Wahudumu wa hotel, Bar na migahawa Tanzania wana shida gani?


The Naked Truth.
 
Customer Caring ni BIG ZERO kwa wahudumu wa restaurants Tanzania....wa Hotels hasa za kitalii wana nafuu kubwa kwasababu wanasomea though hatujawafikia majirani wa Kenya
Halafu kingine: sehemu nyingi za Bar au hotel wanafanya complication zisizo na umuhimu. eg hakuna sababu ya ''kunawishwa mikono'' wakati wanaweza kutengeneza sehemu ya kunawia.
 
Kipi kianze?
Huduma nzuri au tip bila kujali ubora wa huduma kwa minajali watabadilika na kuwa bora baadaye wakiwa wanapata tips??
 
Halafu kingine: sehemu nyingi za Bar au hotel wanafanya complication zisizo na umuhimu. eg hakuna sababu ya ''kunawishwa mikono'' wakati wanaweza kutengeneza sehemu ya kunawia.
Hii nayo muhimu sana, ni usafi zaidi kunawa mikono bombani kuliko kwenye vibobo na mabeseni.
 
Sehemu ambayo ina wahudumu wanajielewa ni Samaki Samaki na nduguye Wavuvi Kempu ukitoa 4/5* hotels. Wahudumu wa Carlito ni well-trained halafu pisi zimenyooka. Wenye bar mjifunze kwa Samaki Samaki.
Kama unapenda kitimoto enda pale sinza lego utafurahia huduma maana unakimbiliwa na wahudumu
 
Sehemu ambayo ina wahudumu wanajielewa ni Samaki Samaki na nduguye Wavuvi Kempu ukitoa 4/5* hotels. Wahudumu wa Carlito ni well-trained halafu pisi zimenyooka. Wenye bar mjifunze kwa Samaki Samaki.
Sio kila mtu anapenda kwenda sehemu zenye kelele, pombe na vibe. Watu wengine wanataka kukaa tu mahali jioni au weekend baada ya kazi wale au wanywe kahawa kwa utulivu huku wakipata huduma bora, sasa badala yake unakuta mnaanza kufokeana na kusukumana tena na wahudumu.
 
Nefaland, Royal Village,Rombo Hotel, Peacock Hotel,Silver Paradise Hotel naona wana huduma nzuri wahudumu wapo active sana na customers care nzuri
 
Umehudumiwa vibaya hiyo tip utatoaje? Yaani umekereka Hadi chenji Yako unataka uichae tu maana umeisubiri kuliko muda ule ulio tumia kula!

Unaenda kwenye mgahawa Hadi una uliza wahudumu wako wapi? Ndo anakuja hasalimii Wala kuonyesha kuchangamka tembea yake tu kana kwamba anaulaani ujio wako hapo!

Daah Kuna shida kubwa Sana Kwa wahudumu wa mbogo.

Nimewahi enda Uganda kwenye lile kanisa la RC nadhani Namgongo kama sijakosea wahudumu walikuwa Smart hatari japo kiswahili changamoto kwao
 
Mkuu Tanzania ni watoa huduma zote sekta zote wako. Hospitalini ndiyo kabisaa. Polisi. Mahakamani. Ofisi zote za serikali. Makondakta wa magari. Mpaka viongozi wa serikali. Ni utamaduni tumeujenga.
Nilitaka kusema hili. Unaweza ingia ofisi ya serikali kupeleka pesa ukadhani wewe ndo umefata pesa hivyo wanakukwepa. Watu wamevimba, mabega juu, wapo serious na simu au laptop.
 
Sahihi, unafika mahali mhudumu anakuja baada ya dakika tano, unamuuliza chakula kitachukua muda gani kuwa tayari anakuambia nusu saa tu halafu kinakuja baada ya saa na nusu, umemaliza kula humuoni akanawishe na akupe bill yako, ukimpata akishachukua pesa yako unaanza tena kumtafuta akurudishie chenji yako sasa unampa tip ya nini!
 
Tatizo ni Bad Customer care!
Customer care ni tatizo kubwa Sana kwa Watu weusi wengi. Na baadhi ya Wahudumu Wana lugha chafu sana kwa wateja. Kwenye nchi moja fulani niliyowahi kuzuru, nimeona baadhi ya Wamiliki wa Migahawa (Restaurant) kubwa kubwa wameanza kutumia 'Maroboti' katika kutoa huduma kwa Wateja ili kuepukana na hili tatizo la bad customer care linalofanywa na Wahudumu Binadamu.
 
Hapo kwenye chenji sasa wengi wanapenda kuminya,yaani wanakusikilizia
Ngoja niingie hapa nikapige kitu cha kituruki

Ova
 

Attachments

  • 20240727_101424.jpg
    2.3 MB · Views: 1
Sehemu ambayo ina wahudumu wanajielewa ni Samaki Samaki na nduguye Wavuvi Kempu ukitoa 4/5* hotels. Wahudumu wa Carlito ni well-trained halafu pisi zimenyooka. Wenye bar mjifunze kwa Samaki Samaki.
Na salt pia

Ova
 
Sana sana kama una roho ndogo una mtu kama tu
 
Waarabu hawana ustaarabu huu wa kuomba omba? Huenda tumeathiriwa nao kutoka huko kwa wajomba zako,

Ninafahamu wazungu hawana huu ustaarabu kwa hiyo siwezi kuwahusianisha wakoloni na huo "ustaarabu" wa kipuuzi.
Nini maana ya neno "ustaarabu'? Unaelewa au unakurupuka tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…