DOKEZO Wahudumu wa afya ya jamii(CWH) wilaya ya Ruangwa hawajapewa vifaa, hawapewi stahiki zao na kazi wanafanya

DOKEZO Wahudumu wa afya ya jamii(CWH) wilaya ya Ruangwa hawajapewa vifaa, hawapewi stahiki zao na kazi wanafanya

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Joined
Oct 1, 2022
Posts
7
Reaction score
4
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliandaa wahudumu wa afya ya jamii kwa kuwagharamia mafunzo yaani Ada, malazi chuoni na chakula na kila kitu kuhusu mafunzo hayo.

Baada ya kumaliza wahitimu wanatakiwa kupewa vifaa vya kufanyia kazi kama baiskeli, vishkwambi na vifaa vingine vinavyohitajika ili kazi ifanyike.

Huku Ruangwa wahitimu hao wa Intake ya pili wamemaliza mwezi wa 9 mwaka 2025, na mwezi wa 10 wakasaini mkataba wa kuanza kazi rasmi bila ya vifaa, lakini kwa uvumilivu walifanya kazi katika mazingira hayo hayo.

Cha ajabu hadi leo vifaa hakuna, na hata posho kulingana na mkataba HAWAJAPEWA. Na sasa umefika muda wa kurenew mkataba.

So, nataka kujua je serikali imeachana na mpango huu au shida hiko wapi mana inakokwenda watu wataachanao na kulazima kuwa train watu wengine
 
Back
Top Bottom