Wahitimu wengi wa vyuo vikuu hawana maarifa ya kufanya mabadiliko chanya kwao na kwa jamii

Lecturer hajawahi fanya kazi katika field husika anayo-train, baada ya kumaliza tu, akabakishwa shuleni.

Mwanachuo hajawahi fanya field, kipindi chote cha masomo yake, anafanya tu "projects".

Ma-bro kazi zilizowafata chuoni kipindi hicho "waajiri leo", wamekua mwiba, kuhoji ubora na uwezo wa hawa graduates wa sasa.

Nimekuelewa sana katika msingi wa hoja zako katika hili.
 
Mbona nyuzi za kuwaponda graduates zimekuwa nyingi humu ? .
Mna msongo wa mawazo na ugumu wa maisha ?
 
Umetoa summary nzuri sana.. Pamoja mkuu 🙏🙏
 
Ubora wa elimu upi ? , Hao waliograruate miaka ya 60,70,80,90 huko wameleta impact gani kwenye jamii hii ya kitz sio kila siku kukaa na kuandika ujinga hapa kwamba graduates hawana impact hao ambao walikuwa na impact ya kuleta mabadiliko nchi hii ndio wakina nani ,? .
Nchi hii miaka 60 bado inapambana na ujenzi wa vyoo kwa misaada ya USAID
 
Mwanachuo anauhakika wa kupata matokeo mazuri kwa uwezo wa fedha yake ambayo atatoa kwa waalimu. Matokeo makubwa tunazalisha wanasomi wenye uwezo mdogo sana.
Kwa mantiki hiyo “wanauwezo mkubwa wa kuchanganua mambo”; Kama ‘udhaifu’ wa mhadhiri ni ‘vijisenti’ kwanini ujitese!!?


Kuna tofauti kati ya “attitude” na “aptitude”; shida tuliyonayo ni “attitude” sio “aptitude”, darasa la saba ana “aptitude” ndogo sana kulinganisha na “graduate”.

Ila inahitajika “right attitude at the right era and society”, ‘darasa la saba’ mwenye “right attitude" lazima ata m-“outshine” mwanachuo yeyote.

Hata hivyo wasomi wa za amani ndio wametufikisha hapa; vijana hawaokoti na wala hawajatengeneza mifumo yao. Tumefikishwa hapa tulipo na hao “ma-cream” wa enzi hizo:

"form-six-ya-zamani”
”form-ya-zamani”
“darasa-la-saba-la-zamani”
 
Nyie zenu kulalamika
 
Hivi kwa huu utaratibu wa vyuo vingi tulivyo navyo hapa nchini tunatarajia hawa wasomi wetu watatutoa kweli. Vyuo vingi vinatoa wahitimu wengi lakini ambao wanakosa sifa za kiusomi kwa sababu nyingi.
Kuna “werevu” na “weledi”, kwa namna ambavyo wasomi wa zamani wametufikisha hapa utakugundua kuna ‘kambegu-ka-unafiki’ kalipandwa bilashaka bila ya kujua.
Elimu ilizalisha ‘wafuasi wa fikra’ huku utundu vikitafsiriwa kama utovu wa nidhamu.
Walimu kama wapishi wakuu wakisadinisha woga katika akili na mioyo ya wanafunzi. Mifumo ya siasa na falsafa viliithiri elimu ambayo ikazaa wanafunzi wenye fikra fuasi , walilprogramishwa utii na adabu na walihimizwa kusoma kwa bidii ili wapate kazi.

Wasomi ambao walisoma miaka ambayo simu, mpira, ajira, muziki shuleni vilitafsrika kama uhuni na sio ajira!

Jamii imebadilika na ukweli umebadilika mabo yamekuwa tofauti , wasomi wetu wa zamani bado wanahubiri kwenye shule zetu mambo yale yale
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…