Kwani imeisha?? Nayo naskia ni kama isidingo haiishi.
Kinachonikera kwenye tamthilia ni hicho tu, hizi chuma haziishagi.
Nakumbuka ni 2021 sijui ile, nilikuta home wanakimbizana kuangalia huba, ajabu mpaka 2023 naskia bado ipo. Nahamaki zaidi ati hadi leo 2024 bado chuma ipo tu, huwa mnaangalia vinini hivyo visivyoisha.
Ikaanza hiyo juakali, mwanzo ilisifiwa sana nikaona sio kesi nichingulie kidogo, mwanzo story ilikua inaflow vizuri mno, lahaula ghafla bin vuu waigizaji wakaanza kuongezeka, mara huyu mara yule. Ikawa mparanganyiko yani vululu vululu nayo ni ivo ivo haiishi na kuisha kwake ni mpaka labda Lamata afulie, au Dstv wagome kumpa maokoto.