Poleni sana wamama wnenzangu. Ndo hayo ninayoyakataa mimi. sijasema kuwa wangu ni msafi sana, ila sitaki kuja kujuta............ hata mimi kuna kipindi huwa napata sana kishawishi cha kuangalia simu ya mzee. utakuta kuna kipindi anapokea sms halafu kwa jinsi wasivyojua kujikausha utaona kabisa kuna walakini, lakini huwa napotezea kiaina ili nisizushe la kuzusha. na sometimes hali hiyo ikinikuta sana huwa nasali na kumkemea shetani; maana naona ni lishetani tu hilo linataka kuniharibia maisha yangu................. nimesema sitaki presha mimi, na itakuwa hivyo... sigusi simu yake ng'o, hata akiisahau akaenda kazini ataikuta alipoiacha. full stop!