A
Anonymous
Guest
Sisi Wahudumu tuliofanya kazi ya usajili wa majengo kwenye mfumo wa kodi katika Wilaya ya Muleba, Mkoa wa Kagera mwezi Juni mwaka 2025 kwa kushirikiana na mamlaka husika katika zoezi la usajili wa majengo.
Hata hivyo, mpaka sasa hatujalipwa malipo yoyote kwa kazi tuliyoifanya, licha ya kukamilisha majukumu tuliyopewa. Baada ya kumaliza zoezi hilo, tuliombwa kuwasilisha majina yetu pamoja na idadi ya nyumba tulizosajili kwa ajili ya taratibu za malipo, lakini hadi sasa hatujapata mrejesho wowote wala taarifa kuhusu lini tutalipwa.
Tunaomba viongozi na mamlaka husika zifuatilie suala hili ili kupata ufafanuzi na kuhakikisha haki yetu ya malipo inalipwa kwa kazi tuliyoifanya. Kukaa kimya kwa muda mrefu kumeleta changamoto kwa wahusika ambao walitumia muda, nguvu na rasilimali zao kutekeleza zoezi hilo.
Pia soma ~ Wahudumu wa Usajili wa Majengo Muleba - Kagera tuliokuwa tunadai tangu Juni 2025 tumeanza kulipwa