Wahubiri wangu wa mfano Tanzania

🙏🙏🙏
 
Katika orodha tunayotoa tukumbuke wahubiri wana huduma tofauti. Wengine ni wachungaji, wainjilisti na walimu bila kusahau mitume na manabii. Kila mmoa amebobea kwenye eneo lake
 
Katika orodha tunayotoa tukumbuke wahubiri wana huduma tofauti. Wengine ni wachungaji, wainjilisti na walimu bila kusahau mitume na manabii. Kila mmoa amebobea kwenye eneo lake
🙏🙏🙏
 
sawa mk
sawa mkuu kwa wa nje kaa na haggin basi hao wengine chenga
 
Mwampo sio tapeli watu wanapona wenye matatizo wwngi wamefunguliwa



Mshauri bei ya maji auze ya kawaida na sio buku kwa lita moja.
Walau auze kwa jero kwa lita moja ili watu wasielemewe maana wengi wa wanaenda pale wamechoka sana kiuchumi .
 
Mwakasege ni Mtumishi wa Mungu haswa,nampenda sababu semina zake hazina udhehebu mule ndani mpka waislamu unawakuta.

ila nikienda semina ya mwakasege ndugu zangu NASINZIA,mahuburi ya vile binafsi siyawezi siwi Active napenda mahubiri ya nakshi nakshi ku refresh ubongo.

Kina Kimaro
Kina Mastai
Kina Mtokambali (TAG pastors wote)

Sina mtumishi mmoja wala favourite mimi yeyote mtoa Mawe nayapokea nayafanyia kazi.
 
Kwangu mm nikisikiliza mahubiri na mafundisho ya KIROHO toka wa Mzee wa UPAKO Anthony Lusekelo hakika NABARIKIWA SANA.

MAHUBIRI NA MAFUNDISHO YAKE, yanaujazo wa Kiroho na upekee. Kuna mafundisho ambayo anayatoa huku msikilizaji ukiduwaa na kushangaa katoa wapi hili huku Roho yako IKIKUBALI ni mafundisho ya ROHO MTAKATIFU.

Ingekuwa vyema sana, Mch ANTHONY LUSEKELO kama Angemlea au kumuweka kariba mch EMMANUEL MASANJA ( COMEDIAN) huyu kijana anakuja vzr sana.

Hakika nikimsikiliza napata baraka sana. Anavitu vya Kiroho na anaviwakilisha vyema kwa wasikilizaji wake. Ushauri namuongezea tu! APENDE kuwatembelea viongozi wote wa KIDINI wazidi KUMUIMARISHA.
 
Mzee Kulola yule mpaka mapepo yalikua yanamtambua kua ni mtu wa Mungu,waulize wachawo nguli watakwambia kuhusu marehemu kulola...amemaliza kazi yake kwa ushindi mkubwa.
 
Kua mentor wa mtumishi fulani sio kigezo,..watu hubadirika,anaweza anza vizuri akamaliza vibaya,..mfano mzee kulola amezaa watumishi wengi kiroho lkn wengine wamesha haribika,hawatembei kwenye ile misingi ya kwanza,kwa hiyo,mtumishi inabidi kila wakati awe makini na Roho Mtakatifu ili asitoke kwenye mstari.
 
Umetema madini sana.
 
Binafsi watumishi wengi wa kiroho nawakubali,hasa wenye misimamo thabiti ya kiroho...lkn mtumishi wangu pendwa ni MAREHEMU DR MOSES KULOLA..huyu mtumishi hua nasikiliza sana injili yake...pia mwenye mikanda ya mahubiri ya huyu mzee niko tayari kuinunua tuwasiliane,natunza kumbukumbu yaweze nisaidia.
 
Siku hizi wengi ni maslahi kwanza !

Ndiyo maana wanahubiri mafanikio kwanza badala ya utaua na kwa Habari ya kutafuta ufalme wa Mungu kwanza.

Yesu kama mfano hakuwawahi kuonesha kujali maslahi ya fedha na mali.

Siku hizi sadaka mtatoa na michango mbali na sadaka mtatoa.

Mimi huwa najiuliza Kwani. Kazi ya zile sadaka zitolewazo ni nini?

Kwanini tena michango?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…