Waimbaji nyimbo za injili wanakera sana

Waimbaji nyimbo za injili wanakera sana

KIBURUDISHO

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2011
Posts
1,002
Reaction score
277
WanaJF wenzangu mimi binafsi kwa kipindi kirefu huwa nakerwa sana na hawa waimbaji wa nyimbo za injili,hadi najiuliza hivi hakuna chombo kinachoratibu maadili na mienendo ya hawa waimbaji wa nyimbo za injili?.Hasa kinachokera ni mavazi wanayoyavaa sijui kama kwenye biblia kuna sehemu inayomruhusu mwanamke kuvaa suruali.Waimbaji hawa wakumbuke kuwa biblia haifanyiwi marekebisho kama katiba na pia kama wanashindana na waimbaji wa kizazi kipya wawe wazi tuwaelewe mmoja wao namnukuu anayeimba SHETANI HUNIWEZI IMEKULA KWAKO!!!!!!
 
Wako kibiashara zaidi!
 
Wanatafuta mbinu za kufanya kazi zao ziuzike, so wana check kwanza watu wanapenda kuona mavazi gani, bado kidogo tutaona na vimini vinavaliwa
 
Wanatafuta mbinu za kufanya kazi zao ziuzike, so wana check kwanza watu wanapenda kuona mavazi gani, bado kidogo tutaona na vimini vinavaliwa
Hayo ndiyo maneno,....
 
Muziki ni biashara, na wewe ukitaka anza kuimba kaswida kwa magita na vinanda, tena piga kaswida yako kwa mahadhi ya hot funky ndio itabamba kinoma, halafu utaitwa MBUNIFU
 
Wanatafuta mbinu za kufanya kazi zao ziuzike, so wana check kwanza watu wanapenda kuona mavazi gani, bado kidogo tutaona na vimini vinavaliwa

Kwani lengo lao ni nini? Mi navyojua lengo la nyimbo za injili ni kumsifu kumtukuza na kumwabudu Mungu aliyejuu, suala la mauzo hilo ni kama sadaka kwa sababu Mungu aliamuru makuhani wale madhabahuni hali kadhalika waimbaji lakini sasa wameipa kipa umbele biashara kuliko kumsifu Mungu hence sasa wanachofanya ni ubatili mtupu na kujilisha upepo hawaimbi kwa ajili ya kumsifu aliye juu bali kushibisha matumbo yao ndo mana tungo zao zikoziko tu hazitukuzi chochote huwezi linganisha hata na zaburi ya Daudi kwa ujumla wamepotoka na kupungukiwa na utukufu wa Mungu na kubaki na utukufu wa dunia kumbuka kumsifu Mungu kwawapasa wanyofu wa mioyo na Mungu hukaa katika sifa na Mungu ni Mungu mwenye wivu.
 
bora umeliona hilo ndugu yangu maana wamekuwa waimbaji wa mipasho na sio injili ya kweli. pia wapo kibiashara zaid ndio maana wanavurunda tu mambo yao
 
There is nothing godly about their singing anyway, hawa ni opportunists tu wamepata mwanya wa kudanganya watu.
Jaribu hata kusikiliza nyimbo zao utaona ni chorus tu the rest ni blah blah
 
Usiangalie MAVAZI! Angalia mioyo yao! Maana mavazi hawatakwenda nayo mbinguni! suala la kibiashara zaidi! hivi mnataka wakale wapi? Ajira zenyewe ndio hz!
 
Kama sikosei-Daudi alimwimbia Mungu hadi mavazi yake yakamtoka-sembuse hawa wanaovaa suruali?
me nazani swala si suruali-swala ni imani na behaviour zao,kuna watu hata macho wameficha ila mambo yao ni makuu
 
Na wale wanaovaa magauni yaliyobana hadi zile nguo za sirini zinaonekana mbona hamuwasemi? Naona mmengangania tu suruali. Dont judge a book by its cover. Hakuna vazi litakalompeleka mtu Mbunguni bali imani na mtendo yako. Chamuhimu ni kuwashauri waangalie na mitindo ya nguo wanazovaa imekaaje.
 
huwa naogopa sana kuitumia hii justification imani na matendo.ivi umetoka kwenye kideo umegonga bikini unamwimbia bwana, ndio una matendo mia,imani mia lakini what about us!tunaokuangalia huoni unatikisa imani yetu hutuonei huruma!vaa kwa staha bana kha!
 
Bora za Rc ndio hazjakaa kibiashara.
 
wachungaji/mapadre/masheikh wanabaka waumini wao seuze hao waimbaji wenye vivazi??

by the way ndugu yangu, kwenye hukumu ya mwisho utasimama wewe peke yako...usijeshangaa huyo unayesema anakukera ndiye akanyakuliwa wewe ukabaki!

wee angalia maandiko yanasema nini. period.
 
UMEKOSEA! sema baadhi ya waimbaji. wapo wanaojiheshimu na wanaimba ktk ROHO NA KWELI. usiconclud kwa mawazo yako
 
WanaJF wenzangu mimi binafsi kwa kipindi kirefu huwa nakerwa sana na hawa waimbaji wa nyimbo za injili,hadi najiuliza hivi hakuna chombo kinachoratibu maadili na mienendo ya hawa waimbaji wa nyimbo za injili?.Hasa kinachokera ni mavazi wanayoyavaa sijui kama kwenye biblia kuna sehemu inayomruhusu mwanamke kuvaa suruali.Waimbaji hawa wakumbuke kuwa biblia haifanyiwi marekebisho kama katiba na pia kama wanashindana na waimbaji wa kizazi kipya wawe wazi tuwaelewe mmoja wao namnukuu anayeimba SHETANI HUNIWEZI IMEKULA KWAKO!!!!!!

Hapo nilipoweka nyekundu naona umekosea:

300 Changes In The NIV and Other Modern Bible Versions

source: 300 Changes In The NIV and Other Modern Bible Versions

Isiyobadilika ni Qur'an pekee.
 
Back
Top Bottom