Wahubiri wangu wa mfano Tanzania

Hongera sana
 

Jamani Pastor Carlos; Mungu azidi kumtunza na kumtumia Mtumishi wake.
 
🙏🙏🙏
 
Akili za kuchambia kama hizi ndiyo sisiemu wanazitaka ......watu kama nyinyi wenye akili kubwa sana za kuchambi ni tunu ya ccm
Msiseme natukana [emoji19]
 
Kwa Tanzania Mwl Mwakasege, nje ya Tanzania Chris Oyakhilome, na mwamba mmoja toka Ghana anaitwa Pastor Mensa Otabil. Huyu Otabil fanya kutafuta seminar zake YouTube ni [emoji91][emoji91]
Mnapotoshwa
 
1. Mwakasege ni Mwl
2. Dr. Barnabas Mtokambali ni mwl.

Tofautolisha watu kwa huduma zao
 

Mbona wahubiri wengi sana wa hayo makanisa ni vijana vijana tu? Wazee wachache kabisa! Kuna siri gani hapo? Hata matapeli wanaojiita waganga wa kienyeji ni vijana vijana tu tofauti na waganga wa kienyeji wa kale! Siri ni nini au kuna nini nyuma ya pazia?
 
1.Mwakasege, napenda ufundishaji wake

2.Kuhani Mussa Mwacha napenda mahubiri yake angalau wahubiri wa kizazi hiki wanaoweza kukemea dhambi mpaka ukitaka kuitenda ukikumbuka sauti yake unaacha....

NB:nisiulizwe mambo ya kupenda pesa wote wanazipenda!
 
Ondoa hapo Uegbert Angel na Eliona Kimaro. Hao wameshapoteza uhalali wa kusikilizwa. Tamaa ya fedha imewaponza. Hao waweke kwenye list ya GeorDavie, Bushiri na Mwamposa.
 
Ondoa hapo Uegbert Angel na Eliona Kimaro. Hao wameshapoteza uhalali wa kusikilizwa. Tamaa ya fedha imewaponza. Hao waweke kwenye list ya GeorDavie, Bushiri na Mwamposa.
Tamaa ya fedha imewaponzaje?
 
PAST Elingarami Munishi,namuona yuko objective sana.
Huyo jamaa ni real Pastor.
Niliwahi kumsikiliza mara moja kwenye redio nikamuelewa, nikaja kumsikiliza tena mara kadhaa katika mahubiri tofauti tofauti baada ya muda mrefu kupita, bado kitu ni kile kile, anajua Bible na anakufundisha kujua Bible.
 
Duh huyu sijui kwanini nasita sita kukubali maubiri yake.
Kwa sababu ni utapeli, ujanja ujanja na mauza uza. Mwamposa, GearDevi, Mzee wa upako, Kuhani Musa ni matapeli wa kawaida sana kwa mgongo wa Injili.
 
Mkuu, pastor wa wapi huyo? Kanisa lake linaitwaje?
Achana naye huyo.
Anazungumzia tapeli fulani hivi wa kutafuta kick kwa mgongo wa injili hapo Dar, anajiita Pastor Ceasar, akishirikia na mkewe (mmiliki wa kampuni ya vipodozi ya Grace Product), alifahamika zaidi kwa mahubiri yake ya kutetea mashoga, na kanisa lake kufutiwa Usajiri kwa muda.
 
Yupo nabii mmoja mbeya alimpa mtu upako wa kuzaa mtoto akazaa nyoka sijui nani vile watu wa mbeya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…