KERO Waingizaji wa mizigo walalamikia TBS kwa kuchelewa kutolewa kwa Control Number na gharama kubwa za storage

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Waingizaji wa mizigo kutoka nje ya nchi tunaendelea kukabiliwa na changamoto kubwa kutokana na kuchelewa kwa mfumo wa TBS kutoa Control Number.

Kwa mfano, ombi langu liliwasilishwa tangu Jumatano iliyopita, lakini hadi sasa sijapatiwa Control Number, hali ambayo imenilazimisha kuanza kulipa gharama za kuhifadhi mzigo (storage) kiasi cha Dola za Marekani 60 kwa siku.

Hali hii imekuwa ikisababisha hasara kubwa kwa waingizaji wa bidhaa, ambao hulazimika kugharamia ucheleweshaji ambao haujasababishwa na wao.

Tunaomba mamlaka husika zifuatilie suala hili na kuchukua hatua za haraka kuboresha mfumo huo ili kupunguza changamoto na hasara zinazoendelea kuwakumba waingizaji wa bidhaa nchini.

Tunawasilisha malalamiko haya kwa heshima na matumaini ya kupata ufumbuzi wa haraka.
 
Mpaka leo hawana a single unified intergrated system? yaani wanasumbua pale ,ilitakiwa vitu vyote vitoke sehemu moja ya Singel window au Tancis ..Hizi Taasisi wanapingana kutokana na maslahi .
 
Waingizaji wa mizigo kutoka nje ya nchi tunaendelea kukabiliwa na changamoto kubwa kutokana na kuchelewa kwa mfumo wa TBS kutoa Control Number.

Kwa mfano, ombi langu liliwasilishwa tangu Jumatano iliyopita, lakini hadi sasa sijapatiwa Control Number, hali ambayo imenilazimisha kuanza kulipa gharama za kuhifadhi mzigo (storage) kiasi cha Dola za Marekani 60 kwa siku.

Hali hii imekuwa ikisababisha hasara kubwa kwa waingizaji wa bidhaa, ambao hulazimika kugharamia ucheleweshaji ambao haujasababishwa na wao.

Tunaomba mamlaka husika zifuatilie suala hili na kuchukua hatua za haraka kuboresha mfumo huo ili kupunguza changamoto na hasara zinazoendelea kuwakumba waingizaji wa bidhaa nchini.

Tunawasilisha malalamiko haya kwa heshima na matumaini ya kupata ufumbuzi wa haraka.
Tatizo kubwa huwezi kulodge zbs mpaka upate assessment ya Tra, wakati zamani ilikua unalodge kwa pamoja, ni kama kuna conspiracy hivi
 
Back
Top Bottom