifanye kazi zaidi ya kituo kimoja.

USHAURI WANGU KWA VIJANA WAHITIMU KATIKA UTAFUTAJI
Ushauri wangu kwa vijana wasaka tonge wahanga wa ajira na vijana woote watafutaji kwa ujumla napenda kutoa ushauri kama ifuatavyo:-

(i). Uvumilivu kwenye hizo fursa tunazoenda kuanzisha maana nako pia tutakutana na changamoto ila tusivunjike moyo na tusikate tamaa mapambano yaendelee.

(ii). Tuzijue hizo fursa na kutambua majira ya hizo fursa itasaidia kutambua muda gani muafaka wa kuanza tusikurupuke kuna kuanguka pia.

(iii). Kama unamtaji usianze na pesa yote ya mtaji maana hauna uhakika 100% kuwa itaenda sawa hivyo kujipanga kwa hilo ni muhimu.

(iv). Kupata ushauri kwa waliofanikiwa ni muhimu itakuongezea maarifa kwa yale usiyo yajua.

(v). Usimuamini kila mtu katika utafutaji wako wengine watakukwamisha. Mfano wanao kopa ni sumu kwako unaeanza utafutaji.

(vi). Tambua hitaji la jamii ikizungukayo. Kama jamii inataka mahindi wapelekee mahindi na sio mchele.

(vii). Ishi vizuri na watu na waheshimu watu kwa imani zao makabila yao na rangi zao. Kuwa na lugha nzuri.

(viii). Zingatia usafi kwenye ofisi yako kuwa na mpangilio mzuri pia toa huduma iliyo bora sio bora huduma.

(ix). Muhimu na la kukumbukwa kila unapopata kidogo kitunze kadri kinavyo kua kiwekeze kitaleta zaidi.

(X). Fanya shughuli halali, kuwa muaminifu, uadilifu ni muhimu na kufuata sheria za nchi yetu katika utafutaji.
 
Upvote 1.6K
Ni kweli ,serikali iki deal na ku identify masoko ya mazao ndani na nje ya nchi then kulima iwe kazi ya wananchi/vijana tutamove foward. i think vijana wengi wanasita kuingia kwenye kilimo sababu ya unpredictability ..wakiwa na uhakika wa kuuza na kupata faida wengi wataingia kwenye kilimo.

Pili nahisi hii ya kuuza mazao ya kilimo nje ya Tanzania inahitaji mjadala mpana, in my opinion kuwe na Brand ambayo ni ya serikali, ndiyo itumike kuuza mazao nje ya nchi, people are more willing to buy something from trusted source, a brand that they can rely on, that can be traced. (trustability/dependability/traceability), hivyo basi serikali iji brand na kuchukua jukumu la kununua mazao kutoka kwa wananchi na kuuza nje. Trust me zikiwekwa brand mbili moja ya serikali nyingine ya random person from the country utashangaa hio ya serikali inanunuliwa zaidi. Sijui mnaonaje hili??lol

Umegusia viwanda,ni kweli tunahitaji sana vitu kama nyanya ingependeza kuwa proccessed,packed,kuna wakati zinakuwa bei mno na kuna wakati ni nyingi mno, proccessed makopo yangesaidia...lol
Kuhusu soko. Ukiangalia nature ya mikoa yenye baridi inazalisha mboga mboga na matunda ambazo zinaweza kuuzwa mpaka nchi za nje. Mfano kuna maapple ya kutoka South Afrika yanakuja hapa nchini tunayaona sio kwamba hatuwezi kuyazalisha hapana tunaweza ila hatujawa serious km wenzetu. Mikoq kama Iringa, njombe, kilimanjaro, arusha na mingine yenye ubaridi halisi inaweza kuzalisha maapple km yale na yakauzwa ndani na nje.
 
Tanzania tuna ardhi nzuri kweli. Maana ukiangalia kwa East Afrika hapa Tanzania ndio nchi inayozalisha vyakula kwa kiwango kikibwa ni vyema kwa taifa letu lingekua na sera zinazoeleweka na hiyo brand unayosema ambayo itajivisha jukumu la kuongoza uuzwaji wa bidhaa toka Tanzania tuchukulie mfano brand hiyo iwe kama German zama zilizopita ilihusika kwa ubora wa bidhaa. Ukiangalia historia walikua wanaaminika kwa bidhaa bora. Kuhusu brand waangalie ubora zaidi mbona kilimo kingelipa zaidi na zaidi
Fact
 
Kuhusu soko. Ukiangalia nature ya mikoa yenye baridi inazalisha mboga mboga na matunda ambazo zinaweza kuuzwa mpaka nchi za nje. Mfano kuna maapple ya kutoka South Afrika yanakuja hapa nchini tunayaona sio kwamba hatuwezi kuyazalisha hapana tunaweza ila hatujawa serious km wenzetu. Mikoq kama Iringa, njombe, kilimanjaro, arusha na mingine yenye ubaridi halisi inaweza kuzalisha maapple km yale na yakauzwa ndani na nje.
Ulivyotaja apple nkaingia google kutafuta picha moja ama mbili ili wasiojua haya matunda wayaone hapa. Ni ukweli tunaweza kuzalisha tofaa(apple) kutokana na aina za hali ya hewa nchini kwetu mikoa uliyotaja hiyo pia kuna sehemu inaitwa Lushoto ipo Tanga wanalima apple lakini kilimo chao ni local sana katika haya matunda na hali ya hewa inawaruhusu tatizo zao hili limechukuliwa poa sana na jamii au Taifa kwa ujumla. Kule Lushoto ndoo moja ya apple tena zile apple local wanauza 10,000/= kipindi chake maana hayawi.kila wakati kulingana na majira ya mvua. Wao wanapanda miti local tu kama muembe unavyopanda local tu afu wanauza ikiwa tayari kwa kuzaa ma apple. Ila inachukua miaka kadhaa apple za kienyeji kuwa tayari. Niwazo zuri serikali na wadau wa kilimo wa fikiria na hili wawapatie wakulima mbegu bora za matunda hayo na watanue soko la nje na ndani tutfanikiwa[emoji1313]picha ya tofaa au apple
e2121b6a7e660ed3.jpg
63fed06e7e7e0ed8.jpg
(picha hizi kutoka homeliness bustani)
 
Ulivyotaja apple nkaingia google kutafuta picha moja ama mbili ili wasiojua haya matunda wayaone hapa. Ni ukweli tunaweza kuzalisha tofaa(apple) kutokana na aina za hali ya hewa nchini kwetu mikoa uliyotaja hiyo pia kuna sehemu inaitwa Lushoto ipo Tanga wanalima apple lakini kilimo chao ni local sana katika haya matunda na hali ya hewa inawaruhusu tatizo zao hili limechukuliwa poa sana na jamii au Taifa kwa ujumla. Kule Lushoto ndoo moja ya apple tena zile apple local wanauza 10,000/= kipindi chake maana hayawi.kila wakati kulingana na majira ya mvua. Wao wanapanda miti local tu kama muembe unavyopanda local tu afu wanauza ikiwa tayari kwa kuzaa ma apple. Ila inachukua miaka kadhaa apple za kienyeji kuwa tayari. Niwazo zuri serikali na wadau wa kilimo wa fikiria na hili wawapatie wakulima mbegu bora za matunda hayo na watanue soko la nje na ndani tutfanikiwa[emoji1313]picha ya tofaa au appleView attachment 1930694View attachment 1930693(picha hizi kutoka homeliness bustani)
Kwenye kilimo mazao ni mengi sambamba na hali za hewa nchini mbona kuna fursa nyingi kwenye kilimo. Kilimo kwanza serikali yetu ile kauli mbiu ya kilimo kwanza iliishia wapi
 
Kaka na wewe karibu hapa umwage mauzoefu uliyonayo.iwe kilimo, biashara, uwindaji, ajira vyote unakaribishwa kwa maana naamini hukosi lolote mkuu[emoji1317][emoji1317]
 
Kwenye kilimo mazao ni mengi sambamba na hali za hewa nchini mbona kuna fursa nyingi kwenye kilimo. Kilimo kwanza serikali yetu ile kauli mbiu ya kilimo kwanza iliishia wapi
Mimi naweza kukuelezea mazao tu niliyoyaona mkoa nilioishi na kusoma hapo mkoa wa Tanga unamatunda mengi haswaa kuanzia maembe tambarare yote ile Tanga mjini, kuja muheza, korogwe, handeni na kuja lushoto hizo wilaya zingine sija bahatika kufika ili hizi nimefika kipindi ya machungwa yanakua mengi kiasi kwamba utinzaji unahitajika kwa maana ni matunda ya msimu, maembe hivyo hivyo, njoo kule lushoto kwenye hzo apple pia kuna peas, kuna matunda mengine mengi tu majina yake nimesahau yote hukua kwenye ubaridi yanalika mijini sio kidogo lakini mwamko wa kuyalima ni mdogo kutokana na kuwa msimu ukifika yapo mengi hadi yanaoza sasa mkulima kwanini ajipe hasara anaona bora akate miti ya matunda alime mboga mboga au mahindi
 
Kwenye kilimo mazao ni mengi sambamba na hali za hewa nchini mbona kuna fursa nyingi kwenye kilimo. Kilimo kwanza serikali yetu ile kauli mbiu ya kilimo kwanza iliishia wapi
Mkuu kuna na hizi baadhi ya mboga zinalimwa maeneo yenye ubaridi nchini mfano Arusha, mbeya, njombe, lushoto, kilimanjaro nk mboga hizi zinasoko zuri tu kwa ndani kwa maana hotel na migahawa karibia yote mijini inategemea mboga hizi lakini hali ikiboreshwa wakulima wakapewa elimu ya kilimo hiki na kutengenezewa mazingira bora ya utunzaji wa mazao haya hakika na.tukapata soko nje ya nchi kwa maana hizi mboga pia zinauzwa nje ya nchi sio kitu cha kuficha au uongo hizi zinasafirishwa kwenda nje zinalika ulaya saana maana huko ndio asili ya hizi mboga.

Picha zote nimetoa mtandaoni.
1. Mboga hii huitwa broccoli nadhani kama sijakosea jina lake ila ndio hilo
xbroccoli-flowerheads.jpg.pagespeed.ic.RcX_eRKyv5.jpg

Mbaga hii hukuzwq sana sana Arusha, kilimanjaro na Tanga lushoto nk japo wakulima wengi hulima local walati wenzetu hulima kwa njia ya kisasa

2. Mboga hii huitwa cauliflowers
_108296302_cauliflowergetty.jpg
picha hii kutoka BBC.
Hii nayo inaendana na hiyo ya juu. Kwa hali ya hewa nk

Mambo ni mengi mkuu..
 
Ulivyotaja apple nkaingia google kutafuta picha moja ama mbili ili wasiojua haya matunda wayaone hapa. Ni ukweli tunaweza kuzalisha tofaa(apple) kutokana na aina za hali ya hewa nchini kwetu mikoa uliyotaja hiyo pia kuna sehemu inaitwa Lushoto ipo Tanga wanalima apple lakini kilimo chao ni local sana katika haya matunda na hali ya hewa inawaruhusu tatizo zao hili limechukuliwa poa sana na jamii au Taifa kwa ujumla. Kule Lushoto ndoo moja ya apple tena zile apple local wanauza 10,000/= kipindi chake maana hayawi.kila wakati kulingana na majira ya mvua. Wao wanapanda miti local tu kama muembe unavyopanda local tu afu wanauza ikiwa tayari kwa kuzaa ma apple. Ila inachukua miaka kadhaa apple za kienyeji kuwa tayari. Niwazo zuri serikali na wadau wa kilimo wa fikiria na hili wawapatie wakulima mbegu bora za matunda hayo na watanue soko la nje na ndani tutfanikiwa
emoji1313.png
picha ya tofaa au appleView attachment 1930694View attachment 1930693(picha hizi kutoka homeliness bustani)
Kwenye kilimo mazao ni mengi sambamba na hali za hewa nchini mbona kuna fursa nyingi kwenye kilimo. Kilimo kwanza serikali yetu ile kauli mbiu ya kilimo kwanza iliishia wapi
Mkuu kuna na hizi baadhi ya mboga zinalimwa maeneo yenye ubaridi nchini mfano Arusha, mbeya, njombe, lushoto, kilimanjaro nk mboga hizi zinasoko zuri tu kwa ndani kwa maana hotel na migahawa karibia yote mijini inategemea mboga hizi lakini hali ikiboreshwa wakulima wakapewa elimu ya kilimo hiki na kutengenezewa mazingira bora ya utunzaji wa mazao haya hakika na.tukapata soko nje ya nchi kwa maana hizi mboga pia zinauzwa nje ya nchi sio kitu cha kuficha au uongo hizi zinasafirishwa kwenda nje zinalika ulaya saana maana huko ndio asili ya hizi mboga.

Picha zote nimetoa mtandaoni.
1. Mboga hii huitwa broccoli nadhani kama sijakosea jina lake ila ndio hiloView attachment 1930747
Mbaga hii hukuzwq sana sana Arusha, kilimanjaro na Tanga lushoto nk japo wakulima wengi hulima local walati wenzetu hulima kwa njia ya kisasa

2. Mboga hii huitwa cauliflowers View attachment 1930748picha hii kutoka BBC.
Hii nayo inaendana na hiyo ya juu. Kwa hali ya hewa nk

Mambo ni mengi mkuu..
Hakika mambo ni mengi.
 
Kwenye kilimo mazao ni mengi sambamba na hali za hewa nchini mbona kuna fursa nyingi kwenye kilimo. Kilimo kwanza serikali yetu ile kauli mbiu ya kilimo kwanza iliishia wapi

Hakika mambo ni mengi.
Sana. Shukran mate mchango wako na uheshimu humu. Usisite kila wakati kujaza maujuzi yoyote hapa. Hapa ni nyumbani kwako karibu kila wakati[emoji1317][emoji1317][emoji1303]
 
Mkuu, asante sana kwa kuonyesha fursa zilizopo ambazo wadogo zetu wanaweza kuzitumia, tatizo ni jamii yetu kwa ujumla wake, imetuaminisha kuwa msomi hastahili kufanya shughuli zisizo rasmi kama vile kubeba mizigo stendi, kuendesha bodaboda nk. Jamii itakuona kama mtu aliyefeli na asiyeelimika.

Vv
 
Kweli. Ila inabidi vijana wahitimu watumie hata hiyo waliopata na kuja mtaani kubuni au kujua kipi wakifanye na hatua zao katika kujikwamua ndizo.zitaifundisha jamii kutokudharau kazi yoyote. Kila kazi inapimwa kwa matokeo au tuseme mafanikio ha hiyo kazi. Vijana wanatakiwa wasiogope jamii inavyowachukulia wakifanya shughuli si sizo rasmi. Kikubwa wajue kuzipambania ndoto zao itakuja kubadilisha mtazamo hasi katika jamii zetu.
 
Habari zenu wana Jamii Forums, hususani jukwaa hili la stories of change. Ni tumaini langu nyote ni wazima.

Andiko hili litaangazia maisha ya vijana wahitimu wa vyuo waliotegemea kuajiriwa na hali imekua tofauti na matarajio yao.

Naanza kwa kuelezea maisha ya mtaani na baadhi ya fursa zenye kuhitaji mitaji na zisizohitaji mitaji na changamoto zake na vipi tunaweza kuzikabili changamoto na kutuwezesha kupita katika baadhi ya hizo fursa na tuweze kujikwamua.

Maisha ya mtaani katika jamii zetu karibia kote yana mfanano kwa asilimia kubwa. Kuanzia ngazi ya familia za wahitimu walio wengi zinafanana kichumi kitamaduni na hata kimalengo. Familia nyingi za jamii zetu Tanzania tunasoma ili tuajiriwe na sio kujiajiri kwa waliowengi, hali iliyopo kwa sasa sio siri imeenda kinyume na malengo na matarijio ya vijana waliokuwa wanasoma na wanaoendelea kusoma mashuleni mpaka vyuoni.

NITAANZA KUELEZEA CHANGAMOTO ZINAZO WAKABILI VIJANA WAHITIMU KATIKA UTAFUTAJI.

1. Kutokujiamini na kutokubaliana na hali halisi iliyopo. Wengi hawa jiamini na wanashindwa kufikiria nje ya kitu walichosomea na kukianza kitu kipya ina wawia ngumu.

2. Mazingira yanoyowazunguka wahitimu, jamii ina wapa wakati mgumu kwa kuwahukumu kuwa wamesoma bure, elimu yao haina faida. Hili sio sawa.

3. Kukosa kampani au muunganiko na watu waliotangulia kwenye mitaa, hapa unakuta wahitimu hawana muunganiko na waliotangulia kwenye mitaa kiutafutaji.

4. Kutokua na mitaji, hususani kwenye biashara au fursa zinazohitaji mitaji.

5. Kutokua na uelewa wa mitaa na utaftaji wenyewe. Yaani kutozijua fursa au kutozitambua biashara na majira yake. Maana kila biashara ina majira yake.

6. Kuchagua kazi. Hii inahusika saana baadhi ya wahitimu hii changamoto kubwa kwao. Hawako tayari kubeba hata gunia wanaona aibu au wanaona haiba yao hawastahili kubeba gunia.

JINSI GANI WANAWEZA KUPAMBANA NA HIZI CHANGAMOTO:-

1. Kujikubali na kujichanganya na watafutaji wengine mitaani bila kuwaza au kujutia muda uliopoteza shuleni na vyuoni.

2. Kukubali hali halisi hususani kuwa tayari kwa kazi yoyote bila kuchagua kazi. Mfano baadhi ya wahitimu ina muwia ngumu kufanya kazi kama kuuza mkaa au kununua chupa za plastiki zilizotumika kwa kuhofia taaluma yake au watu watamuonaje.

3. Kuzitambua fursa na kuwa tayari kupambana nazo maana utaftaji mtaani ni ushindani.

4. Kuyajua mazingira ya biashara unayotaka kwenda kuanzisha, hapa itahitaji muunganiko na wanaoitambua biashara husika unayotaka kuanzisha kwenye mazingira unayopanga.

5. Kupunguza matumizi yale yasiyo muhimu, hapa matumizi yasiyomuhimu ambayo yanafuja pesa hainabudi kuyaacha. Mfano unywaji wa pombe, kubet, uvutaji wa sigara au ulevi wowote na anasa zingine zinazo hitaji pesa.

6. Kufanya uchaguzi sahihi wa kile unachoweza kukifanya mtaani na sio kufwata mkumbo. Je mhitimu unaweza kitu gani kama ni kilimo basi fanya kilimo kama ni ufundi fanya ufundi.

7. Usisahau kutunza kile unachokipata hata kama kidogo. (Bandu bandu humaliza gogo)

FURSA ZILIZOPO KATIKA JAMII ZETU AMBAZO WAHITIMU AU MTAFUTAJI YEYOTE ANAWEZA KUZITAZAMA NA KUANZA KUJIPATIA KIPATO KUPITIA HIZO FURSA

1. Fursa zisizo hitaji mitaji na zisizo hitaji mitaji mikubwa sana. (Hizi kwa ajili ya kuanza kujipatia mitaji kidogo kidogo)

(i) Vibarua viwandani
Kwa wale wahitimu waliopo mijini kuliko na viwanda kuna upatikanaji wa vibarua wa kutwa na wale wanaolipwa kwa wiki kwenye viwanda. Kuna kubeba mizigo viwandani kupakia na kupakua mizigo inayoingia na inayotoka na kazi zingine kulingana na kiwanda husika.

(ii) Fursa kwenye standi za mabasi ya abiria
Pia kwenye standi za mabasi kuna baadhi ya fursa zisizohitaji mitaji au zinazohitaji mitaji midogo, mfano kubeba mizigo ya abiria kuwa wakala wa kukata tiketi na kuunza bidhaa ndogo ndogo kama karanga maji, juisi na matunda.

(iii) Kununua plastiki na kwenda kuziuza
Hapa kuna hii fursa ya kununua plastiki na kwenda kuuza mfano kilo moja unanunua kuanzia 300 hadi 400 na kuuza iliyosagwa ni kuanzia 800 hadi 1200 isiyo sagwa ni 800 bei ya kuuza. Hii ni fursa japo inadharauliwa.

(iv) Kuwa dalali wa mazao shambani au magari ya kusafirisha mizigo au dalali wa nyumba viwanja nk
Hii nayo haihitaji mtaji kwenye kuanza uaminifu wako na kujua chimbo za unachofanya ndio mtaji wako.

(v) Kuanzisha twisheni (tuition) mtaani kwenu
Hii pia saa zingine haihitaji mtaji itahitaji tu utayari wako na uwepo wa wanafunzi wanaosoma na kuitangaza. Japo maeneo mengine hii haina nafasi maana muitiko unakua mdogo hasa vijijini.

(vi) Kubeba mizigo kwenye masoko kupakua na kupakia mazao na bidhaa mbalimbali
Tunaweza kuidharau lakini ni fursa ukibeba mizigo 25 yenye kulipwa 1000 kila mzigo kwa siku una shilingi 25000. Haitaki mtu mwenye aibu na usharobaro.

(v). Kipaji kiwe cha uandishi, uimbaji, ususi, uchoraji, na michezo
Kipaji pia ni fursa kubwa tena isiyo hitaji mtaji ila itataka utayari wako kujituma na ubunifu zaidi na uvumilivu uliomithilika.

(vi). Kuwa saidia fundi ujenzi, fundi wa kuchomelea dirisha na mageti, fundi randa nk, (Ufundi wa aina yoyote).

Kusaidia fundi atakulipa kidogo itategemea na kazi iliyopo hapo unajifunza ufundi, kujiandaa kuwa fundi ili ujitegemee. Mfano saidia fundi ujenzi hulipwa sio chini ya 10,000/= kwa siku.

(vii). Kuuza mahindi ya kuchoma na ya kuchemsha.
Hii hususani sehemu zenye mikusanyiko, stand za mabasi, barabarani na kwenye vyombo vya usafiri hususani mabasi.

2. Fursa zinazohitaji mitaji mikubwa au ya kiasi. Nitataja baadhi na ambazo ni rahisi kujichanganya kama ifuatavyo:-

(i). Kununua mazao mashambani na kuleta mjini kwenye masoko
Hapa kuna mahindi, viazi aina zote, mchele mboga mboga kutoka mashambani kuleta mijini. Kikubwa kufanya tathmini vizuri.

(ii). Umachinga wa kuuza vitu mtaani kando ya barabara au kutembeza au kutengeneza banda lako sehemu inayoonekana kwa wateja

(iii). Kilimo, uvuvi na ufugaji

Kilimo kinahitaji uwe na shamba, mbegu, pembejeo za kilimo mbolea na dawa za kupulizia kuua vijidudu hatarishi kwa mazao nacho kilimo kitategemea na aina ya mazao unayolima.

Ufugaji
Mfano wa kuku lazima uwe na mtaji wa kununua kuku, pumba, uduvi na mifupa.

(iv). Udereva boda boda au bajaji
Huu nao utahitaji uwe na mtaji au upate ya mtu. Mfano bado boda hakosi kupata 25000 hadi 30000 kwa siku.

(v). Kuanzisha saloon zote za kunyoa nywele na kusuka nywele
Hapa kwa wanaume na kwa wanawake kuna kunyoa na kusuka hivyo sehemu uliyopo kama pana uhitaji hii ni fursa.

(vi). Huduma ya kutuma pesa kwa njia za simu.
Kuanzisha M pesa, airtel money, tigo pesa na halopesa.

(vii). Kuanzisha mgahawa, mama ntilie au ukaangaji wa chipsi na kuchoma mishkaki.

(viii). Kununua na kuuza vyuma chakavu. Hii pia ni fursa inayolipa vizuri ni jambo la kufanya uchunguzi na kuthubutu.

MAMBO YANAYO WEZA KUTEKELEZWA NA SERIKALI PAMOJA NA SEKTA BINAFSI KUWASAIDIA VIJANA WAHITIMU.

1. Kuwapa motisha na muongozo wa kuanzisha vikundi vya ujasiriamali. Hapa serikali inapaswa kuwa mhusika mkuu wakuwapa vijana wasio na kazi usaidizi.

2. Kuwapatia mikopo yenye riba nafuu au isiyo na riba kabisa.(Bejeti iwe na fungu lao)
Serikali na sekta binafsi kupitia benki na taasisi zingine za kifedha wanaowajibu wakuwawezesha kwa mikopo isiyo na riba.

3. Mazingira wezeshi kwa watafutaji wanaoanza kutafuta mtaani. Hapa kuwaondolea kodi kandamizi.

4. Kuwapatia semina mbali mbali za kiujasirimali. Hapa lazima kuwapa semina juu ya fursa zilizopo na vipi wataweza kukabiliana na changamoto katika utafutaji.

5. Serikali na sekta binafsi zinapaswa kwa pamoja kuwaamini vijana na kuondoa kigezo cha uzoefu katika kuwapatia kazi.

6. Serikali na sekta binafsi kuwa husisha vijana katika juhudi za kuwainua iwe mikopo au semina za kiujasiriamali.

7. Mfumo wa elimu uboreshwe hususani mitaala iwe rahisi kuwa andaa vijana kujitegemea kulingana na elimu waipatayo.

8.Kuwe na uwazi katika masuala ya ajira. Iwe za serikali mpaka mashirika binafsi uwazi uwepo.

9. Ukabila, rushwa, umaeneo na udini viepukwe katika kuwapatia vijana ajira.

10. Waliofikia umri wa kustaafu wasiruhusiwe kuendelea kufanya kazi.

11. Uwepo mgawanyo wa kazi.
Ili mtu mmoja asifanye kazi zaidi ya kituo kimoja.

Hitimisho
Ushauri wangu kwa vijana wasaka tonge wahanga wa ajira na vijana woote watafutaji kwa ujumla napenda kutoa ushauri kama ufuatao:-

(i). Uvumilivu kwenye hizo fursa tunazoenda kuanzisha maana nako pia tutakutana na changamoto ila tusivunjike moyo na tusikate tamaa mapambano yaendelee.

(ii). Tuzijue hizo fursa na kutambua majira ya hizo fursa itasaidia kutambua muda gani muafaka wa kuanza tusikurupuke kuna kuanguka pia.

(iii). Kama unamtaji usianze na pesa yote ya mtaji maana hauna uhakika 100% kuwa itaenda sawa hivyo kujipanga kwa hilo ni muhimu.

(iv). Kupata ushauri kwa waliofanikiwa ni muhimu itakuongezea maarifa kwa yale usiyo yajua.

(v). Usimwamini kila mtu katika kufanya utafutaji wako wengine watakukwamisha. Mfano wanao kopa ni sumu kwako unaeanza utafutaji.

(vi). Tambua hitaji la jamii ikizungukayo. Kama jamii inataka mahindi wapelekee mahindi na sio mchele.

(vii). Ishi vizuri na watu na waheshimu watu kwa imani zao makabila yao na rangi zao.

(viii). Kuwa msafi au zingatia usafi kwenye ofisi yako kuwa na mpangilio mzuri na boresha mazingira ya ofisi yako.

(ix). Muhimu na la kukumbukwa kila unapopata kidogo kitunze kadri kinavyo kua kiwekeze kitaleta zaidi.

(X). Fanya shughuli halali na kufuata sheria za nchi yetu katika utafutaji wako.

Hapa nimefikia mwisho wa andiko langu. Natumaini kidogo kitaeleweka kwa wengi haijaelezea kila kitu ila nimeelezea kwa uchache kwa yale niliyojionea na kujifunza mtaani.

MUHIMU:
Msisahau kupigia kura andiko hili [emoji1317].
Safi sana.upvoted
 
Back
Top Bottom