SoC01 Wahitimu wa Vyuo na Maisha ya utafutaji Mtaani

Stories of Change - 2021 Competition

Theb

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2019
Posts
3,927
Reaction score
7,276
Habari zenu wana Jamii Forums, hususani jukwaa hili la "Stories of Change". Ni tumaini langu wote ni wazima.

Andiko hili litaangazia maisha ya vijana wahitimu wa vyuo waliotegemea kuajiriwa na hali imekua tofauti na matarajio yao. Mwanzo, nitaelezea maisha ya mtaani, changamoto zinazo wakabili na vipi watatue hizo changamoto, Pili, nitaelezea fursa zisizohitaji mitaji na zenye kuhitaji mitaji. Tatu, nitaelezea mchango wa serikali na sekta binafsi katika kuwasaidia vijana kupata ajira na kujiajiri. Mwisho, nitamalizia kwa kutoa ushauri wangu katika kuwawezesha vijana wahitimu kujikwamua.

Maisha ya mtaani katika jamii zetu karibia kote yana mfanano kwa asilimia kubwa. Kuanzia ngazi ya familia za wahitimu walio wengi zinafanana kiuchumi, kitamaduni na hata kimalengo. Familia nyingi katika jamii zetu Tanzania tunasoma ili tuajiriwe na sio kujiajiri kwa waliowengi, hali iliyopo kwa sasa imeenda kinyume na malengo na matarijio ya vijana waliokuwa wanasoma na wanaoendelea kusoma mashuleni mpaka vyuoni.

CHANGAMOTO ZINAZO WAKABILI VIJANA WAHITIMU KATIKA UTAFUTAJI.

1. Kushindwa kujiamini na kushindwa kuikubali hali halisi iliyopo. Wengi wameshindwa kujiamini na kufikiria nje ya kitu walichosomea na kuanza kitu kipya ina wawia ngumu.

2. Mazingira yanayo wazunguka wahitimu, jamii ina wapa wakati mgumu kwa kuwahukumu kuwa wamesoma bure, elimu yao haina faida. Hili sio sawa.

3. Ukosefu wa muunganiko baina ya wahitimu na waliotangulia kwenye utafutaji, hapa unakuta wahitimu hawana muunganiko na waliotangulia kwenye utafutaji mitaani.

4. Ukosefu wa mitaji, hususani kwenye biashara au fursa zinazohitaji mitaji.

5. Kukosa uelewa katika utafutaji wenyewe. Kutozijua fursa au kutozitambua biashara na majira yake. Maana kila biashara ina majira yake.

6. Kuchagua kazi. Baadhi ya wahitimu hii changamoto kubwa kwao. Hawako tayari kubeba hata mizigo wanaona aibu au wanaona haiba yao hawastahili kubeba mizigo.

7. Mfumo na mitaala ya elimu nchini haikidhi dhumuni la kujiajiri kwa sababu imejikita katika nadharia zaidi na sio hali halisi katika kujiajiri.

JINSI YA KUPAMBANA NA HIZO CHANGAMOTO:-

1. Wazazi wasaidie watoto wao kuchagua fani zitakazo wawezesha kujiajiri pindi watakapo hitimu vyuoni.

2. Kujikubali, kujitambua na kujichanganya na watafutaji wengine mitaani bila kuwaza au kujutia muda uliopoteza shuleni na vyuoni.

3. Kukubali hali halisi hususani kuwa tayari kwa kazi yoyote bila kuchagua kazi. Mfano baadhi ya wahitimu ni ngumu kufanya kazi kama kuuza mkaa au kununua chupa za plastiki zilizotumika kwa kuhofia taaluma yake au watu watamuonaje.

4. Kuzitambua fursa na kuwa tayari kupambana nazo maana utafutaji mtaani ni ushindani.

5. Kufanya uchunguzi wa biashara unayotaka kwenda kuanzisha, hapa itahitaji kutafiti kwa kile unachotaka kufanya mtaani.

6. Kupunguza matumizi yale yasiyo muhimu. Kuwa na matumizi sahihi ya fedha. Mfano waache unywaji wa pombe, kubet, uvutaji wa sigara au ulevi wowote na anasa zingine zinazo hitaji pesa.

7. Kufanya uchaguzi sahihi wa kile unachoweza kukifanya mtaani na sio kufuata mkumbo. Fanya unachokipenda na unachokiweza

8. Usisahau kutunza kile unachokipata hata kama kidogo. (Bandu bandu humaliza gogo)

FURSA ZINAZOWEZA KUSAIDIA WAHITIMU KATIKA UTAFUTAJI MTAANI

1. Fursa zisizo hitaji mitaji na zisizo hitaji mitaji mikubwa sana. (Hizi kwa ajili ya kuanza kujipatia mitaji kidogo kidogo)

(i) Vibarua viwandani
Kwa wale wahitimu waliopo mijini kuna viwanda, vipo vibarua vya kutwa na wale wanaolipwa kwa wiki viwandani. Kuna kubeba mizigo viwandani kupakia na kupakua mizigo inayoingia na inayotoka na kazi zingine kulingana na kiwanda husika.

(ii) Fursa kwenye standi za mabasi ya abiria
Pia kwenye standi za mabasi kuna baadhi ya fursa zisizohitaji mitaji au zinazohitaji mitaji midogo. Mfano kubeba mizigo ya abiria kuwa wakala wa kukata tiketi na kuunza bidhaa ndogo ndogo kama karanga maji, juisi na matunda.

(iii) Kununua plastiki na kwenda kuziuza
Hapa kuna hii fursa ya kununua plastiki na kwenda kuuza mfano kilo moja unanunua kuanzia 300 hadi 400 na kuuza iliyosagwa ni kuanzia 800 hadi 1200 isiyo sagwa ni 800 bei ya kuuza. Hii ni fursa japo inadharauliwa.

(iv) Kuwa dalali wa mazao shambani au magari ya kusafirisha mizigo au dalali wa nyumba na viwanja
Haihitaji mtaji kwenye kuanza uaminifu wako na kujua chimbo za unachofanya ndio mtaji wako.

(v) Kuanzisha twisheni (tuition) mtaani kwenu
Hii pia saa zingine haihitaji mtaji itahitaji tu utayari wako na uwepo wa wanafunzi wanaosoma na kuitangaza. Japo maeneo mengine hii haina nafasi maana muitiko unakua mdogo hasa vijijini.

(vi) Kubeba mizigo kwenye masoko kupakua na kupakia mazao na bidhaa mbalimbali
Tunaweza kuidharau lakini ni fursa ukibeba mizigo 25 yenye kulipwa 1000 kila mzigo kwa siku una shilingi 25000. Haitaki mtu mwenye aibu na usharobaro.

(v). Kipaji kiwe cha uandishi, uimbaji, ususi, uchoraji, na michezo
Kipaji pia ni fursa kubwa tena isiyo hitaji mtaji ila inahitaji utayari wako kujituma na ubunifu zaidi na uvumilivu uliomithilika.

(vi). Kuwa saidia fundi ujenzi, fundi wa kuchomelea dirisha na mageti, fundi randa nk,

Kusaidia fundi atakulipa kidogo itategemea na kazi iliyopo hapo unajifunza ufundi, kujiandaa kuwa fundi ili ujitegemee. Mfano saidia fundi ujenzi hulipwa sio chini ya 10,000/= kwa siku.

(vii). Kuuza mahindi ya kuchoma na ya kuchemsha.
Hii hususani sehemu zenye mikusanyiko, stand za mabasi, barabarani na kwenye vyombo vya usafiri hususani mabasi.

2. Fursa zinazohitaji mitaji mikubwa au ya kiasi. Nitataja baadhi na ambazo ni rahisi kuzitambua kama ifuatavyo:-

(i). Kununua mazao mashambani na kuleta mjini kwenye masoko
Hapa kuna mahindi, viazi aina zote, mchele mboga mboga kutoka mashambani kuleta mijini. Kikubwa kufanya tathmini vizuri.

(ii). Umachinga wa kuuza vitu mtaani kando ya barabara au kutembeza au kutengeneza banda lako sehemu inayoonekana kwa wateja

(iii). Kilimo, uvuvi na ufugaji

Kilimo kinahitaji uwe na shamba, mbegu, pembejeo za kilimo mbolea na dawa za kupulizia kuua vijidudu hatarishi kwa mazao nacho kilimo kitategemea na aina ya mazao unayolima.

Ufugaji
Mfano wa kuku lazima uwe na mtaji wa kununua kuku, pumba, uduvi na mifupa.

(iv). Udereva boda boda au bajaji
Huu nao utahitaji uwe na mtaji au upate ya mtu. Mfano bado boda hakosi kupata 25000 hadi 30000 kwa siku.

(v). Kuanzisha saloon zote za kunyoa nywele na kusuka nywele
Hapa kwa wanaume na kwa wanawake kuna kunyoa na kusuka hivyo sehemu uliyopo ikiwa na uhitaji hii ni fursa.

(vi). Huduma ya kutuma pesa kwa njia za simu.
Kuanzisha M pesa, airtel money, tigo pesa na halopesa.

(vii). Kuanzisha mgahawa, mama ntilie au ukaangaji wa chipsi na kuchoma mishkaki.

(viii). Kununua na kuuza vyuma chakavu. Hii pia ni fursa inayolipa vizuri ni jambo la kufanya uchunguzi na kuthubutu.

MCHANGO WA SERIKALI PAMOJA NA SEKTA BINAFSI KATIKA KUWASAIDIA WAHITIMU.

1. Kuwapa motisha, semina na muongozo wa namna ya kuanza ujasiriamali.

2. Kuwapatia mikopo yenye riba nafuu au isiyo na riba kabisa.(walemavu wapewe kipaumbele).
Serikali na sekta binafsi kupitia benki na taasisi zingine za kifedha watoe mikopo kwa wahitimu. Pia familia zenye uwezo ziwawezeshe vijana wao waliohitimu.

3. Mazingira wezeshi kwa watafutaji wanaoanza kutafuta mtaani. Hapa kuwaondolea kodi kandamizi. Kuboresha miundo mbinu zaidi mijini na vijijini itasaidia usafirishaji wa bidhaa.

4. Serikali itengeneze mahusiano mazuri na mataifa mengine. Itasaidi kutanua soko la nje kwenye ajira na bidhaa au mazao yatakayo zalishwa nchini.

5. Serikali na sekta binafsi zinapaswa kwa pamoja kuwaamini vijana na kuondoa kigezo cha uzoefu katika kuwapatia kazi/ajira.

6. Serikali na sekta binafsi ziwashirikishe vijana katika juhudi za kuwainua iwe mikopo au semina za kiujasiriamali.

7. Mfumo wa elimu uboreshwe hususani mitaala. Elimu itolewe kwa vitendo na ijikite katika kuwaandaa kujitegemea/kujiajiri.

8. Wazazi, jamii, serikali na mashirika binafsi kwa pamoja watambue na kudhamini karama au vipaji vya wanafunzi toka wakiwa wadogo na kuvisimamia kwa lengo la kujiajiri baadae.

9. Wahitimu wote wenye ulemavu wapatiwe kazi serikalini na mashirika binafsi moja kwa moja. Mfano ajira za mwaka 2021 ualimu na afya serikali haikuwaacha nyuma hili liendelee kila wakati.

10.Kuwe na uwazi katika masuala ya ajira. Iwe za serikali mpaka mashirika binafsi.

11. Ukabila, rushwa, umaeneo na udini viepukwe katika kuwapatia vijana ajira.

12. Waliofikia umri wa kustaafu wasiruhusiwe kuendelea kufanya kazi.

13. Uwepo mgawanyo wa kazi.
Ili mtu mmoja asifanye kazi zaidi ya kituo kimoja.

USHAURI WANGU KWA VIJANA WAHITIMU KATIKA UTAFUTAJI
Ushauri wangu kwa vijana wasaka tonge wahanga wa ajira na vijana woote watafutaji kwa ujumla napenda kutoa ushauri kama ifuatavyo:-

(i). Uvumilivu kwenye hizo fursa tunazoenda kuanzisha maana nako pia tutakutana na changamoto ila tusivunjike moyo na tusikate tamaa mapambano yaendelee.

(ii). Tuzijue hizo fursa na kutambua majira ya hizo fursa itasaidia kutambua muda gani muafaka wa kuanza tusikurupuke kuna kuanguka pia.

(iii). Kama unamtaji usianze na pesa yote ya mtaji maana hauna uhakika 100% kuwa itaenda sawa hivyo kujipanga kwa hilo ni muhimu.

(iv). Kupata ushauri kwa waliofanikiwa ni muhimu itakuongezea maarifa kwa yale usiyo yajua.

(v). Usimuamini kila mtu katika utafutaji wako wengine watakukwamisha. Mfano wanao kopa ni sumu kwako unaeanza utafutaji.

(vi). Tambua hitaji la jamii ikizungukayo. Kama jamii inataka mahindi wapelekee mahindi na sio mchele.

(vii). Ishi vizuri na watu na waheshimu watu kwa imani zao makabila yao na rangi zao. Kuwa na lugha nzuri.

(viii). Zingatia usafi kwenye ofisi yako kuwa na mpangilio mzuri pia toa huduma iliyo bora sio bora huduma.

(ix). Muhimu na la kukumbukwa kila unapopata kidogo kitunze kadri kinavyo kua kiwekeze kitaleta zaidi.

(X). Fanya shughuli halali, kuwa muaminifu, uadilifu ni muhimu na kufuata sheria za nchi yetu katika utafutaji.
 
Upvote 1.6K
Kiongozi naomba nirudie kukupongeza kwa andiko lako. Kisha nijikite kwenye mada kwa machache nitakayoweza kuyaandika.
1. Umetaja suala la wastaafu kupisha vijana. Hilo sina pingamizi nalo. Kumekuwa na ubinafsi mkubwa serikalini, seniors hawataki kuwapatia ujuzi juniors. Wanataka kila kitu wafuatwe kwa ajili ya wao kutoa muongozo.
Lakini vijana wa kisasa nao kuna matatizo, wachache wanakuwa serious, wengi hawataki kujichosha kuanzia chuo hadi kazini. Matokeo yake tuanabaki kusifia wazee kuwa mahiri kwenye vitengo fulani fulani. Hii inafanya hata muda wao unapofika kustaafu wanalazimika au wanaombwa kubaki.
Kifupi hakuna Succession plan.
Imefikia hatua ukitaka ugombane na mkongwe kazini mwambie akufundishe kazi, anaona unamchunguza.
Hii inaenda sambamba na kulundika majukumu kwa mtu mmoja.

2.Uundaji wa vikundi vya ujasiriamali.
Serikali na wadau wasiishie tu kuunda vikundi na kuwapa mikopo. Watoe elimu juu ya miradi ya vikundi kuanzia uzalishaji, uongezaji thamani, masuala ya masoko (marketing strategies) na usimamizi wa fedha.
Tujaribu kuhama kutoka kutoa mikopo kwa lengo la kutafuta kukubalika, bali kuisaidia jamii. Ikibidi vitolewe zaidi vitendea kazi na sehemu ndogo tu ya fedha za uendeshaji badala ya mikopo ya hela ambayo inaishia kuliwa.

3. Kutojiamini kwa wahitimu. Inatokana na mifumo yetu ya elimu. Mfumo unatuandaa kufaulu mitihani na siyo kutujengea ujuzi. Ndiyo maana (ukiacha wahitimu) hata wafanyakazi wengi hawawezi ku take risk na kufanya biashara kubwa sababu hawana ujuzi japo mitaji wanayo.

Nini kifanyike. Kama ulivyoelezea, jamii iwe na msaada badala ya kuwatia hofu na kutowafungulia fursa.
Familia zetu zione kusoma ni kujiongezea maarifa ili kuendana na soko la ushindani kwenye nyanja za ubunifu, uwekezaji, biashara nk.
Ziweke mazingira ya kuwasaidia mitaji na kuwatia moyo baada ya kukosa ajira.

4. Unaweza kujiuliza, kwanini unapoenda mbali na nyumbani unaziona fursa nyingi zingine hazihitaji hata mitaji mikubwa pamoja na courage ya kufanya kazi bila hofu.
Jibu ni moja tu, mazingira yanatudumaza. Tukubali kujichanganya, kutobagua kazi kama ulivyosema nk. Hakuna ufahali bila kitu mfukoni, zamani ndiyo wasomi wangeweza kuchagua kazi za kufanya, maana walikuwa wachache.
Sasa kama degree zinauza maji na karanga, wewe ni nani hadi usiweze?
Kikubwa ni namna gani unafanya kazi zako kwa kuhusisha taaluma yako.

Uligusia fursa za kukatisha tiketi za mabasi.
Tunatakiwa kubadili dhana ya kuwa wakatisha tiketi, bodaboda, dereva wa ubber, wauza vinywaji nk ni watu wa levels za chini. Hizo ni kazi kama zingine na zinahitaji elimu pia.
Leo hii kuna watu wanatoa huduma za tiketi, kama ni mgeni na ukabahatika kukutana naye mara ya kwanza basi utatamani awe mteja wako siku zote na ndugu zako utawaelekeza kwake kutokana na ubora wa huduma anazokupa. Kwa kufanya hivyo, anatengeneza pesa.

5. Kilimo, Ufugaji na Uvuvi.
Huku kuna fursa ambazo wengi hawajaziona au wanadharau.
Kilimo kina changamoto mwanzo, lakini ukichagua mazao kwa usahihi ukapanda kwa kufuata kanuni. Utapunguza gharama za uzalishaji, utavuna muda ambao soko linahitaji bidhaa na mazao yenye ubora sokoni.

Ufugaji hali kadhalika, tena huu unaweza kuanza hata kwa eneo dogo la kupewa na ndugu, mtaji kidogo na baada ya muda ukawa na mradi mkubwa sana. Kikubwa kwenye ufugaji usichoke kujifunza.

Wito wangu kwa wanaobania wengine furs
Usidhani kuwa wingi wa watu wanaofanya biashara aina moja ndiyo kuua biashara ya hiyo. Muhimu ni jinsi gani unajua mahitaji ya wateja wako, namna unavyotoa huduma(ubunifu) na uaminifu wako.

Sikutaka kuongelea la udalali, unajua kwanini?.........[emoji23]
Shukran mkuu kwanza kwa mchango wako hapa[emoji1317][emoji1317]

Ni.kweli baadhibya vijana au wahitimu hawapo makini wanapoaminiwa na kupewa kazi iwe serikalini au sekta binafsi. Hili kwangu mimi naweza kusema linatokana na mfumo tuliojiwekea kama taifa wakutowaamini vijana. Maana kama hawajui kitu inapaswa wahusishwe na wapewe muongozo na pia wakikosea wasiachwe bali ndio njia ya kukifunza zaidi.
Nije kwa vijana wenyewe tunapaswa hujitambua kukubali kujitoa kwa dhati katika kutekeleza shughuli yoyote tutakayo pata kuaminiwa na kuajiriwa.

Kubwa zaidi vijana tupende kukifunza na kukishusha kwa yale tusiyo yajua itatupa mwanya wa kuaminiwa zaidi na wanaojua tusiyo yajua.
 
Hakika
 
Kiongozi naomba nirudie kukupongeza kwa andiko lako. Kisha nijikite kwenye mada kwa machache nitakayoweza kuyaandika.
1. Umetaja suala la wastaafu kupisha vijana. Hilo sina pingamizi nalo. Kumekuwa na ubinafsi mkubwa serikalini, seniors hawataki kuwapatia ujuzi juniors. Wanataka kila kitu wafuatwe kwa ajili ya wao kutoa muongozo.
Lakini vijana wa kisasa nao kuna matatizo, wachache wanakuwa serious, wengi hawataki kujichosha kuanzia chuo hadi kazini. Matokeo yake tuanabaki kusifia wazee kuwa mahiri kwenye vitengo fulani fulani. Hii inafanya hata muda wao unapofika kustaafu wanalazimika au wanaombwa kubaki.
Kifupi hakuna Succession plan.
Imefikia hatua ukitaka ugombane na mkongwe kazini mwambie akufundishe kazi, anaona unamchunguza.
Hii inaenda sambamba na kulundika majukumu kwa mtu mmoja.

2.Uundaji wa vikundi vya ujasiriamali.
Serikali na wadau wasiishie tu kuunda vikundi na kuwapa mikopo. Watoe elimu juu ya miradi ya vikundi kuanzia uzalishaji, uongezaji thamani, masuala ya masoko (marketing strategies) na usimamizi wa fedha.
Tujaribu kuhama kutoka kutoa mikopo kwa lengo la kutafuta kukubalika, bali kuisaidia jamii. Ikibidi vitolewe zaidi vitendea kazi na sehemu ndogo tu ya fedha za uendeshaji badala ya mikopo ya hela ambayo inaishia kuliwa.

3. Kutojiamini kwa wahitimu. Inatokana na mifumo yetu ya elimu. Mfumo unatuandaa kufaulu mitihani na siyo kutujengea ujuzi. Ndiyo maana (ukiacha wahitimu) hata wafanyakazi wengi hawawezi ku take risk na kufanya biashara kubwa sababu hawana ujuzi japo mitaji wanayo.

Nini kifanyike. Kama ulivyoelezea, jamii iwe na msaada badala ya kuwatia hofu na kutowafungulia fursa.
Familia zetu zione kusoma ni kujiongezea maarifa ili kuendana na soko la ushindani kwenye nyanja za ubunifu, uwekezaji, biashara nk.
Ziweke mazingira ya kuwasaidia mitaji na kuwatia moyo baada ya kukosa ajira.

4. Unaweza kujiuliza, kwanini unapoenda mbali na nyumbani unaziona fursa nyingi zingine hazihitaji hata mitaji mikubwa pamoja na courage ya kufanya kazi bila hofu.
Jibu ni moja tu, mazingira yanatudumaza. Tukubali kujichanganya, kutobagua kazi kama ulivyosema nk. Hakuna ufahali bila kitu mfukoni, zamani ndiyo wasomi wangeweza kuchagua kazi za kufanya, maana walikuwa wachache.
Sasa kama degree zinauza maji na karanga, wewe ni nani hadi usiweze?
Kikubwa ni namna gani unafanya kazi zako kwa kuhusisha taaluma yako.

Uligusia fursa za kukatisha tiketi za mabasi.
Tunatakiwa kubadili dhana ya kuwa wakatisha tiketi, bodaboda, dereva wa ubber, wauza vinywaji nk ni watu wa levels za chini. Hizo ni kazi kama zingine na zinahitaji elimu pia.
Leo hii kuna watu wanatoa huduma za tiketi, kama ni mgeni na ukabahatika kukutana naye mara ya kwanza basi utatamani awe mteja wako siku zote na ndugu zako utawaelekeza kwake kutokana na ubora wa huduma anazokupa. Kwa kufanya hivyo, anatengeneza pesa.

5. Kilimo, Ufugaji na Uvuvi.
Huku kuna fursa ambazo wengi hawajaziona au wanadharau.
Kilimo kina changamoto mwanzo, lakini ukichagua mazao kwa usahihi ukapanda kwa kufuata kanuni. Utapunguza gharama za uzalishaji, utavuna muda ambao soko linahitaji bidhaa na mazao yenye ubora sokoni.

Ufugaji hali kadhalika, tena huu unaweza kuanza hata kwa eneo dogo la kupewa na ndugu, mtaji kidogo na baada ya muda ukawa na mradi mkubwa sana. Kikubwa kwenye ufugaji usichoke kujifunza.

Wito wangu kwa wanaobania wengine furs
Usidhani kuwa wingi wa watu wanaofanya biashara aina moja ndiyo kuua biashara ya hiyo. Muhimu ni jinsi gani unajua mahitaji ya wateja wako, namna unavyotoa huduma(ubunifu) na uaminifu wako.

Sikutaka kuongelea la udalali, unajua kwanini?.........[emoji23]
Hapo kwenye kilimo na ufugaji kwangu mimi naona kwa kuwa kuna baadhi ya vijana hawajui hata kushika jembe au hata kufuga mfugo wowote ingependeza mashuleni kukawa na somo la kilimo kuanzia shule za misingi mpaka sekondari kwa wanafunzi wote.

Serikali yetu kuna kipindi ilifuta somo la agriculture kwa baadhi ya shule. Pia bookeeping na commerce yalifutwa ilihali yangesaidia kuwapa vijana maarifa kiasi ambayo yangekua msaada kwao.

Kuna somo la stadi za kazi shule ya msingu sijui.kwa sasa lipo au la.?? Kilindi nasoma shule ya msingi nakumbuka hili somo lilikua linatufundisha stadi za maisha ambazo zingine zimegeuka mtaani ni furaa ila ajabu lile somo hatukufanyia mtihani wa mwisho wa kuelekea sekondari.
 
Na hilo la kuona fursa ukiwa nje na kwenu ni kweli ukitoka kwenu ulipokulia ukaenda sehemu nyingine ni rahisi kung'amua fursa zilizopo kwa sababu.

1. Ile hofu ya watu watanichukuliaje haipo kwako tena huwaogopi watu kwa kuwa hamjuani kabla.

2. Utakua katika utafutaji zaidi na sio kufuatana na watu kama ukiwa kwenu ulipokulia.

3. Wale wa kukopa ukiwa ugenini ni.rahisi kulikataa hilo

4. Ugenini unakua huru zaidi
 
Kiongozi naomba nirudie kukupongeza kwa andiko lako. Kisha nijikite kwenye mada kwa machache nitakayoweza kuyaandika.
1. Umetaja suala la wastaafu kupisha vijana. Hilo sina pingamizi nalo. Kumekuwa na ubinafsi mkubwa serikalini, seniors hawataki kuwapatia ujuzi juniors. Wanataka kila kitu wafuatwe kwa ajili ya wao kutoa muongozo.
Lakini vijana wa kisasa nao kuna matatizo, wachache wanakuwa serious, wengi hawataki kujichosha kuanzia chuo hadi kazini. Matokeo yake tuanabaki kusifia wazee kuwa mahiri kwenye vitengo fulani fulani. Hii inafanya hata muda wao unapofika kustaafu wanalazimika au wanaombwa kubaki.
Kifupi hakuna Succession plan.
Imefikia hatua ukitaka ugombane na mkongwe kazini mwambie akufundishe kazi, anaona unamchunguza.
Hii inaenda sambamba na kulundika majukumu kwa mtu mmoja.

2.Uundaji wa vikundi vya ujasiriamali.
Serikali na wadau wasiishie tu kuunda vikundi na kuwapa mikopo. Watoe elimu juu ya miradi ya vikundi kuanzia uzalishaji, uongezaji thamani, masuala ya masoko (marketing strategies) na usimamizi wa fedha.
Tujaribu kuhama kutoka kutoa mikopo kwa lengo la kutafuta kukubalika, bali kuisaidia jamii. Ikibidi vitolewe zaidi vitendea kazi na sehemu ndogo tu ya fedha za uendeshaji badala ya mikopo ya hela ambayo inaishia kuliwa.

3. Kutojiamini kwa wahitimu. Inatokana na mifumo yetu ya elimu. Mfumo unatuandaa kufaulu mitihani na siyo kutujengea ujuzi. Ndiyo maana (ukiacha wahitimu) hata wafanyakazi wengi hawawezi ku take risk na kufanya biashara kubwa sababu hawana ujuzi japo mitaji wanayo.

Nini kifanyike. Kama ulivyoelezea, jamii iwe na msaada badala ya kuwatia hofu na kutowafungulia fursa.
Familia zetu zione kusoma ni kujiongezea maarifa ili kuendana na soko la ushindani kwenye nyanja za ubunifu, uwekezaji, biashara nk.
Ziweke mazingira ya kuwasaidia mitaji na kuwatia moyo baada ya kukosa ajira.

4. Unaweza kujiuliza, kwanini unapoenda mbali na nyumbani unaziona fursa nyingi zingine hazihitaji hata mitaji mikubwa pamoja na courage ya kufanya kazi bila hofu.
Jibu ni moja tu, mazingira yanatudumaza. Tukubali kujichanganya, kutobagua kazi kama ulivyosema nk. Hakuna ufahali bila kitu mfukoni, zamani ndiyo wasomi wangeweza kuchagua kazi za kufanya, maana walikuwa wachache.
Sasa kama degree zinauza maji na karanga, wewe ni nani hadi usiweze?
Kikubwa ni namna gani unafanya kazi zako kwa kuhusisha taaluma yako.

Uligusia fursa za kukatisha tiketi za mabasi.
Tunatakiwa kubadili dhana ya kuwa wakatisha tiketi, bodaboda, dereva wa ubber, wauza vinywaji nk ni watu wa levels za chini. Hizo ni kazi kama zingine na zinahitaji elimu pia.
Leo hii kuna watu wanatoa huduma za tiketi, kama ni mgeni na ukabahatika kukutana naye mara ya kwanza basi utatamani awe mteja wako siku zote na ndugu zako utawaelekeza kwake kutokana na ubora wa huduma anazokupa. Kwa kufanya hivyo, anatengeneza pesa.

5. Kilimo, Ufugaji na Uvuvi.
Huku kuna fursa ambazo wengi hawajaziona au wanadharau.
Kilimo kina changamoto mwanzo, lakini ukichagua mazao kwa usahihi ukapanda kwa kufuata kanuni. Utapunguza gharama za uzalishaji, utavuna muda ambao soko linahitaji bidhaa na mazao yenye ubora sokoni.

Ufugaji hali kadhalika, tena huu unaweza kuanza hata kwa eneo dogo la kupewa na ndugu, mtaji kidogo na baada ya muda ukawa na mradi mkubwa sana. Kikubwa kwenye ufugaji usichoke kujifunza.

Wito wangu kwa wanaobania wengine furs
Usidhani kuwa wingi wa watu wanaofanya biashara aina moja ndiyo kuua biashara ya hiyo. Muhimu ni jinsi gani unajua mahitaji ya wateja wako, namna unavyotoa huduma(ubunifu) na uaminifu wako.

Sikutaka kuongelea la udalali, unajua kwanini?.........[emoji23]
Kwanini.hutaki kuuongelea udalali mkuu wakati masokoni tunaendesha biashara kwa kuwategemea madalali na wana mpaka vitambulisho vyao kabsa.
 
Hapo kwenye kilimo na ufugaji kwangu mimi naona kwa kuwa kuna baadhi ya vijana hawajui hata kushika jembe au hata kufuga mfugo wowote ingependeza mashuleni kukawa na somo la kilimo kuanzia shule za misingi mpaka sekondari kwa wanafunzi wote.

Serikali yetu kuna kipindi ilifuta somo la agriculture kwa baadhi ya shule. Pia bookeeping na commerce yalifutwa ilihali yangesaidia kuwapa vijana maarifa kiasi ambayo yangekua msaada kwao.

Kuna somo la stadi za kazi shule ya msingu sijui.kwa sasa lipo au la.?? Kilindi nasoma shule ya msingi nakumbuka hili somo lilikua linatufundisha stadi za maisha ambazo zingine zimegeuka mtaani ni furaa ila ajabu lile somo hatukufanyia mtihani wa mwisho wa kuelekea sekondari.
Elimu yetu kuna sehemu haitoi majibu ya changamoto za jamii.
Somo la agriculture kwa nchi kama yetu ni muhimu. Ila linoreshwe liache kufundisha kilimo cha babu na bibi, twende kwenye kilimo cha kisasa.
Stadi za kazi nadhani bado lipo, ingawa sijui materials contents zake (nimesoma enzi za EDU & Sayansi Kilimo).

Ukiachilia mbali kuboresha mitaala, hii ni kwa ajili ya vijana wa baadaye. Lakini tayari lipo kundi kubwa la vijana mtaani wanahitaji msaada kwa wakati.
 
Kweli. Stadi za kazi ipo nadhani lakini hawaifanyii mtihani.wa mwisho nakumbuka maana kipindi nasoma hatukulifanyia mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi hilo somo.
 
Elezea tu mkuu ndio vizuri walete ujuzi, uzoefu nk.
Ni kazi kama nyingine endapo itafanyika kwa umakini.

Achilia mbali kuwa wanapunguza nguvu ya makubaliano (bargaining power) baina ya muuzaji na mnunuzi, madalali wana mambo mengi sana

1. Baadhi wanatumia ushirikina kwenye kazi yao.
2. Hawaangalii maslahi ya mmiliki wa boashara au mzalishaji.
3. Wanataka kila sehemu kupata faida kubwa kumbe kuna kazi zinalipa nyingine hazilipi ila inakupa kazi nyingine itakayokulipa.

Huanza kidogo kama mzaha, kazi ikikolea huachi. Zaidi hujifunza utapeli na roho mbaya(hapa ndipo ushirikina unaanzia)

Wafanyakazi (baadhi na siyo wote) hutaka kufanyia udalali hadi mambo ambayo ni haki ya mtu. Hii inazaa rushwa and the alikes.

Lakini mwisho udalali unabaki kuwa kipaji asilia. Ndiyo maana kuna watu hawatambuliki kama madalali lakini matendo yana vinasaba vya udalali.
 
Ndio saa zingine baadhi ya madalali hujawa na tamaa na kukimbia hata na mali ya mteja. Zipo kesi nyingi za madalali waliokimbia na pesa za mauzo ya mizigo kwenye masoko na hata huko mashambani dalali kapewa pesa atafute mzigo hisika tamaa zimemjaa kakimbia na pesa ya mteja. Au amtafutie mteja bidhaa isiyo bora ambayo kwa mteja inakua ni hasara.

Na suala la ushirikina lipo kila sehemu iwe ofisini, mtaani, kwenye shughuli yoyote uahirikina unaweza kuwepo kikubwa ni je mhusika nayeye ana imani ipi..? Hili ni suala la kiimani zaidi japo yapo tena sio kidogo.
 
[emoji120]
 
Swali lako la pili.

Nikweli vipaji navyo visipo tumika kwa kufuata tamaduni za jamii zetu vinaweza kutupa matokeo mabaya kama kuhamasisha vitendo viovu.

Mfano mziki na uigizaji suala la maadili lisipo zingatiwa baaadhi ya kazi zao wasanii zinatujengea jamii isiyo na maadili. Hivyo wote wanaohusika na masuala km hayo inabidi wawekewe sheria za kuwazuia kuenda kinyuma na maadili yetu[emoji1317][emoji1317]
Na maadili wanayaharibu hawa wavaa nusu uchi tena wanavujisha mpaka mipicha na video zao za ngono ilehali wanajua kuwa jamii yetu haiendani na huo ufska wao. Nashangaa baadhi ya wasanii wanajiita kioo cha jamii hivi ni kwa ufska wao au kwa lipi.?? Japo sio wote ni baadhi tu
 
Ndio saa zingine baadhi ya madalali hujawa na tamaa na kukimbia hata na mali ya mteja. Zipo kesi nyingi za madalali waliokimbia na pesa za mauzo ya mizigo kwenye masoko na hata huko mashambani dalali kapewa pesa atafute mzigo hisika tamaa zimemjaa kakimbia na pesa ya mteja. Au amtafutie mteja bidhaa isiyo bora ambayo kwa mteja inakua ni hasara.

Na suala la ushirikina lipo kila sehemu iwe ofisini, mtaani, kwenye shughuli yoyote uahirikina unaweza kuwepo kikubwa ni je mhusika nayeye ana imani ipi..? Hili ni suala la kiimani zaidi japo yapo tena sio kidogo.
Mkuu udalali bila ya kuwa mshirikina na mtu wa fitina huwezi kufanya au hata ukifanya mwezi utaisha hata huulizwi na wateja.
Ngoja nikupe mfano mmoja hivi ambao umemtokea jirani yangu ambaye yeye kazi yake ni fundi ujenzi,sasa ikatokea hapo hapo mtaani kwetu kuna nyumba ilikuwa inauzwa basi ingawa jamaa kazi yake ni fundi ujenzi akaona si vibaya afanye udalali kwenye ile nyumba inayouzwa ili apate 10 percent maisha yasonge.
Basi jamaa akaanza kutafuta wateja sehemu mbalimbali basi kwenye pitapita huko akakutana na mama mmoja anatafuta nyumba ya kununua jamaa akaona hii inaweza ikawa bahati nikapiga hela.
Basi yule mama akatoa appointment kuwa nitakuja siku fulani kuiona hiyo nyumba kisha wakapeana mawasiliano,basi kweli ilivyofika ile siku mama akaja kukutana na jamaa akampeleka kumuonesha ile nyumba.
Mama akaingia ndani akaikagua kila mahali kisha akasema sawa nimeiona ngoja nikajipange nikitaka kuja tena nitakufahamisha kisha wakaagana mama akaondoka zake,ikumbukwe yule mama pale ni mgeni hafahamiki ametoka mbali ni kama mtu wa kutoka manzese aende kuulizia nyumba mbezi.
Basi jamaa akawa anasubiri kwa hamu mama aje kununua avute pesa yake ya udalali lakini ikawa siku zinasogea hapigiwi simu na yule mama.
Basi ikapita kama wiki hivi jamaa akawa anapita kwenye ule mtaa inakouzwa ile nyumba akaja kushangaa anawakuta madalali wapo na yuleyule mama kwenye ile ile nyumba wanafanya mauziano na mama kalipia pesa zote siku hiyo hiyo jamaa yangu akaishiwa nguvu.
Jamaa akabaki na maswali mengi je hawa madalali wa hapa mtaani walimpataje huyu mama,walimjulia wapi maana pale ni mgeni kabisa,Na kwa nini siku ya kwanza alikataa kulipia pesa lakini walivyomwita madalali wenyewe hakuchomoa kalipa siku hiyo hiyo tu.
Hivi ndivyo ilivyo kwenye kazi ya udalali ndugu yangu.
 
Kiongozi naomba nirudie kukupongeza kwa andiko lako. Kisha nijikite kwenye mada kwa machache nitakayoweza kuyaandika.
1. Umetaja suala la wastaafu kupisha vijana. Hilo sina pingamizi nalo. Kumekuwa na ubinafsi mkubwa serikalini, seniors hawataki kuwapatia ujuzi juniors. Wanataka kila kitu wafuatwe kwa ajili ya wao kutoa muongozo.
Lakini vijana wa kisasa nao kuna matatizo, wachache wanakuwa serious, wengi hawataki kujichosha kuanzia chuo hadi kazini. Matokeo yake tuanabaki kusifia wazee kuwa mahiri kwenye vitengo fulani fulani. Hii inafanya hata muda wao unapofika kustaafu wanalazimika au wanaombwa kubaki.
Kifupi hakuna Succession plan.
Imefikia hatua ukitaka ugombane na mkongwe kazini mwambie akufundishe kazi, anaona unamchunguza.
Hii inaenda sambamba na kulundika majukumu kwa mtu mmoja.

2.Uundaji wa vikundi vya ujasiriamali.
Serikali na wadau wasiishie tu kuunda vikundi na kuwapa mikopo. Watoe elimu juu ya miradi ya vikundi kuanzia uzalishaji, uongezaji thamani, masuala ya masoko (marketing strategies) na usimamizi wa fedha.
Tujaribu kuhama kutoka kutoa mikopo kwa lengo la kutafuta kukubalika, bali kuisaidia jamii. Ikibidi vitolewe zaidi vitendea kazi na sehemu ndogo tu ya fedha za uendeshaji badala ya mikopo ya hela ambayo inaishia kuliwa.

3. Kutojiamini kwa wahitimu. Inatokana na mifumo yetu ya elimu. Mfumo unatuandaa kufaulu mitihani na siyo kutujengea ujuzi. Ndiyo maana (ukiacha wahitimu) hata wafanyakazi wengi hawawezi ku take risk na kufanya biashara kubwa sababu hawana ujuzi japo mitaji wanayo.

Nini kifanyike. Kama ulivyoelezea, jamii iwe na msaada badala ya kuwatia hofu na kutowafungulia fursa.
Familia zetu zione kusoma ni kujiongezea maarifa ili kuendana na soko la ushindani kwenye nyanja za ubunifu, uwekezaji, biashara nk.
Ziweke mazingira ya kuwasaidia mitaji na kuwatia moyo baada ya kukosa ajira.

4. Unaweza kujiuliza, kwanini unapoenda mbali na nyumbani unaziona fursa nyingi zingine hazihitaji hata mitaji mikubwa pamoja na courage ya kufanya kazi bila hofu.
Jibu ni moja tu, mazingira yanatudumaza. Tukubali kujichanganya, kutobagua kazi kama ulivyosema nk. Hakuna ufahali bila kitu mfukoni, zamani ndiyo wasomi wangeweza kuchagua kazi za kufanya, maana walikuwa wachache.
Sasa kama degree zinauza maji na karanga, wewe ni nani hadi usiweze?
Kikubwa ni namna gani unafanya kazi zako kwa kuhusisha taaluma yako.

Uligusia fursa za kukatisha tiketi za mabasi.
Tunatakiwa kubadili dhana ya kuwa wakatisha tiketi, bodaboda, dereva wa ubber, wauza vinywaji nk ni watu wa levels za chini. Hizo ni kazi kama zingine na zinahitaji elimu pia.
Leo hii kuna watu wanatoa huduma za tiketi, kama ni mgeni na ukabahatika kukutana naye mara ya kwanza basi utatamani awe mteja wako siku zote na ndugu zako utawaelekeza kwake kutokana na ubora wa huduma anazokupa. Kwa kufanya hivyo, anatengeneza pesa.

5. Kilimo, Ufugaji na Uvuvi.
Huku kuna fursa ambazo wengi hawajaziona au wanadharau.
Kilimo kina changamoto mwanzo, lakini ukichagua mazao kwa usahihi ukapanda kwa kufuata kanuni. Utapunguza gharama za uzalishaji, utavuna muda ambao soko linahitaji bidhaa na mazao yenye ubora sokoni.

Ufugaji hali kadhalika, tena huu unaweza kuanza hata kwa eneo dogo la kupewa na ndugu, mtaji kidogo na baada ya muda ukawa na mradi mkubwa sana. Kikubwa kwenye ufugaji usichoke kujifunza.

Wito wangu kwa wanaobania wengine furs
Usidhani kuwa wingi wa watu wanaofanya biashara aina moja ndiyo kuua biashara ya hiyo. Muhimu ni jinsi gani unajua mahitaji ya wateja wako, namna unavyotoa huduma(ubunifu) na uaminifu wako.

Sikutaka kuongelea la udalali, unajua kwanini?.........😂
Kiukweli bila kukataa kilimo kinalipa tena sana lakni mkuu je vijana wote wanauwezo wa kupata aridhi..? Je wanakijua kilimo..? Na je masula kama yale ya kipindi fulani wananchi wa kusini walirubumiwa korosho zao sijui mpaka leo wamelipwa au lahayawezi kujirudia?? Tuwashauri waanze na kilimo kwa haya mazao yanayouzika kwa haraka na kwa wakati hususani ya mazao ya vyakula na mboga mboga
 
Mkuu udalali bila ya kuwa mshirikina na mtu wa fitina huwezi kufanya au hata ukifanya mwezi utaisha hata huulizwi na wateja.
Ngoja nikupe mfano mmoja hivi ambao umemtokea jirani yangu ambaye yeye kazi yake ni fundi ujenzi,sasa ikatokea hapo hapo mtaani kwetu kuna nyumba ilikuwa inauzwa basi ingawa jamaa kazi yake ni fundi ujenzi akaona si vibaya afanye udalali kwenye ile nyumba inayouzwa ili apate 10 percent maisha yasonge.
Basi jamaa akaanza kutafuta wateja sehemu mbalimbali basi kwenye pitapita huko akakutana na mama mmoja anatafuta nyumba ya kununua jamaa akaona hii inaweza ikawa bahati nikapiga hela.
Basi yule mama akatoa appointment kuwa nitakuja siku fulani kuiona hiyo nyumba kisha wakapeana mawasiliano,basi kweli ilivyofika ile siku mama akaja kukutana na jamaa akampeleka kumuonesha ile nyumba.
Mama akaingia ndani akaikagua kila mahali kisha akasema sawa nimeiona ngoja nikajipange nikitaka kuja tena nitakufahamisha kisha wakaagana mama akaondoka zake,ikumbukwe yule mama pale ni mgeni hafahamiki ametoka mbali ni kama mtu wa kutoka manzese aende kuulizia nyumba mbezi.
Basi jamaa akawa anasubiri kwa hamu mama aje kununua avute pesa yake ya udalali lakini ikawa siku zinasogea hapigiwi simu na yule mama.
Basi ikapita kama wiki hivi jamaa akawa anapita kwenye ule mtaa inakouzwa ile nyumba akaja kushangaa anawakuta madalali wapo na yuleyule mama kwenye ile ile nyumba wanafanya mauziano na mama kalipia pesa zote siku hiyo hiyo jamaa yangu akaishiwa nguvu.
Jamaa akabaki na maswali mengi je hawa madalali wa hapa mtaani walimpataje huyu mama,walimjulia wapi maana pale ni mgeni kabisa,Na kwa nini siku ya kwanza alikataa kulipia pesa lakini walivyomwita madalali wenyewe hakuchomoa kalipa siku hiyo hiyo tu.
Hivi ndivyo ilivyo kwenye kazi ya udalali ndugu yangu.
Ndio maushirikina yapo kwenye utafutaji saana lakini pia mkuu na juhudi binafsi pia maana ujue kila kazi ina pita pita na mbilinge zake jamaa labda hakujua jinsi ya kumshawishi mama au mama alimuona labda tapeli huwezi jua na mwisho wa yote inatupaswa tuwe na imani tunayoiamini kama mtu utaamini hivyo inabidi na sisi tutumie hiyo hiyo njia maana kila kitu kinaanza na.imani.

Mimi.nasema. Imani+juhudi = matokeo (imani itategemea wewe mwenyewe) lakini nakubali ushirikina upo tena sana hasa kwenye utafutaji wa riziki
 
Na maadili wanayaharibu hawa wavaa nusu uchi tena wanavujisha mpaka mipicha na video zao za ngono ilehali wanajua kuwa jamii yetu haiendani na huo ufska wao. Nashangaa baadhi ya wasanii wanajiita kioo cha jamii hivi ni kwa ufska wao au kwa lipi.?? Japo sio wote ni baadhi tu
Ndio mkuu. Kwenye kila jambo.wapo wema na wabaya kwa kuwa tunasema kila ulipo mkusanyiko au shughuli yoyote basi wapo wenye tabia njema na tabia mbaya. Kikubwa ni sheria za nchi nazo zilinde maadili yetu kwa kuwawekea mipaka hawa wasanii katika kuzitenda kazi zao.

Na wasanii wapewe semina au elimu juu ya kuyalinda maadili yetu. Na usawa uwepo maana kuna baadhi wakipitiwa na rungu la basata wao wanakuja na hoja kuwa mziki wao wakimataifa hivyo hawapaswi kufuata sheria hii ni aibu ya chombo chenye mamlaka ya kusimamia hawa wasanii.

Mfano. Kuna wasanii wanaimba nyimbo za kuikosoa serikali na nyimbo.zao.zilifungiwa mfano nay wa mitego na roma mkatoliki.ilihali hazina uvunjifu wa maadili yetu. Lakini muda huo huo kuna nyimbo za bongo fleva zikichezwa kwenye TV kama upo na wanao.au wazazi wako.lazima mtabadilisha station kwa maana hazifai kutazamwa kimaadili.
 
Kiukweli bila kukataa kilimo kinalipa tena sana lakni mkuu je vijana wote wanauwezo wa kupata aridhi..? Je wanakijua kilimo..? Na je masula kama yale ya kipindi fulani wananchi wa kusini walirubumiwa korosho zao sijui mpaka leo wamelipwa au lahayawezi kujirudia?? Tuwashauri waanze na kilimo kwa haya mazao yanayouzika kwa haraka na kwa wakati hususani ya mazao ya vyakula na mboga mboga
[emoji2960][emoji2960][emoji2960] unaongelea kipindi ya awamu ya 5..?
 
Hiyo hyo. Watu walikopa wakaingiza mitaji shambani afu hali ikawa vile. Pia viongozi waangalie sera zao katika vipindi vyao vyajongozi
 
Hapo kweli. Inakua too much kila ajaye anakuja na ubabe wake. Na lawama hizi za ukosefu wa ajira nina zitupa kwao maana wao ndio wenye dhamana kubwa mkuu. Wanatubana kila sehemu yaani noma sana.
 
Back
Top Bottom