Tetesi: Waihiga Mwaura kuwa Mrithi wa Salim Kikeke BBC

Notorious thug

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2021
Posts
2,817
Reaction score
10,667
Baada ya Salimu Kikeke kutangaza rasmi kustaafu kazi ya utangazaji pale BBC swali kubwa lilikua nani mrithi wake?

Kutoka The Citizen Tv ya nchini Kenya hadi BBC ni ndugu Waihiga Mwaura(38) ambaye amehudumu The Citizen Tv kwa miaka kumi na nne(14) ndio anayeenda kuirithi nafasi ya Salim Kikeke.

 
ndo ujue Waandishi wenye uweledi bongo niwachache

BBC walichungulia na kuona waandishi wa habari ambao kutwa ni KUSIFIA NA KUABUDU UJINGA.Waroho wa teuzi na si wa sema kweli.

Toka ametoka charlse hillary, zuhura yunus na sasa kikeke hakuna replacment yyte ya maana toka TZ zaidi ya Ambwene Mwamwaja.

KUNA HAJA YA MIANDISHI YA TANZANIA MINGI KUBADILIKA, TASNIA YA HABARI HAITAKI UCHAWA
 
Natamani angekua mtanzania tena, tatizo watangazaji wa tanzania hawako professional wengi ni machawa na elimu wise hawako vizuri. Wakenya wamejipanga japo kiswahili chao wame jifunzia Tanzania, kwamfano Mauleed kitenge angeweza ila mihemuko mingi sana na kelele.
 
Natamani angekua mtanzania tena, tatizo watangazaji wa tanzania hako professional wengi ni machawa na elimu wise hawako vizuri. Wakenya wamejipanga japo chao wamejifunzia Tanzania
Kinachowasumbua Watangazaji wengi wa Tanzania ni Njaa kugeuka kua machawa na kufanya mambo mengi ya kitoto ili kutafuta trending.
 
Kinachowasumbua Watangazaji wengi wa Tanzania ni Njaa kugeuka kua machawa na kufanya mambo mengi ya kitoto ili kutafuta trending.
Tanzania ni nchi peke inao kosa serious daily Gazeti, serious Radio stetion, FM zote muondo wa presenters ni ule ule, TV ndo usiseme ukiondoa UTV ya Azam zingine taarifa ni ile ile, maanake tumeshindwa kutoa journalist wa maana wote ni wasakatonge machawa.
 
Miaka ya nyuma tulikuwa tunapeleka waandishi wetu huko miaka ya hivi karibun sioni tukifanya hivyo
Hata chuo kikuu miaka ya nyuma tulikua na professor wenye majina makubwa kwenye kila department, unatamani kumsikiliza, sasa neenda udom na udsm uone ma profesor uliopo hawana hata academic popularity, sasa hivi tunarudi reverse sio mbele tena.
 
Zama za Salim kikeke,Tido,Charles Hiraly,zimepita,sasa hv bongo hakuna waandishi wa habari,Kuna wapayukaji tu!na wachambuzi wa mpira,na maisha ya watu,
Na wanachojua ni kufanya vituko Ili "vitrend"mitandaoni,
Akili kubwa zipo Kenya!!
Sasa mtu ana hama Efm kwenda Wasafi!!anaona big deal kisa mshahara usiofika 10M!!
 

Attachments

  • Screenshot_20230502-120640_2.jpg
    65.1 KB · Views: 8
  • 20230502_133922.jpg
    170.4 KB · Views: 8
Kwa bongo ,yupo mmoja tu,Daniel Kijo,ni foreign correspondent wa SABC!
Huyu ni akili kubwa!!
 
Akina Adam mchomvu, mwijaku na masanja nao wangeapply huko BBC ili kupeperusha bendera ya TZ anga za kimataifa
Waende kupigana mitama huko studio,
Mwingine anaongea na kucheka mwenyewe.
Huyo mwingine mwache aendelee kuvalishwa night dress kwanza na kukata miuno mpk badae
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…