SoC01 Wahitimu wa Vyuo na Maisha ya utafutaji Mtaani

SoC01 Wahitimu wa Vyuo na Maisha ya utafutaji Mtaani

Stories of Change - 2021 Competition

Theb

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2019
Posts
3,927
Reaction score
7,276
Habari zenu wana Jamii Forums, hususani jukwaa hili la "Stories of Change". Ni tumaini langu wote ni wazima.

Andiko hili litaangazia maisha ya vijana wahitimu wa vyuo waliotegemea kuajiriwa na hali imekua tofauti na matarajio yao. Mwanzo, nitaelezea maisha ya mtaani, changamoto zinazo wakabili na vipi watatue hizo changamoto, Pili, nitaelezea fursa zisizohitaji mitaji na zenye kuhitaji mitaji. Tatu, nitaelezea mchango wa serikali na sekta binafsi katika kuwasaidia vijana kupata ajira na kujiajiri. Mwisho, nitamalizia kwa kutoa ushauri wangu katika kuwawezesha vijana wahitimu kujikwamua.

Maisha ya mtaani katika jamii zetu karibia kote yana mfanano kwa asilimia kubwa. Kuanzia ngazi ya familia za wahitimu walio wengi zinafanana kiuchumi, kitamaduni na hata kimalengo. Familia nyingi katika jamii zetu Tanzania tunasoma ili tuajiriwe na sio kujiajiri kwa waliowengi, hali iliyopo kwa sasa imeenda kinyume na malengo na matarijio ya vijana waliokuwa wanasoma na wanaoendelea kusoma mashuleni mpaka vyuoni.

CHANGAMOTO ZINAZO WAKABILI VIJANA WAHITIMU KATIKA UTAFUTAJI.

1. Kushindwa kujiamini na kushindwa kuikubali hali halisi iliyopo. Wengi wameshindwa kujiamini na kufikiria nje ya kitu walichosomea na kuanza kitu kipya ina wawia ngumu.

2. Mazingira yanayo wazunguka wahitimu, jamii ina wapa wakati mgumu kwa kuwahukumu kuwa wamesoma bure, elimu yao haina faida. Hili sio sawa.

3. Ukosefu wa muunganiko baina ya wahitimu na waliotangulia kwenye utafutaji, hapa unakuta wahitimu hawana muunganiko na waliotangulia kwenye utafutaji mitaani.

4. Ukosefu wa mitaji, hususani kwenye biashara au fursa zinazohitaji mitaji.

5. Kukosa uelewa katika utafutaji wenyewe. Kutozijua fursa au kutozitambua biashara na majira yake. Maana kila biashara ina majira yake.

6. Kuchagua kazi. Baadhi ya wahitimu hii changamoto kubwa kwao. Hawako tayari kubeba hata mizigo wanaona aibu au wanaona haiba yao hawastahili kubeba mizigo.

7. Mfumo na mitaala ya elimu nchini haikidhi dhumuni la kujiajiri kwa sababu imejikita katika nadharia zaidi na sio hali halisi katika kujiajiri.

JINSI YA KUPAMBANA NA HIZO CHANGAMOTO:-

1. Wazazi wasaidie watoto wao kuchagua fani zitakazo wawezesha kujiajiri pindi watakapo hitimu vyuoni.

2. Kujikubali, kujitambua na kujichanganya na watafutaji wengine mitaani bila kuwaza au kujutia muda uliopoteza shuleni na vyuoni.

3. Kukubali hali halisi hususani kuwa tayari kwa kazi yoyote bila kuchagua kazi. Mfano baadhi ya wahitimu ni ngumu kufanya kazi kama kuuza mkaa au kununua chupa za plastiki zilizotumika kwa kuhofia taaluma yake au watu watamuonaje.

4. Kuzitambua fursa na kuwa tayari kupambana nazo maana utafutaji mtaani ni ushindani.

5. Kufanya uchunguzi wa biashara unayotaka kwenda kuanzisha, hapa itahitaji kutafiti kwa kile unachotaka kufanya mtaani.

6. Kupunguza matumizi yale yasiyo muhimu. Kuwa na matumizi sahihi ya fedha. Mfano waache unywaji wa pombe, kubet, uvutaji wa sigara au ulevi wowote na anasa zingine zinazo hitaji pesa.

7. Kufanya uchaguzi sahihi wa kile unachoweza kukifanya mtaani na sio kufuata mkumbo. Fanya unachokipenda na unachokiweza

8. Usisahau kutunza kile unachokipata hata kama kidogo. (Bandu bandu humaliza gogo)

FURSA ZINAZOWEZA KUSAIDIA WAHITIMU KATIKA UTAFUTAJI MTAANI

1. Fursa zisizo hitaji mitaji na zisizo hitaji mitaji mikubwa sana. (Hizi kwa ajili ya kuanza kujipatia mitaji kidogo kidogo)

(i) Vibarua viwandani
Kwa wale wahitimu waliopo mijini kuna viwanda, vipo vibarua vya kutwa na wale wanaolipwa kwa wiki viwandani. Kuna kubeba mizigo viwandani kupakia na kupakua mizigo inayoingia na inayotoka na kazi zingine kulingana na kiwanda husika.

(ii) Fursa kwenye standi za mabasi ya abiria
Pia kwenye standi za mabasi kuna baadhi ya fursa zisizohitaji mitaji au zinazohitaji mitaji midogo. Mfano kubeba mizigo ya abiria kuwa wakala wa kukata tiketi na kuunza bidhaa ndogo ndogo kama karanga maji, juisi na matunda.

(iii) Kununua plastiki na kwenda kuziuza
Hapa kuna hii fursa ya kununua plastiki na kwenda kuuza mfano kilo moja unanunua kuanzia 300 hadi 400 na kuuza iliyosagwa ni kuanzia 800 hadi 1200 isiyo sagwa ni 800 bei ya kuuza. Hii ni fursa japo inadharauliwa.

(iv) Kuwa dalali wa mazao shambani au magari ya kusafirisha mizigo au dalali wa nyumba na viwanja
Haihitaji mtaji kwenye kuanza uaminifu wako na kujua chimbo za unachofanya ndio mtaji wako.

(v) Kuanzisha twisheni (tuition) mtaani kwenu
Hii pia saa zingine haihitaji mtaji itahitaji tu utayari wako na uwepo wa wanafunzi wanaosoma na kuitangaza. Japo maeneo mengine hii haina nafasi maana muitiko unakua mdogo hasa vijijini.

(vi) Kubeba mizigo kwenye masoko kupakua na kupakia mazao na bidhaa mbalimbali
Tunaweza kuidharau lakini ni fursa ukibeba mizigo 25 yenye kulipwa 1000 kila mzigo kwa siku una shilingi 25000. Haitaki mtu mwenye aibu na usharobaro.

(v). Kipaji kiwe cha uandishi, uimbaji, ususi, uchoraji, na michezo
Kipaji pia ni fursa kubwa tena isiyo hitaji mtaji ila inahitaji utayari wako kujituma na ubunifu zaidi na uvumilivu uliomithilika.

(vi). Kuwa saidia fundi ujenzi, fundi wa kuchomelea dirisha na mageti, fundi randa nk,

Kusaidia fundi atakulipa kidogo itategemea na kazi iliyopo hapo unajifunza ufundi, kujiandaa kuwa fundi ili ujitegemee. Mfano saidia fundi ujenzi hulipwa sio chini ya 10,000/= kwa siku.

(vii). Kuuza mahindi ya kuchoma na ya kuchemsha.
Hii hususani sehemu zenye mikusanyiko, stand za mabasi, barabarani na kwenye vyombo vya usafiri hususani mabasi.

2. Fursa zinazohitaji mitaji mikubwa au ya kiasi. Nitataja baadhi na ambazo ni rahisi kuzitambua kama ifuatavyo:-

(i). Kununua mazao mashambani na kuleta mjini kwenye masoko
Hapa kuna mahindi, viazi aina zote, mchele mboga mboga kutoka mashambani kuleta mijini. Kikubwa kufanya tathmini vizuri.

(ii). Umachinga wa kuuza vitu mtaani kando ya barabara au kutembeza au kutengeneza banda lako sehemu inayoonekana kwa wateja

(iii). Kilimo, uvuvi na ufugaji

Kilimo kinahitaji uwe na shamba, mbegu, pembejeo za kilimo mbolea na dawa za kupulizia kuua vijidudu hatarishi kwa mazao nacho kilimo kitategemea na aina ya mazao unayolima.

Ufugaji
Mfano wa kuku lazima uwe na mtaji wa kununua kuku, pumba, uduvi na mifupa.

(iv). Udereva boda boda au bajaji
Huu nao utahitaji uwe na mtaji au upate ya mtu. Mfano bado boda hakosi kupata 25000 hadi 30000 kwa siku.

(v). Kuanzisha saloon zote za kunyoa nywele na kusuka nywele
Hapa kwa wanaume na kwa wanawake kuna kunyoa na kusuka hivyo sehemu uliyopo ikiwa na uhitaji hii ni fursa.

(vi). Huduma ya kutuma pesa kwa njia za simu.
Kuanzisha M pesa, airtel money, tigo pesa na halopesa.

(vii). Kuanzisha mgahawa, mama ntilie au ukaangaji wa chipsi na kuchoma mishkaki.

(viii). Kununua na kuuza vyuma chakavu. Hii pia ni fursa inayolipa vizuri ni jambo la kufanya uchunguzi na kuthubutu.

MCHANGO WA SERIKALI PAMOJA NA SEKTA BINAFSI KATIKA KUWASAIDIA WAHITIMU.

1. Kuwapa motisha, semina na muongozo wa namna ya kuanza ujasiriamali.

2. Kuwapatia mikopo yenye riba nafuu au isiyo na riba kabisa.(walemavu wapewe kipaumbele).
Serikali na sekta binafsi kupitia benki na taasisi zingine za kifedha watoe mikopo kwa wahitimu. Pia familia zenye uwezo ziwawezeshe vijana wao waliohitimu.

3. Mazingira wezeshi kwa watafutaji wanaoanza kutafuta mtaani. Hapa kuwaondolea kodi kandamizi. Kuboresha miundo mbinu zaidi mijini na vijijini itasaidia usafirishaji wa bidhaa.

4. Serikali itengeneze mahusiano mazuri na mataifa mengine. Itasaidi kutanua soko la nje kwenye ajira na bidhaa au mazao yatakayo zalishwa nchini.

5. Serikali na sekta binafsi zinapaswa kwa pamoja kuwaamini vijana na kuondoa kigezo cha uzoefu katika kuwapatia kazi/ajira.

6. Serikali na sekta binafsi ziwashirikishe vijana katika juhudi za kuwainua iwe mikopo au semina za kiujasiriamali.

7. Mfumo wa elimu uboreshwe hususani mitaala. Elimu itolewe kwa vitendo na ijikite katika kuwaandaa kujitegemea/kujiajiri.

8. Wazazi, jamii, serikali na mashirika binafsi kwa pamoja watambue na kudhamini karama au vipaji vya wanafunzi toka wakiwa wadogo na kuvisimamia kwa lengo la kujiajiri baadae.

9. Wahitimu wote wenye ulemavu wapatiwe kazi serikalini na mashirika binafsi moja kwa moja. Mfano ajira za mwaka 2021 ualimu na afya serikali haikuwaacha nyuma hili liendelee kila wakati.

10.Kuwe na uwazi katika masuala ya ajira. Iwe za serikali mpaka mashirika binafsi.

11. Ukabila, rushwa, umaeneo na udini viepukwe katika kuwapatia vijana ajira.

12. Waliofikia umri wa kustaafu wasiruhusiwe kuendelea kufanya kazi.

13. Uwepo mgawanyo wa kazi.
Ili mtu mmoja asifanye kazi zaidi ya kituo kimoja.

USHAURI WANGU KWA VIJANA WAHITIMU KATIKA UTAFUTAJI
Ushauri wangu kwa vijana wasaka tonge wahanga wa ajira na vijana woote watafutaji kwa ujumla napenda kutoa ushauri kama ifuatavyo:-

(i). Uvumilivu kwenye hizo fursa tunazoenda kuanzisha maana nako pia tutakutana na changamoto ila tusivunjike moyo na tusikate tamaa mapambano yaendelee.

(ii). Tuzijue hizo fursa na kutambua majira ya hizo fursa itasaidia kutambua muda gani muafaka wa kuanza tusikurupuke kuna kuanguka pia.

(iii). Kama unamtaji usianze na pesa yote ya mtaji maana hauna uhakika 100% kuwa itaenda sawa hivyo kujipanga kwa hilo ni muhimu.

(iv). Kupata ushauri kwa waliofanikiwa ni muhimu itakuongezea maarifa kwa yale usiyo yajua.

(v). Usimuamini kila mtu katika utafutaji wako wengine watakukwamisha. Mfano wanao kopa ni sumu kwako unaeanza utafutaji.

(vi). Tambua hitaji la jamii ikizungukayo. Kama jamii inataka mahindi wapelekee mahindi na sio mchele.

(vii). Ishi vizuri na watu na waheshimu watu kwa imani zao makabila yao na rangi zao. Kuwa na lugha nzuri.

(viii). Zingatia usafi kwenye ofisi yako kuwa na mpangilio mzuri pia toa huduma iliyo bora sio bora huduma.

(ix). Muhimu na la kukumbukwa kila unapopata kidogo kitunze kadri kinavyo kua kiwekeze kitaleta zaidi.

(X). Fanya shughuli halali, kuwa muaminifu, uadilifu ni muhimu na kufuata sheria za nchi yetu katika utafutaji.
 
Upvote 1.6K
Ndio maushirikina yapo kwenye utafutaji saana lakini pia mkuu na juhudi binafsi pia maana ujue kila kazi ina pita pita na mbilinge zake jamaa labda hakujua jinsi ya kumshawishi mama au mama alimuona labda tapeli huwezi jua na mwisho wa yote inatupaswa tuwe na imani tunayoiamini kama mtu utaamini hivyo inabidi na sisi tutumie hiyo hiyo njia maana kila kitu kinaanza na.imani.

Mimi.nasema. Imani+juhudi = matokeo (imani itategemea wewe mwenyewe) lakini nakubali ushirikina upo tena sana hasa kwenye utafutaji wa riziki
Ni kweli mkuu kila mahali kuna ushirikina lakini kuna baadhi ya tasnia ushirikina ni wa lazima na sio option.
Kwa mfano ukijiingiza kwenye kazi ya uchimbaji madini kule kuna ushirikina wanafanya ili kuweza kuyaona hayo madini kiurahisi,bila hivyo utachimba miaka 100 hupati kitu.
 
Hapo kweli. Inakua too much kila ajaye anakuja na ubabe wake. Na lawama hizi za ukosefu wa ajira nina zitupa kwao maana wao ndio wenye dhamana kubwa mkuu. Wanatubana kila sehemu yaani noma sana.
Mnahimizwa mjiajiri ndio mshasahaulika na kutolewa nje ya mfumo wa ajira hivyo. Njooni tukomae mtatukuta ila muache u brothermen na usista du. Huku sio mahala pake
 
Kiukweli bila kukataa kilimo kinalipa tena sana lakni mkuu je vijana wote wanauwezo wa kupata aridhi..? Je wanakijua kilimo..? Na je masula kama yale ya kipindi fulani wananchi wa kusini walirubumiwa korosho zao sijui mpaka leo wamelipwa au lahayawezi kujirudia?? Tuwashauri waanze na kilimo kwa haya mazao yanayouzika kwa haraka na kwa wakati hususani ya mazao ya vyakula na mboga mboga
Nakubaliana na wewe kwa kiwango kikubwa. Kupinga hoja yako ni sawa na kujifananisha na wale wanaowaambia vijana wajiajiri bila kiwapa elimu ya maeneo gani ya ajira, ujuzi & mitaji.

1. Kuna watu wana ardhi nzuri zenye rutuba lakini hawana mitaji(hii ni nguvu kazi ambayo iko under utilized). Na wengine wana mitaji lakini ardhi hawana huku wengine wana elimu & ujuzi wa kilimo/ufugaji bora lakini hawajui pa kuanzia.

Ukitumia combination hii unatengeneza business partnership kama watawekewa mazingira wezeshi.

2. Wapo wakulima wanakosa soko la mazao yao ya kilimo na mifugo, au soko kuwa la chini lisilolipa gharama za uzalishaji.
Sera zetu zinatakiwa kubadilika ili kufanya kilimo kiwe injini ya uchumi wetu. Serikali isipende kuvuna isipopanda.
Zitungwe sheria zinazosimamia uanzishwaji na uendeshaji wa Ushirika badala ya kufanya kimazoea na kusikiliza interests za kisiasa.Hiibitawasaidia kuingia mikataba ya uzalishaji na masoko, kiwafanya kuwa na sauti moja na kuepuka na changamoto zankupanda na kushuka kwa bei.

Mfano.
a) Kama kuna sheria inayowataka wasindikaji wa mahindi kuweka walau 4-10% ya muhogo. Moja kwa moja soko la muhogo litakuwa siyo kikwazo kwa wakulima.
b) Kuchangia 5-10% ya korosho na kuacha zinazobaki ziingie sokoni kwa ushindani na hiyo asilimia itumike mashuleni, vituo vya yatima na maofisini badala ya kupunguza bajetibya chai ofisini. Vivyo hivyo kwa wakulima wa ngano na maharage.
c) Kuanzisha kanda za Kilimo na Mifugo (Agricultural zones) kulingana na tabia za nchi, rutuba, nguvu kazi nk.
Hii itarahisisha allocation of resources ikiwemo utaalamu na moundombinu.

Nadhani nimejibu walau sehemu ya hoja zako.
 
Ni kweli mkuu kila mahali kuna ushirikina lakini kuna baadhi ya tasnia ushirikina ni wa lazima na sio option.
Kwa mfano ukijiingiza kwenye kazi ya uchimbaji madini kule kuna ushirikina wanafanya ili kuweza kuyaona hayo madini kiurahisi,bila hivyo utachimba miaka 100 hupati kitu.
Noma aisee ndio mambo yakuambiana maana njia za utafutaji zina mambo mengi ila tu mtu asije akawadhuru watu kisa hizi imani chonde chonde.
 
Noma aisee ndio mambo yakuambiana maana njia za utafutaji zina mambo mengi ila tu mtu asije akawadhuru watu kisa hizi imani chonde chonde.
Kuna mdau aliwahi kuandika uzi wa kuhusu mgodini,unaambiwa kule ukienda ikatokea umepata jeraha linalovujisha damu watu wanakutoa kafara ili mgodi uteme.
 
Mnahimizwa mjiajiri ndio mshasahaulika na kutolewa nje ya mfumo wa ajira hivyo. Njooni tukomae mtatukuta ila muache u brothermen na usista du. Huku sio mahala pake
Hakika. Hilo tuna lijua kwa wasio lijuahilo muda utawajuza nadhani. Muda ninmwalimu mzuri zaidi.maana anasema ukweli kwa yote yale ambayo mwanadamu anapitia.[emoji1317]
 
Kuna mdau aliwahi kuandika uzi wa kuhusu mgodini,unaambiwa kule ukienda ikatokea umepata jeraha linalovujisha damu watu wanakutoa kafara ili mgodi uteme.
Aisee sasa kule pia na sikia ukipata madini unayaficha wenzio wakiona wanaweza kukuua nk naambiwa wanayamezaga au anajitoboa kwenye mwili na kujishona afiche madini. Sina uhakika maana ni.story za vijiweni sijui zina ukweli..?
 
Weka akilini nakukumbusha tena ubraza men usista du au ubishoo hatuuhitaki mtaani hususani kwa kazi nyingi
 
Nakubaliana na wewe kwa kiwango kikubwa. Kupinga hoja yako ni sawa na kujifananisha na wale wanaowaambia vijana wajiajiri bila kiwapa elimu ya maeneo gani ya ajira, ujuzi & mitaji.

1. Kuna watu wana ardhi nzuri zenye rutuba lakini hawana mitaji(hii ni nguvu kazi ambayo iko under utilized). Na wengine wana mitaji lakini ardhi hawana huku wengine wana elimu & ujuzi wa kilimo/ufugaji bora lakini hawajui pa kuanzia.

Ukitumia combination hii unatengeneza business partnership kama watawekewa mazingira wezeshi.

2. Wapo wakulima wanakosa soko la mazao yao ya kilimo na mifugo, au soko kuwa la chini lisilolipa gharama za uzalishaji.
Sera zetu zinatakiwa kubadilika ili kufanya kilimo kiwe injini ya uchumi wetu. Serikali isipende kuvuna isipopanda.
Zitungwe sheria zinazosimamia uanzishwaji na uendeshaji wa Ushirika badala ya kufanya kimazoea na kusikiliza interests za kisiasa.Hiibitawasaidia kuingia mikataba ya uzalishaji na masoko, kiwafanya kuwa na sauti moja na kuepuka na changamoto zankupanda na kushuka kwa bei.

Mfano.
a) Kama kuna sheria inayowataka wasindikaji wa mahindi kuweka walau 4-10% ya muhogo. Moja kwa moja soko la muhogo litakuwa siyo kikwazo kwa wakulima.
b) Kuchangia 5-10% ya korosho na kuacha zinazobaki ziingie sokoni kwa ushindani na hiyo asilimia itumike mashuleni, vituo vya yatima na maofisini badala ya kupunguza bajetibya chai ofisini. Vivyo hivyo kwa wakulima wa ngano na maharage.
c) Kuanzisha kanda za Kilimo na Mifugo (Agricultural zones) kulingana na tabia za nchi, rutuba, nguvu kazi nk.
Hii itarahisisha allocation of resources ikiwemo utaalamu na moundombinu.

Nadhani nimejibu walau sehemu ya hoja zako.
Tilishuhudia sera zilivyo haribu mauzo ya zao la mbaazi na korosho hiyo ni mifano halisi na pia mahindi yaliadhiriwa na sera zetu kutoka kwa viongozi wetu.

Tulichoma vifaranga vya wakenya ikatuletea tabu sana inaharibu mausiano ya nchi hizi mbili. Mimi naona soko la mazao ya kilimo linaendana na sera zetu katika uhisiano na mataifa jirani na mbali pia.

Hakuna biashara ya kujiuzia mwenyewe.
 
Hakika biashara zinategemea ushirika mwema baina ya majirani zako hata katika ngazi ya mtu mmoja.mmoja huwezi kuwa na mahusiano duni.kwenye jamii ma biashara ikatanuka na kukua zaidi. Never
 
Ni ukweli kabisa ndio iko hivyo.
Kwa mfano bosi mwenye mgodi kuna wale vibarua wanamchimbia mgodi kila siku kwa makubaliano fulani mara nyingi ujira wao ni chakula tu.
Basi unaambiwa hiyo siku ya Bosi kwenda kuchukua madini anakuwa na ulinzi mkali wa silaha hawaaminiani siku hiyo.
Bila silaha wanakugeuka fasta
 
Weka akilini nakukumbusha tena ubraza men usista du au ubishoo hatuuhitaki mtaani hususani kwa kazi nyingi
Haya nimei #NOTE hiyo haswaa na shukran mkuu ubarikiwe sana
 
Ni ukweli kabisa ndio iko hivyo.
Kwa mfano bosi mwenye mgodi kuna wale vibarua wanamchimbia mgodi kila siku kwa makubaliano fulani mara nyingi ujira wao ni chakula tu.
Basi unaambiwa hiyo siku ya Bosi kwenda kuchukua madini anakuwa na ulinzi mkali wa silaha hawaaminiani siku hiyo.
Bila silaha wanakugeuka fasta
Sema nadhani hiyo ni kutoka labda na kufanya baishara hiyo kimagendo kwa maana ikiwa wanauziana kwenye sehemu salama au sehemu zilizoidhinishwa na serikali sidhani kama kuna kugeukana na kama wanalipana kupitia banks nadhani hapo usalama utakuepo. Tatzo wanalipana kienyeji au tuseme wanauziana kimagendo bila kutaka kulipia kodi wanakwepa kodi itakua.
 
Hiyo ni kweli,kule ni porini sasa wanaona usumbufu kwenda hadi mjini mtu anataka auze fasta akale bata zikiisha aingie shimoni tena
 
Hiyo ni kweli,kule ni porini sasa wanaona usumbufu kwenda hadi mjini mtu anataka auze fasta akale bata zikiisha aingie shimoni tena
Hapo sasa suala la.usalama halipo. Kiukweli ndio maana vitisho vingi
 
Um
Hakika biashara zinategemea ushirika mwema baina ya majirani zako hata katika ngazi ya mtu mmoja.mmoja huwezi kuwa na mahusiano duni.kwenye jamii ma biashara ikatanuka na kukua zaidi. Never
Umeonaeeh. Kuna mahala umesema ishi vizur na watu wote na imani zao rangi zao nk. Hii inanafasi yake katika utafutaji popote pale maana mteja ili adumu kwako inategemea na kauli zako zilivyo. Kama kauli ni chafu ataacha kuja. Huduma yako ikiwa bora pia atazidi kuwa mteja wako mara zote akihitaji huduma unayotoa. Ndugu andiko lako lipo vzuri saana na linawajenga vijana kwa kuwapa mwanga na changamoto mbalimbali ila vijana nawaambia tu utafutaji unataka ujasiri na udhubutu na kujitambua, kuwa bahili nk mengi mdau ameyasema tayari
 
Shukran mkuu kwa mchango wako unaowajenga watafutaji kwa kiasi kikubwa karibu tena na tena kila wakati maoni.hoja uzoefu wako ni muhimu hapa kutusaidia wote kwa kupashana moja na mbili katika utafutaji
 
Hiyo ni kweli,kule ni porini sasa wanaona usumbufu kwenda hadi mjini mtu anataka auze fasta akale bata zikiisha aingie shimoni tena
Mkuu shukran sana kwa mchango wako unaohimiza kuwajenga vijana katika utafutaji. Hususani wawe makini ndio point kubwa nimeiona kwako na nyingine nyingi wakipitia mitaa hii watajifunza mengi[emoji1317][emoji1317][emoji1303]
 
Nakubaliana na wewe kwa kiwango kikubwa. Kupinga hoja yako ni sawa na kujifananisha na wale wanaowaambia vijana wajiajiri bila kiwapa elimu ya maeneo gani ya ajira, ujuzi & mitaji.

1. Kuna watu wana ardhi nzuri zenye rutuba lakini hawana mitaji(hii ni nguvu kazi ambayo iko under utilized). Na wengine wana mitaji lakini ardhi hawana huku wengine wana elimu & ujuzi wa kilimo/ufugaji bora lakini hawajui pa kuanzia.

Ukitumia combination hii unatengeneza business partnership kama watawekewa mazingira wezeshi.

2. Wapo wakulima wanakosa soko la mazao yao ya kilimo na mifugo, au soko kuwa la chini lisilolipa gharama za uzalishaji.
Sera zetu zinatakiwa kubadilika ili kufanya kilimo kiwe injini ya uchumi wetu. Serikali isipende kuvuna isipopanda.
Zitungwe sheria zinazosimamia uanzishwaji na uendeshaji wa Ushirika badala ya kufanya kimazoea na kusikiliza interests za kisiasa.Hiibitawasaidia kuingia mikataba ya uzalishaji na masoko, kiwafanya kuwa na sauti moja na kuepuka na changamoto zankupanda na kushuka kwa bei.

Mfano.
a) Kama kuna sheria inayowataka wasindikaji wa mahindi kuweka walau 4-10% ya muhogo. Moja kwa moja soko la muhogo litakuwa siyo kikwazo kwa wakulima.
b) Kuchangia 5-10% ya korosho na kuacha zinazobaki ziingie sokoni kwa ushindani na hiyo asilimia itumike mashuleni, vituo vya yatima na maofisini badala ya kupunguza bajetibya chai ofisini. Vivyo hivyo kwa wakulima wa ngano na maharage.
c) Kuanzisha kanda za Kilimo na Mifugo (Agricultural zones) kulingana na tabia za nchi, rutuba, nguvu kazi nk.
Hii itarahisisha allocation of resources ikiwemo utaalamu na moundombinu.

Nadhani nimejibu walau sehemu ya hoja zako.
Tilishuhudia sera zilivyo haribu mauzo ya zao la mbaazi na korosho hiyo ni mifano halisi na pia mahindi yaliadhiriwa na sera zetu kutoka kwa viongozi wetu.

Tulichoma vifaranga vya wakenya ikatuletea tabu sana inaharibu mausiano ya nchi hizi mbili. Mimi naona soko la mazao ya kilimo linaendana na sera zetu katika uhisiano na mataifa jirani na mbali pia.

Hakuna biashara ya kujiuzia mwenyewe.
Ni ukweli kabisa ndio iko hivyo.
Kwa mfano bosi mwenye mgodi kuna wale vibarua wanamchimbia mgodi kila siku kwa makubaliano fulani mara nyingi ujira wao ni chakula tu.
Basi unaambiwa hiyo siku ya Bosi kwenda kuchukua madini anakuwa na ulinzi mkali wa silaha hawaaminiani siku hiyo.
Bila silaha wanakugeuka fasta
Wakuu shukrani zangu kwenu saana kwa mchango wenu hapa kuhusiana na utafutaki hivyo mzidi kukaribia kila wakati zikiletwa hoja maswali [emoji1317][emoji1317][emoji1303] mbatikiwe wapendwa
 
Back
Top Bottom