TANMO
JF-Expert Member
- Apr 12, 2008
- 11,763
- 11,873
Nilitaka kujisajili kwenye Huduma ya TIGO PESA cha kushangaza nikaambiwa eti nilishajisajili hivyo nikalazimika kwenda kwenye Ofisi za Tigo pale Mlimani city kutaka kufahamu ukweli wa hili suala pamoja na kuomba kupatiwa namba ya siri.
Yapo mazuri niliyokutana nayo pale na kwa haya Tigo wanastahili pongezi:
....Utaratibu mzuri wa kutumia namba ili kuepusha migogoro ya foleni
.... Mhudumu wa pale mlangoni anafanya kazi yake kwa ufasaha na hababaishi
.... Mlinzi pia ana ushirikiano wa kutosha kwa wateja
Sasa tatizo linakuja pale unapokwenda kwa wale akina dada watoa huduma......
....Hawako friendly hata kidogo, ukienda pale wanakuona kama unawasumbua
....wakati mwingine wanaacha kumsikiliza mteja wanazungumza kwenye simu
....kuna mmoja alipigiwa simu huyo akanyanyuka kwenda kupokea na aliporudi bila hata kumwomba samahani mteja anamuuliza "una shida gani?"
....wana tabia ya kupiga stori wenyewe kwa wenyewe huku wamemweka mteja pending
....mara wanatumiana sijui vitu gani online wanaambiana "iicheki hiyo" huku mteja ukisubiri
....Wana dharau sana wateja na wanatoa majibu ya hovyo hovyo
....wana tabia ya kutoa majibu ambayo hayaridhishi na siyo ya kitaalamu, ukiwauliza maswali zaidi wanakuonesha dhahiri kukerwa na maswali yako, mara washike simu mradi tu kukufanya ukate tamaa uondoke.
....Cha kushangaza wakati mwingine wanatumia hata kiingereza, ukiwauliza swali kwa lugha hiyo hiyo, wanabadilisha wanatumia kiswahili
Jana ilikuwa mara yangu ya Tatu kwenda pale ili nisaidiwe kupata suluhu ya Tatizo hilo hilo, cha kushangaza waliniambia kuwa nimesajiliwa kwenye hiyo huduma ingawa hawakuniambia nilisajiliwa lini na katika kituo gani, kwa maelezo kuwa ni long process mpaka wanipe majibu yote hayo (nikaridhika). Kila ninapoomba kupatiwa namba ya siri ninaambiwa kuwa nitatumiwa ndani ya masaa 24 kwa sms, bado naisubiri hapa!
TIGO licha ya mazuri yenu kwetu wateja, pamoja na matatizo mbalimbali mliyo nayo pia mnaangushwa na watu wa jinsi hii, manake mteja ninakwenda kwenye Ofisi zenu kutatuliwa tatizo lakini badala ya ufumbuzi wa tatizo langu ninaondoka pale nimekereka kwa sababu ya majibu ya dharau ya wahudumu wenu.
Mapendo.
TANMO.