Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
🙏🙏🙏Kimataifa nianze na Bonke, Cerullo, Janks, Joyce Mayor, Hinn. Tanzania nianze na Mabondo, Kulola, Kakobe, Mwakasege, kuna muhubiri wa kimataifa raia wa Dermark aishiye Arusha Egon Falk. Kuna wachungaji wa mikoani/kikanda nao wako vizuri kama John Mafyimbo, Brown Mwakipesile, Mwizarubi, Mahene, Gamanywa, Katunzi, Mulenga, Jecha, hao mapastor ukisikiliza injili wanayoihubiri utaokoka tu. Orodha ni ndefu kwa leo niishie hapa
Ndiyo! Ni mume na mke.Niulize tu, Keneth Copeland na Gloria Copeland ni wahubiri wakubwa, je wana uhusiano gani wa kifamilia? Je ni mume na mke au ni kaka na dada?
🙏🙏🙏Tusimchukulea poa Mwamposa, ana kitabu kinaitwa nguvu ya kuona, ni kitabu chenye mafundisho ya imani
🙏🙏🙏Katika orodha tunayotoa tukumbuke wahubiri wana huduma tofauti. Wengine ni wachungaji, wainjilisti na walimu bila kusahau mitume na manabii. Kila mmoa amebobea kwenye eneo lake
sawa mkuu kwa wa nje kaa na haggin basi hao wengine chengaWa Kimataifa/ toka Mataifa mengine ni hawa:
1. Kenneth Hagin
2. Kenneth Copeland
3. Smith Wigglesworth
4. Dr. David Oyedepo
5. Pastor Chris Oyakilome
6. Uebert Angel
7. T. L. Osborn
8. Gloria Copeland
9. F. F. Bosworth
10. Charles Capps
11. Norvel Hayes
12. Andrew Wommack
13. E. W. Kenyon
14. Jerry Savelle
Kwa Tanzania, ni hawa wafuatao:
1. Aaron B. C. Mabondo
Kwa sasa ni marehemu. Alikuwa katibu Mkuu wa Kanisa la Pentekoste Tanzania. Nilimfahamu kwa mara ya kwanza mwaka 2003, mwezi June, nilipohudhuria Camp iliyoandaliwa na NEW LIFE BAND ya jijini Arusha na kufanyikia katika shule ya Sekondari Moshi mkoani Kilimanjaro.
Nilibarikiwa na masomo yake ya Imani na jinsi alivyokuwa akiishi Imani yake. Baada ya kuaga dunia, nilifanikiwa kukisoma kitabu cha Historia ya maisha yake. Nimevutiwa na misimamo yake ya kiimani, kiasi cha kutokukubali kuwekewa mipaka ya kidhehebu.
Inasemekana, kupitia mafundisho yake, alichochea "uamsho" kwenye Makanisa yasiyokuwa ya Kipentekoste, kama Moravian, Anglikana, n.k. Huwa ninabarikiwa sana na wahubiri wanaolisambaza Neno la Mungu bila kuzingatia mipaka ya madhehebu yao. Msimamo wa Mabondo ulikuwa kwamba hakutumwa kuyahubiria madhehebu, bali kila kiumbe. Kwa hiyo alikuwa yupo tayari kuhubiri popote, bila kujali dhehebu litakalomwalika.
2. Dr. Mosses Kulola
Aliifanya huduma yake kwa uaminifu mkubwa sana. Hakuwa akitafuta maslahi yake binafsi. Alikuwa tayari kuhubiri hata katika mazingira magumu. Alikuwa ni mtu wa lengo moja tu maishani mwake, KUHUBIRI INJILI.
3. Mwl Christopher Mwakasege
Tokea aanze huduma, amekuwa "focused" kwenye hiyo huduma. Angeweza kufanya shughuli zingine za kiuchumi, hasa ukizingatia kuwa ni msomi wa Uchumi, lakini kwa kuwa ameukubali wito wa KULIFUNDISHA Neno la Mungu, ameamua kuachana na vingine vyote na kubaki na kimoja tu, huduma aliyoitiwa.
Kingine ninachompendea, ni tabia yake ya kutokuendekeza "udini". Timu ya huduma yake inadhihirisha hilo. Ina wahudumu kutoka madhehebu mablimbali yaliyopo Tanzania.
Kwa ufahamu wangu, yeye ni miongoni mwa wahubiri wachache walioweza kukivuka kiunzi cha udhehebu nchini Tanzania.
4. Mch. Elyona Kimaro
Japo sijamfuatilia sana, lakini kwa vipindi vyake vichache nilivyovitazama kupitia Upendo TV, amenibariki kwa kweli. Ni kiongozi mzuri. Kiongozi huona hitaji na kutafuta kulitimiza kabla ya kuambiwa. Ndivyo alivyofanya Kimaro kwenye Kanisa analoliongoza, ametafuta jinsi ya kukata kiu ya kiroho ya watu wake.
5. Dr. Augustine Mpemba
Ni Mtanzania anayeishi Marekani. Alikuwa Askofu wa Kanisa la TFE Jijini Mwanza, lakini sijui kama angali kiongozi wa hilo Kanisa kwa sasa. Nilishakisoma kitabu chake kimoja, na nilishasikiliza mtandaoni mafundisho yake kadhaa. Ana uelewa mpana wa mambo ya kiroho na kijamii. Madhalani, yupo vizuri sana kwenye masomo ya IMANI, masomo ambayo ni adimu sana katika Makanisa mengi ya Tanzania.
6. Prosper Ntepa
Sijawahi kusikiliza mahubiri yake, lakini nimevisoma vitabu kadhaa alivyoviandika. Kuna kimoja kinachohusiana na uponyaji, nilikipenda sana. Ni Mwalimu mzuri sana kwenye somo la Imani. Na kama ilivyo kwa tabia ya walimu wengi, yeye naye ni msomaji mzuri sana wa Vitabu.
7. Pastor Famous
Huyu ni Mchungaji wa Winners Chapel Jijini Mwanza. Nafikiri ni Mnigeria, alikuwa akiliongoza Kanisa la Winners Chapel lililopo Pasiansi jijini Mwanza. Sijui kama bado yupo pale au la.
8. Dr. Barnaba Mtokambali
Ni Askofu Mkuu wa TAG na pia ni Rais wa Makanisa ya Assemblies barani Afrika. Kama hiyo haitoshi, ni Mwenyekiti wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania.
Ana maono ya kiuongozi. Si bure CPCT wamempa Uenyekiti.
NB. Naweza nisiwe nakubaliana na kila kitu kwa baadhi ya hao watumishi wa Mungu, lakini kwa kuamua kuwataja kama miongoni mwa wahubiri wangu wa mfano, ni kwa sababu kuna maeneo wamenibariki.
Na, katika wahubiri woote, "my favourite" ni KENNETH HAGIN. Japo alishaaga dunia tokea mwaka 2003, vitabu vyake vimenisaidia sana , hasa katika eneo la IMANI.
Hatujawahi kukutana ana kwa ana, lakini kupitia vitabu vyake, amekuwa kama baba kwangu. Nimeshavisoma zaidi ya vitabu vyake hamsini. Nimeshavisoma karibia vitabu vyote alivyoviandika. Ni vichache sana ndiyo bado.
Tuwekee na wewe watumishi au viongozi wa dini unaowachukulia kama watumishi wa Mungu au viongozi wa mfano kwako.
Karibu!!!
Mwampo sio tapeli watu wanapona wenye matatizo wwngi wamefunguliwa
Mzee Kulola yule mpaka mapepo yalikua yanamtambua kua ni mtu wa Mungu,waulize wachawo nguli watakwambia kuhusu marehemu kulola...amemaliza kazi yake kwa ushindi mkubwa.Mkuu, sikuelewi kabisa unachomaanisha kwa kusema kuwa Mwalimu wetu hajawaji kuexperince wokovu wa kweli. Ni Mwalimu yupi huyo? Mwakasege?
Mimi binafsi, Mwalimu wangu ni Roho Mtakatifu, na Mwakasege ni Mtumishi wa MUNGU anayefundisha Neno la Mungu lililovuviwa na Roho Mtakatifu.
Kuhusu kuexperince wokovu, sijajua umemaanisha nini hasa.
Labda nikuulize kama hutojali! Unamfahamu Marehemu Ask. Mosses Kulola? Na Aaron Mabondo je? Hao watumishi - Kulola na Mabondo waliexperience wokovu wa kweli?
Kua mentor wa mtumishi fulani sio kigezo,..watu hubadirika,anaweza anza vizuri akamaliza vibaya,..mfano mzee kulola amezaa watumishi wengi kiroho lkn wengine wamesha haribika,hawatembei kwenye ile misingi ya kwanza,kwa hiyo,mtumishi inabidi kila wakati awe makini na Roho Mtakatifu ili asitoke kwenye mstari.Mkuu, nilieleza kuwa hao niliowaweka ni ambao kwa namna Moja ama nyingine nimebarikiwa na huduma zao.
Nilivisoma vitabu kadhaa vya Uebert Angel, japo kuna baadhi ya mambo ambayo mwanzoni vilinitia mashaka kuhusu huduma yake, niliamua kupuuzia baada ya kubaini kuwa mentor wake ni Pastor Chris.
Pastor Chris naye nilikuwa nina mashaka naye, lakini mashaka yaliisha nilipogundua kuwa rafiki yake wa karibu ni Benny Hinn.
Hata Benny Hinn, nilikuja kumkubali vilivyo baada ya kugundua ukaribu alikokuwa nao na Reinhard Bonnke.
Unauona mnyororo ulivyo? Bonnke, Benny Hinn, Pastor Chris, Uebert Angel.
Lakini sivyo tu, huwa nina "falsafa" yangu kwa habari ya watumishi. Kwamba, katika mafundisho yao, nitatofautisha chuya na wali. Nikikutana na chuya, nitatema lakini wali nitaumeza.
"Sibugii" kila kitu kisemwacho na mtumishi. Nikijiridhisha kuwa akisemacho kipo nje ya Biblia, nakiweka kando nasubiria kingine.
Umetema madini sana.Mkuu sio kwamba nahukumu. Tofautisha hukumu na maoni. Anayeweza kuhukumu ni Mungu tu. Hukumu maana yake kutoa maamuzi ya mwisho kwamba huyu anaenda motoni au mbinguni. Ndio maana hiyo kazi ya kuhukumu ni ya Mungu pekee sio mwanadamu.
Mwanadamu akisema Fulani haendi mbinguni, hiyo ni dhambi na atahukumiwa kwa kuingilia kazi ya Mungu maana yeye Hana mamlaka hayo. Mungu pekee ndio mwenye kuhukumu.
Mimi nimetoa maoni yangu ya kwamba usimhusishe Bonke na matapeli haikumaanisha kwamba Nina wahukumu Bali natoa maoni kwa jinsi ninavyowafahamu. Lazima ujue Benny Hinn na Pastor Chris waliwahi kuachana na wake zao kwa tuhuma mbalimbali, mke wa pastor Chris alidai mumewe ana mchepuko. Ndio maana nikawaita matapeli.
Mchungaji asiyeweza kuitunza ndoa yake utamwitaje?. Unanifundisha kuhusu ndoa wakati wewe umeshindwa kulinda ndoa yako?. Kwangu Mimi Bonke hafananii kuwa na hao watu. Halafu kuombea sio Jambo baya, unaweza kumwombea yeyote. Bonke amewahi kumwombea mtu aliyempinga kuhusu wokovu, sembuse kumuombea huyo Benny Hinn.
Bonke level zake ni akina Cerrullo, Billy Graham, Osborn, Don Double etc.