Wahitimu wengi wa vyuo vikuu hawana maarifa ya kufanya mabadiliko chanya kwao na kwa jamii

uncle

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2007
Posts
325
Reaction score
184
Hivi kwa huu utaratibu wa vyuo vingi tulivyo navyo hapa nchini tunatarajia hawa wasomi wetu watatutoa kweli. Vyuo vingi vinatoa wahitimu wengi lakini ambao wanakosa sifa za kiusomi kwa sababu nyingi.

Na hizi ndizo nilizobaini kwanza uwezo mdogo wa hao wanachuo wenyewe katika mazingira ya kuchanganua mambo na yote hii imezalishwa na mfumo wetu tulojijengea kati ya wanachuo na walimu hivyo wanachuo kukutaka kuumiza vichwa kwa kuwa mwisho wanauhakika wa kupata matokeo mazuri.

Na hii yote inajengwa na rushwa .Mwanachuo anauhakika wa kupata matokeo mazuri kwa uwezo wa fedha yake ambayo atatoa kwa waalimu. Matokeo makubwa tunazalisha wanasomi wenye uwezo mdogo sana.

Angalizo hii sio kwa vyuo vyote kuna baadhi ya vyuo vinazingatia misingi ya elimu bora na wahitimu wake ni bora lakini baadhi ya vyuo vingi mtindo ndio huo na si vyuo binafsi tu hata vyuo vya serikali mtindo ndio huo.

Asalaam Alekuim wahusika wa Elimu mnakaribishwa kwenye mjadala mapana
 
Ubora wa elim ya juu ni sifa linganifu, ungekua kwanza specific, tulinganishe wahitimu waliohitim miaka ipi,. 1990's vs 2000's au 2010's vs 1980's?
 
Kwa uandishi huu, utakuwa ni mmoja kati ya watoa fedha huko chuoni.
 
Hoja nyingi kuhus wahitimu ni kukompleni tu kwamba hawaajiriwa na hawana impact kwenye jamii. Wenye ukomav wa akili na mawazo wanajua kama hili ni tatizo la jamii. Naona umezungumzia mfumo. Mfumo ndo utalaumiwa hawa gradueta ni wahanga tu
 
Ubora wa elim ya juu ni sifa linganifu, ungekua kwanza specific, tulinganishe wahitimu waliohitim miaka ipi,. 1990's vs 2000's au 2010's vs 1980's?
Ungemchapia na kimombo mkuu hapo anaweza akasema hajaelewa Kiswahili.
 
Hivi unajua faida ya kuwa na Chuo Kikuu katika Jamii.

Kwa ufupi tu sio kugawa vyeti au kujitafutia pesa (ingawa hio ndio motive siku hizi)

Faida ni kufanya reasearch za maana na nchi / jamii kutumia hizo research katika kutengeneza sera na mwisho wa siku kuisaidia Jamii.

Kwahio mpaka tutakapobadilisha mindset ya kuona mtu bora ni mvumbuzi na sio ana vyeti kiasi gani..., ni nini kinahitajika na kifanyiwe research na sio ni nini kitaingiza pesa zaidi..., na makampuni ku-invest katika vyuo kwa kuwapa pesa za kufanya research na sio waalimu kuwaambia wanafunzi fulani alifanya kile au hiki....

Mwisho kabisa tabia ya kuhoji ndio itatutoa hapa mpaka pale sasa kama kila kitu tunaona ni mpango wa Mungu basi tuendelee na tulivyopangiwa...
 
Mkifeli wengi lecturer anakuwa mkombozi, anaongeza vimaksi kwa wote af mambo yanaenda

Na kuna wale lecturers hawapo nondo, hajipi tabu, test na mitihani vitonga watu wanateleza tu ili wasimsumbue

Bado kuna vijiji 😁😁 hata kama mtu hajasoma, wakipiga formation nzuri wote mnatoka

Ila kuna lecturers wanasimamia misingi ndio ile unasikia, kile chuo siendi wanakaza sana
 
Ubora wa elim ya juu ni sifa linganifu, ungekua kwanza specific, tulinganishe wahitimu waliohitim miaka ipi,. 1990's vs 2000's au 2010's vs 1980's?
Ubora wa elimu sijui kama umebadilika unless tungeona inventions na innovations za waliosoma miaka hiyo zaidi ya kuketi kwenye ajira ambazo posts walizipata directly vyuoni

Ila kisichopingwa ni kuwa shule na vyuo ilikuwa vichache kwa hiyo wote waliofika juu ilikuwa ni cream tupu

"selection kama shule za vipaji maalumu"

Sasa hivi mambo yamebadilika, access ya kuingia vyuo vikuu imekuwa rahisi kwa wingi wa vyuo. Wanafunzi wengi zaidi wenye uwezo average au hata hafifu nao wana degree

In this situation, usitegemee cream ya miaka hiyo uilinganishe na average minds za wakati huu ili upime ubora wa elimu. Utakwama
 
Kwanini tulinganishe cream ya miaka hiyo dhidi ya average minds ya miaka hii? Je, miaka hii, huko vyouni hakuna creams kati ya hao wadahiliwa?
 
Uwezekano wa kukutana na cream kwa miaka hiyo ulikuwa ni slope ndio maana kila msomi alionekana yupo vizuri

Uwezekano huo huo kwa miaka hii ni finyu sana ndio maana unaweza kutana na graduates watano wa kawaida ukafungua uzi kwa kudhani graduates wote wapo hivyo

Ila kama ukibahatika kuwa kukutana na cream ya miaka hii hutoona tofauti sana na wale wa miaka hiyo
 
Umechambua vema sana jambo hili, shukrani.
 
Yaani kwenye elimu ndipo ccm inajipigia hatuna sera wala mipango madhubuti.
Unakutana au unatambulishwa kijana huyu katoka chuo ukimuangalia au ukimchukua maelezo unabaki kujiuliza hiki chuo ndo kinazalisha wasomi wa hivi?
Yule mbunge wa Kahama aliwahikuchangia hoja bungeni upande wa elimu kuhusu wanaomaliza chuo HAWANA KITU CHA KUTUSHAURI KUHUSU CHANGAMOTO ZA MAISHA AU KUZITATUA mtoto kamaliza chuo lakini yupo yupo kama kuku wa kizungu. Kiasi kwamba hata kumtuma mjini unahisi atagongwa huko
 
Ubora wa elimu sijui kama umebadilika unless tungeona inventions na innovations za waliosoma miaka hiyo zaidi ya kuketi kwenye ajira ambazo posts walizipata directly vyuoni

Ila kisichopingwa ni kuwa shule na vyuo ilikuwa vichache kwa hiyo wote waliofika juu ilikuwa ni cream tupu

"selection kama shule za vipaji maalumu"

Sasa hivi mambo yamebadilika, access ya kuingia vyuo vikuu imekuwa rahisi kwa wingi wa vyuo. Wanafunzi wengi zaidi wenye uwezo average au hata hafifu nao wana degree

In this situation, usitegemee cream ya miaka hiyo uilinganishe na average minds za wakati huu ili upime ubora wa elimu. Utakwama
Ubora wa elimu una pimwa na kigezo kipi ?

Kwako wewe ulitaka mwanafunzi awe na sifa gani ili kujiunga na elimu ya juu ?

Sasa dunia ipo katika mageuzi ya kisayansi na Teknolojia je ubora wa elimu hauwezi zingatia mageuzi hayo ? Na kutokana na mageuzi hayo kwanini kiwango Cha Elimu ya Sasa kionekane chenye shaka na kuona Cha nyuma kipo bora kwa kuzingatia sayansi na Teknolojia ya wakati huo?
 
Hivi kwa huu utaratibu wa vyuo vingi tulivyo navyo hapa nchini tunatarajia hawa wasomi wetu watatutoa kweli. Vyuo vingi vinatoa wahitimu wengi lakini ambao wanakosa sifa za kiusomi kwa sababu nyingi.

Na hizi ndizo nilizobaini kwanza uwezo mdogo wa hao wanachuo wenyewe katika mazingira ya kuchanganua mambo na yote hii imezalishwa na mfumo wetu tulojijengea kati ya wanachuo na walimu hivyo wanachuo kukutaka kuumiza vichwa kwa kuwa mwisho wanauhakika wa kupata matokeo mazuri.

Na hii yote inajengwa na rushwa .Mwanachuo anauhakika wa kupata matokeo mazuri kwa uwezo wa fedha yake ambayo atatoa kwa waalimu. Matokeo makubwa tunazalisha wanasomi wenye uwezo mdogo sana.

Angalizo hii sio kwa vyuo vyote kuna baadhi ya vyuo vinazingatia misingi ya elimu bora na wahitimu wake ni bora lakini baadhi ya vyuo vingi mtindo ndio huo na si vyuo binafsi tu hata vyuo vya serikali mtindo ndio huo.

Asalaam Alekuim wahusika wa Elimu mnakaribishwa kwenye mjadala mapana
98% Elimu ya Tanzania inazalisha misukule na watumwa.
 
Ubora wa elimu una pimwa na kigezo kipi ?

Kwako wewe ulitaka mwanafunzi awe na sifa gani ili kujiunga na elimu ya juu ?

Sasa dunia ipo katika mageuzi ya kisayansi na Teknolojia je ubora wa elimu hauwezi zingatia mageuzi hayo ? Na kutokana na mageuzi hayo kwanini kiwango Cha Elimu ya Sasa kionekane chenye shaka na kuona Cha nyuma kipo bora kwa kuzingatia sayansi na Teknolojia ya wakati huo?
Wengi hawahoji mfumo wa elimu kwa kuonesha kitu gani specific ni kibaya katika mfumo wa elimu ila wanakosoa kwa kuangalia uwezo wa wahitimu.

Hapo Ndipo nilipoegemea kwa kuonesha vigezo vya sasa na zamani ni tofauti kutokana na mazingira,

zamani walioenda chuo ni wale wenye uwezo wa juu zaidi darasani kwa sababu vyuo havikutosha ila kwa sasa access ni kubwa kwa hiyo average ability ya watahiniwa lazma ishuke

Mfumo wa zamani kwa kiasi kikubwa ndio wa sasa, unamuandaa mtu kuajiriwa kama wakoloni walivyokusudia, haumuandai mtu kuwa innovative zaidi ya kufanya administrative tasks

Mfumo huu haukukosolewa zamani sababu kazi zilikuwepo bwelele na ajira ilikuwa ndio final destination ila kwa sasa wasomi wamekuwa wengi na kiwango cha ajira kilichopo ni kidogo. Ndo maana hizi kelele za elimu zimekuwa nyingi kwa sababu mahitaji ya sasa na elimu inayotolewa hayaendani

Mfumo wa sasa unatakiwa kuwa zaidi ya knowledge based kama siku zote, unatakiwa kuwa skill based maana hizo ndo zinahitajika katika dunia ya sasa inayohitaji watu innovative wanaoweza kutoa solutions mbalimbali na kujiajiri kupitia usomi wao.

Lakini hili haliwezi kufanyika kama lecturers tutawapata kwa kuwachukua fresh from school kwa sababu tu ya academic performance lakini watahiniwa watahitaji zaidi ya good grades, so huyo lecturer ataweza wapa ya ziada

Hapa ndo unaona mfumo wa elimu unatakiwa kugusa kila angle hadi ubora wa waalimu ambao bado wanachaguliwa randomly na huko mavyuoni wengi wanachukuliwa fresh from school. Mambo ni mengi kuyaandika katika paragraph ndogo ndogo lakini nachoamoni Hii cycle haiwezi isha kirahisi kama wakufunzi hawatoguswa 🙏🙏
 
Back
Top Bottom