'Wahuni' wateketeza mali za kanisa Sumbawanga

'Wahuni' wateketeza mali za kanisa Sumbawanga

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
Watu wasiojulikana,wamevamia na kufyeka ekari 25 za mahindi katika shamba linalomilikiwa na Kanisa la Efatha la Sumbawanga.

Tukio hilo lilitokea wiki iliyopita na eneo lililofyekwa ni sehemu ya ekari 96 za shamba hilo.

Akizungumzia tukio hilo, Meneja wa shamba hilo, Peter Kibona,alisema liligunduliwa na vijana wake walipokuwa wanakwenda shambani kwao. "Walipofika katika eneo hilo, vijana walishangaa kukuta mahindi yakiwa yamefyekwa katika eneo kubwa, kwa kweli inasikitisha sana,"alisema Kibona.

Meneja huyo alisema waliofanya kitendo hicho, wameteketeza kiasi kikubwa na chakula ambacho kingesaidia jamii katika siku zijazo. "Ekari moja inazalisha gunia 20 na kwa hesabu hizo, ekari 25 tungepata magunia 500 ya mahindi," alisema Kibona. Alisema tayari uongozi wa shamba hilo umetoa taarifa za tukio hilo.

Meneja huyo wa shamba, alisema kumekuwa na mfululizo wa matukio katika shamba hilo linalomiliki kihalali na kanisa. "Wananchi waliwahi kuchoma matrekta mapya mawili yanayomilikiwa na Efatha jambo ambalo ni hasara kwao," alisema.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda, alisema polisi wana taarifa za tukio hilo na kwamba tayari wameanza kufanya upelelezi ili kujua wahusika na lengo lao.

Source: Mwananchi
PIA SOMA

- Uelewa wangu juu ya kundi la watu wasiojulikana

~ Matukio ya Watu kupotea na wengine kudaiwa kutekwa, nini kinaendelea kuhusu usalama wa raia

- Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana
 
'Wahuni' wafyeka ekari
25 za mahindi.
Watu wasiojulikana,
wamevamia na kufyeka
ekari 25 za mahindi
katika shamba
linalomilikiwa na Kanisa
la Efatha la Sumbawanga. Tukio hilo lilitokea wiki
iliyopita na eneo
lililofyekwa ni sehemu
ya ekari 96 za shamba
hilo. Akizungumzia tukio
hilo, Meneja wa shamba
hilo, Peter Kibona,
alisema liligunduliwa na
vijana wake
walipokuwa wanakwenda shambani
kwao. “Walipofika katika eneo
hilo, vijana
walishangaa kukuta
mahindi yakiwa
yamefyekwa katika
eneo kubwa, kwa kweli inasikitisha sana,”
alisema Kibona. Meneja huyo alisema
waliofanya kitendo
hicho, wameteketeza
kiasi kikubwa na
chakula ambacho
kingesaidia jamii katika siku zijazo. “Ekari moja inazalisha
gunia 20 na kwa hesabu
hizo, ekari 25 tungepata
magunia 500 ya
mahindi,” alisema
Kibona. Alisema tayari uongozi
wa shamba hilo umetoa
taarifa za tukio hilo. Meneja huyo wa
shamba, alisema
kumekuwa na mfululizo
wa matukio katika
shamba hilo linalomiliki
kihalali na kanisa. “Wananchi waliwahi
kuchoma matrekta
mapya mawili
yanayomilikiwa na
Efatha jambo ambalo ni
hasara kwao,” alisema. Kamanda wa Polisi wa
Mkoa wa Rukwa, Jacob
Mwaruanda, alisema
polisi wana taarifa za
tukio hilo na kwamba
tayari wameanza kufanya upelelezi ili
kujua wahusika na
lengo lao.

Source:Mwananchi

Wangefyeka ekari zote, hizo nyingine wamemwachia nani
 
Waisilamu wao pia maana wanatufuatfuata ss. Ee mungu tsaidie
 
... Udini tena!
Serikali ihunde tume ili kubainisha wahusika, na nia zao nini.
Pia waletwe wapelelezi wa kimataifa wa kukodishwa "IFB au CIA" ili kuchunguza hili suala.
 
Nachojua kuna mgogoro mkubwa kati ya wana kijiji na Efatha kwenye umilikaji wa hilo shamba. Na kwa sababu serikali haiwezi kumaliza migogoro ya ardhi then wanakijiji wanajichukulia sheria mkononi. Mpaka atakapouwawa mtu hapo ndipo na waziri mkuu utasikia kaenda. Usipoziba ufa utajenga ukuta.
 
Inasemekana wamiliki wa hilo shamba EFATHA waliweka walinzi,nasikia ni wamasai walikua wanalinda na bunduki.Walikataza raia yeyote kupita maeneo yale,na wengi wanaopita ni wenyeji wa hayo maeneo.Kuna mama mmoja mwenyeji wa hapo alipita na mtoto wake mgongoni akarushwa kichura na hao jamaa.

Hadi sasa nasikia walinzi hao walivamiwa na wanakijiji na kukatwakatwa na mapanga hadi ICU Sumbawanga.

Hiki kisa nimesimuliwa leo na mwenyeji wa huko karibu na gereza la MORO Sumbawanga tulipokua tunasafiri toka Sumbawanga-Mbeya.
 
... Udini tena!
Serikali ihunde tume ili kubainisha wahusika, na nia zao nini.
Pia waletwe wapelelezi wa kimataifa wa kukodishwa "IFB au CIA" ili kuchunguza hili suala.

mwishoo na wake zenu wakichukuliwa mtaagiza fbi ili wachunguze mbinu walizotumia kuwarubuni,
 
EFATHA kaeni na raia mmalize matatzo yenu hukohuko,alafu mnasema gunia 500 zingesaidia wananchi,kama lini na watu gani?
 
Waislamu wanavuna sifa mbaya kwa kuwa na mtiririko wa vitendo vya kutumia nguvu na jazba hata katika mtafaruku mdogo tu! hivyo basi kwa kuwa wapinzani wa kubwa wa imani ya kikristo ni waislamu basi tatizo lolote litakalo wapata wakristo moja kwa moja mhtumiwa wa kwanza ni waislamu lakini ukweli wa uhalibifu huu hauhusiani na mitafaruku ya kidini, ushauri wangu waislamu jaribuni kutumia busara kwenye maamuzi panic na jazba it is a wrong way to solution
 
ukiishi na watu vizuri nao watakujali, km ukiwawaona hawa masikini hawana kitu watanisaidia nini na dharau kibao matokeo yake ndo haya
 
Waislamu wanavuna sifa mbaya kwa kuwa na mtiririko wa vitendo vya kutumia nguvu na jazba hata katika mtafaruku mdogo tu! hivyo basi kwa kuwa wapinzani wa kubwa wa imani ya kikristo ni waislamu basi tatizo lolote litakalo wapata wakristo moja kwa moja mhtumiwa wa kwanza ni waislamu lakini ukweli wa uhalibifu huu hauhusiani na mitafaruku ya kidini, ushauri wangu waislamu jaribuni kutumia busara kwenye maamuzi panic na jazba it is a wrong way to solution

Ungeanza na hao walifyeka mahindi ya Nabii Tapeli !
Nabii mavi ya kuku.....gademmit !
 
ukiishi na watu vizuri nao watakujali, km ukiwawaona hawa masikini hawana kitu watanisaidia nini na dharau kibao matokeo yake ndo haya

Nabii anadharau watu wake !? Au ndo nabii wa kigalatia ndi vyo walivyo ?
 
Dah ama kweli...Ata kama kanisa lingefyekwa kutokana na huu mgogoro wa ardhi still wangepointiwa dini fulani kumbe ndo maana sometime hua wanaamua kufanya kweli maanake tuhuma nyingi hua wanazishiwa
 
Back
Top Bottom