Uko sahihi sana. Nafkiri mada ilitakiwa kuzitaja kazi za watumishi na si kulinganisha sifa bila vigezo.
Nitatoa mfano, Paulo, mtumwa wa Yesu Kristo anasema yeye ni zaidi ya wale thenashara. Lakini zaidi katika nini? Ni katika kufungwa, katika kufunga, katika dhoruba na katika mapigo. Yaani zaidi katika taabu ya injili. Lakini pia yeye ndiye aliyefanya kazi ya kusambaza injili zaidi kwa mataifa. Lakini pamoja na yote hakuwadharau wenzake, isipokuwa aliwaonya kwa upendo.
Pia, ikumbukwe hizi karama za roho hutolewa na roho kadri apendavyo roho mtakatifu. Mwingine mwalimu, mwinjilisti, utume na unabii.
Neno linatuagiza tuzijaribu kila roho, tupime au tuwatambue watumishi kwa matunda yao na maisha yao kwa ujumla. Na pia tuangalie nani kawaachia joho, yaani tuangalie baba zao wa kiroho.
Paulo aliitwa na Yesu akapewa Philipo, kuna Elisha na Eliya, kuna Musa na Haroun, Joshua na Caleb, kuna Paulo na Timotheo. Watoto wa Kulola na Lazaro unapata TAG / EAGT hapo kwa DSM hapo ma nguli kama Katunzi, Kakobe na wengi ambao wameanzisha huduma na zimesimama imara mpaka sasa.
Hivi ndivyo vipimo vya kibiblia. Ni muhimu kukumbuka kuwa hiyo ni mifano michache. Wapo watumishi wa Mungu wanafanya kazi kubwa hasa vijijini na wanatumika kweli kweli lakini hawaimbwi sana masikioni mwa watu. Ukiwa mfatiliaji wa injili utalielewa hili.