Waigizaji wa Tanzania wana la kujifunza kwenye tamthilia ya Mpali

Waigizaji wa Tanzania wana la kujifunza kwenye tamthilia ya Mpali

Kwamba hakuna aliyemuona Benson Logic?? Jamaa ananikeraga sana hadi napenda niwe naangalia scene zake tu.
Yeye na dada yake Shupiwe, aah ile familia hatari
Na mjomba Patrik yule wa getini (mshua boi)😂🤣🤣
 
Kwani imeisha?? Nayo naskia ni kama isidingo haiishi.

Kinachonikera kwenye tamthilia ni hicho tu, hizi chuma haziishagi.

Nakumbuka ni 2021 sijui ile, nilikuta home wanakimbizana kuangalia huba, ajabu mpaka 2023 naskia bado ipo. Nahamaki zaidi ati hadi leo 2024 bado chuma ipo tu, huwa mnaangalia vinini hivyo visivyoisha.

Ikaanza hiyo juakali, mwanzo ilisifiwa sana nikaona sio kesi nichingulie kidogo, mwanzo story ilikua inaflow vizuri mno, lahaula ghafla bin vuu waigizaji wakaanza kuongezeka, mara huyu mara yule. Ikawa mparanganyiko yani vululu vululu nayo ni ivo ivo haiishi na kuisha kwake ni mpaka labda Lamata afulie, au Dstv wagome kumpa maokoto.
 
Wakati sina kazi nilikuwa naifuatilia kila siku, ni nzuri. Baada ya kupata kazi naishia kuisikia tu
 
Na mjomba Patrik yule wa getini (mshua boi)😂🤣🤣
Yule mzee si Alitaka kufukuzwa kazi? Kumbe bado yupo getini 1😎
Mtoto wake huyo mzee yuko wapi kwa sasa?
 
Yule mzee si Alitaka kufukuzwa kazi? Kumbe bado yupo getini 1😎
Mtoto wake huyo mzee yuko wapi kwa sasa?
Wote wapo shambani kwa nguzu mshua boi getini alafu mtoto wake yupo na Hambe
 
Back
Top Bottom