Wahubiri jifunzeni kwa Jimmy Lee Swaggart

Wahubiri jifunzeni kwa Jimmy Lee Swaggart

c_alphonce

Member
Joined
Apr 27, 2024
Posts
5
Reaction score
11
Jimmy Lee Swaggart muhibiri kutoka Nchini Marekani na Mjuzi wa muziki. Nilichelewa kumjua Jimmy Swaggart lakini Punde baada ya kumfahamu uelewa wangu juu ya maandiko Matakatifu, juu ya msalaba na Juu ya wokovu uliabadilika kabisa.

Moto wa kuhubiri injili uliwaka ndani yangu. Niliamua kuanza kuhubiri kwenye daladala. Nikiwa Tegeta kibaoni kila Jumapili tulimsikiliza Jimmy Lee nikiwa pamoja na ndugu yangu na rafiki yangu Agustino. Asubuhi tulisikiliza "The message of Cross" kipindi kikiongozwa na Jimmy Swaggart na maprofesa wa Bibilia.

Chumba tulichokaa kilijaa upako na nguvu za Mungu. Jimmy alitulisha neno.

Nilimfuatilia kwa kitambo kirefu; nyimbo hadi mahuburi. "Welcome Holy Spirit" ulikuwa wimbo wangu bora, huku "Fault Worship, Fault Walk, Fault in Battle" ikiwa ni Clip niliyoipenda sana na muda wote.
Jimmy alikuwa mwana uamasho.

Hautaona Mhubiri Jasiri kama Jimmy Swaggart, watu wa kasumba yake si wengi.
Tofauti na sasa Jimmy hakuwa na mahubiri ya sadaka na cake za upako. Ingawa watu waliotoa sadaka na alionekana na mali lakini Jimmy alifundisha na kutualika sote kuzama katika BWANA la damu ya Yesu na kuoshwa humo. Hakusema leta laki saba upone

Hakuuza karama ya Mungu. Jimmy alianguka na kusimama; kwa mwenendo wake kama mwanadamu alikuwa na mapungufu; lakini hakuwahi kupindisha ujumbe wa wokovu wala kuuza karama ya Mungu wala kujikomba kwa wanasiasa. Alisisitiza Kwamba, Yesu Kristo ni Njia, Kweli na Uzima. Na hakuna njia nyingine ya kumuona Mungu isipokuwa YESU KRISTO.

Babu Jimmy Lee alituambia twaweza kuwa weupe tena tukioshwa kwa damu ya mwanakondoo. Alitamka kwa kulia.

Kifo chake akiwa muhibiri aliyeonekana kwenye Luninga muda mrefu zaidi kuliko yoyote niliyemjua kimenihuzunisha mno. Ni kama mwisho wa zama za Kina Reinhard Bonnke na Moses Cerrulo na wengine.

Nilimpenda babu Jimmy alichambua neno na kulifanya rahisi, usipoelewa ujumbe wake ungeelewa machozi ambayo angelia akiwaalika watu katika kumpokea Yesu. Au ungesoma commentary yake yenye wino mwekundu na kuelewa.

Usingeelewa angekukaripia, kama ambavyo maandiko yasemavyo onya na karipia kwa uvumilivu wote.

Tulimpenda, tulipenda vipindi vyake, tuliiga mtindo wake wa kuhubiri. Na tulifarijika na nyimbo zilizopigwa kwa ustadi.

Kipindi ambacho nikiwa sina kazi kilikuwa kifupi sana: ni kipindi ambacho nilisoma vitabu kama evengelization by Fire cha Reinhard Bonnke, One Thing you cannot do in heaven cha Mark Cahill, One Heart Beat A way Cha Mark Cahill pia, na muda wote huo katika chumba chetu kidogo na kilichowaka feni muda wote kwa sababu ya joto la jiji Dar es salaam kiyoyozi chetu kilikuwa ni Son Life Broadcasting Network ambayo ilirusha mahubiri na vipindi Pendwa vya Brother Jimmy Lee Swaggart.

Tulimpenda hata Mjukuu wake Gabriel aliyechapa vyema injili katika kipindi cha vijana Cross Fire.

Ni furaha mbinguni, ni mwaliko kwetu, saa ni saa yetu: mavuno ni mengi na watendakazi ni wachache.
R.I.P babu Jimmy kama ambavyo mimi na Agustino tulimpenda kumuita. Tangu taarifa za kifo chake nimekuwa nikisikiliza wimbo wake wa: "sometimes Hallelujah, sometimes Praise Lord..."


Na, Alphonce Luhamba.
[email protected]
 

Attachments

  • IMG-20250701-WA0023.jpg
    IMG-20250701-WA0023.jpg
    74.8 KB · Views: 34
Ni Morris Cerullo na si Moses Cerullo, by the way mada ni nzuri
 
Back
Top Bottom