Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Mashirika mengi makubwa ya kusafirisha mizigo zimeacha kutumia njia ya bahari ya mkato kupitia bahari nyekundu na Suez kutokana na mashambulizi ya wanamgambo wa Houth walioahidi kuzipiga meli zinazoelekea au kutoka Israel wakiwa na lengo la kuwasaidia watu wa Gaza.
Meli hizo imebidi zipite mbali na Yemen na kuzungukia Afrika kusini jambo ambalo limeongeza muda na gharama za safari.Hata hivyo wapiganaji hao sasa wamepata teknolojia ya kuzifikia meli hizo umbali huo zinakopita.
Hapo juzi waliipiga meli iitwayo MV Sarah iliyokuwa umbali wa meli za nautical 246 masafa ya kutoka Dar es salaam na Mtwara.
Mbali ya shambulio hilo leo tena kwa mara ya mwanzo wanamgambo hao wametangaza kuilenga meli kwenye bandari ya Haifa ambayo ni bandari kubwa ya Israel kule meli zinazozungukia Afrika kusini huenda kutia nanga.