Wahubiri wangu wa mfano Tanzania

Mungu awasimamie watumishi wake Amen.Binafsi tangu nikiwa na Miaka minne Wazazi wangu walikuwa wananunua tapes za Mwl Mwakasege,amekuwa mwalimu mwema sana kwangu Kwa Miaka takribani 30.Mungu amuongezee.
 
Kiongozi wa KIROHO wa Benny Hin nazani ni Catherine kuhlman na huwaga anaenda kutembelea kaburi lake Anasema Ile roho ya Catherine ime incarnate kwake

Sasa sijui hii nini kama sio uchawi
 
Hivi Mitimingi ni nabii,nayakubali sana mafundisho yake ya ndoa na mahusiano.
 
kuna siku nilienda semina ya Mwakasege, niliondoka katikati ya mahubiri aliposema Cain na Abel ni mapacha(tena akarudia mara mbili kusema haya (NI MAPACHA SOMENI BIBLIA YENU VIZURI,,halafu katikati ya mahubiri kuna lugha anaongea ambazo hazieleweki,,ndio wanaita kunena kwa lugha
 
Yeyote unayeona ametumiwa vizuri na Roho Mtakatifu kuhubiri injili, nashauri usimpe sifa yeye wala kumshabikia kama ulivyopanga orodha. Mpe utukufu, sifa, heshima na shukrani Roho Mtakatifu anayewatumia. Nachelea kusema unaweza kujikuta unawaabudu pasipo kujitambua!

Aidha, hakuna awezaye neno lolote pasipo Yesu Kristo aliyetukomboa na kutununua kwa damu yake ya thamani. Mtukuze Yeye daima, si kiumbe au chombo anachokitumia. Ni ushauri tu!
 
Mchungaji Joshua Maponga, ukiskiza sentensi 2 tu huwezi acha kumskiza.

Pan africanist, and true son of Africa & bible hero
 
Je? Kuna watumishi wa mungu ukifka tu wanataja matatizo yako before ujawaelezea? Hii imekaaje wataalam??

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
Kwanza rekebisha andika Mungu kwa kuanza na M kubwa.

Najibu swali lako, ndio wapo watumishi wa namna hiyo. Ila kama alivyosema mdau hapo juu hutakiwi kubebwa na hii ya kutajiwa majina ya baba yako sjui watoto mara uambiwe una jirani anaitwa Mbanga nk

Ukisoma Biblia imeeleza kila kitu kuhusu watumishi feki na wasio feki, na kila mtumishi amepewa sifa zake uamuzi ni wako yupi umfuate yupi usimfuate. Nasikitika wengi wanatekwa na hawa wanaopiga ramli za kutajiwa majina... Utasikia mtumishi anamuuliza mshirika....

Mtumishi: unaitwa John ennh

Mshirika: Ndio baba mchungaji/Nabii

Mtumishi: Mke wako wa kwanza uliachana naye, huyu wa sasa umekuja nae kanisani na anaitwa Kivuli..

Mshirika: Amen mtumishi nimekuja nae

Mtumishi: Mimi na wewe tulishawahi kuonana kabla ya leo?

Mshirika: Hapana leo ndio mara ya kwanza..

Sehemu hii ndiyo watumishi wengi hujizolea kondoo wasiojielewa kwa kutajiwa taarifa zake ambazo anaamini hakuna mwingine anaezijua basi inakuwa ithibati ya kuamini maelezo yote anayopewa.

Tusome neno la Mungu bila kuchoka, tumuombe Mungu bila kukoma, yeye ni yule yule jana leo na hata milele. Mwisho tuwe makini sana na hawa wahubiri wa mafuta dunia iko hovyo kuliko, nafsi nyingi zinatekwa kwenye uharibifu.
 
Yule anahubiri au anasuta na kufanya comedy. Anahubiri saa Zima bila kuweka hata kifungu kimoja cha Biblia zaidi ya kufanya utani na kuchomekea maneno ya mtaani. Mtu mwenye akili timamu hawezi kaa na kumsikiloza mgogo hata mara 1.
We jamaa unaelewa sana, nikiperuzi mtandaoni nikiona clip ya Mgogo huwa nairuka [emoji1787][emoji1787]

Hafanyi rejea yeyote toka kwenye Bible, yule mwamba komedi balaa, wanawake ndio wanapenda kumsikiliza fuatilia utagundua.
 
[emoji120]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…