Waislam kwanini mnaangalia mwandamo wa mwezi?

Aisee umenidadavulia vizuri sana sasa nimekupa, shukrani sana
 
Kwarezma anafunga nani bna,mapadre wenyewe wanapiga gambe tu,kwarezma hufungua kwa kula futari ya mihogo,viazi nk!?
Kufunga ni kufunga tunatofautiana malengo...kwa hiyo KWAREZMA wakifuturu jioni wanakula Dona ndugu !!..tumbo ni lile lile.
 
Sasa kwanini mpaka atangaze Mufti kwamba Mwezi umeonekana? Si atuache tuuone wenyewe?
Ukiona unafunga pia sio shida, Mufti anatanga kwa maana yeye ni Kiongozi na hivyo huwa anapata taarifa kutoka vyanzo mbalimbali, na kwa kuwa kiongozi taarifa yake huwa sahihi, hivyo tamko lake linathibitisha kweli mwezi umeandama.
 
Umeliza swali zuri na kistaarabu, uislam unaelekeza anaeuliza swali ajibiwe na anaeomba asikaripiwe

Naimani umeshapata majibu mazuri na umeelewa.
 
Ooh,kumbe ulitegemea uone watu wamejisinzisha midomo imewakauka miayo mingii huku ikitoa harufu mbaya na wakianza kuulizana swaumu zao zinaendeleaje huku walikula vyakula mpaka saa 10:00 alfajiri?...
Umepata wapi maelekezo ya kufunga na kufungua!?..ndiyo maana mapadre wanakula gambe tu mchana wa kwarezma,wanaofunga wanajulikana funga yao ikifika,hata premier league wametenga muda kuwapisha wafungulie muda ukifika wakati wa game
 
Leo hii musilamu akisoma studies za kufunga imani yake inongezeka badala ya kupungua, sababu vitu vingi tulivyoambiwa kuhusu kufunga vipo on point.
Naomba unieleweshe kwenye mfumo mzima wa jinsi ya kufunga.

Nimeona, mwisho wa kula ni around 5.09am na kufungulia ni around 6.37pm

Asilimia kubwa ya watanzania na waumini hawamudu milo 3 au 2 kwa siku, sasa huyu mwenye uwezo wa kula saa 10 alfajiri, akashindilia vizuri huku jioni alipiga futari drafti, INAWEZEKANA mfungo ukawa na tofautu na hali ya kutomudu misosi 3 kwa siku?

Siwezi kuishi vizuri tu kwa mchana kama nimeshiba vizuri saa 10 alfajiri? Malengo ya kiimani yanafikiwa kweli?
 
Huwezi kugoogle nadhalia, kwanza haipo alafu kuna nadhalia zinazoishi na zilizokufa ambazo kuna binadamu wanazitumia.
Nadharia kivipi!?..unajua maana ya nadharia!?...
 
Naomba unieleweshe kwenye mfumo mzima wa jinsi ya kufunga.

Nimeona, mwisho wa kula ni around 5.09am na kufungulia ni around 6.37pm...
Jaribu kula saa kumi alfajiri halafu usile mpaka saa moja kwa mwezi mzima,uone Kama malengo yanafukiwa au laa
 
Umepata wapi maelekezo ya kufunga na kufungua!?..ndiyo maana mapadre wanakula gambe tu mchana wa kwarezma,wanaofunga wanajulikana funga yao ikifika,hata premier league wametenga muda kuwapisha wafungulie muda ukifika wakati wa game
Hapo kwa mapadre kula gambe  kuna uelekeo unataka tuelekee ila mimi sitafika huko,hiyo para ya mwisho ktk post yako,kama uliisoma post yangu uliyoni-quote kwa umakini hilo nililiandika kwamba wewe na wenzako mnafanya kitu kwa binadamu kwanza Mungu wenu baadae(na wafanyabiashara wazungu wapo well off na nyie)

Umesahau kuongeza vyombo vya habari kutoa update kuhusu mfungo wenu,magazeti radio etc,Wakristo hata vyombo vya habari wanavyovimiliki wao havitakiwi vifanye hivyo kwa sababu "funga ni kati ya muumini na Mungu wake tu". kwa imani yangu mimi hapa hata wewe kujua kwamba nimefunga (japo hunijui sikujui) nimeshajikweza na ni unafiki nimefanya.

Hapa nipo na jamaa yangu Msambaa anapiga simu kwa ndugu zake akiwafahamisha kwamba leo ameanza kufunga na akitaka kujua vipi kuhusu wao?imani yangu siyo yeye tu wote hata wewe huwa mnafanya hivyo but kwa sasa ni vyema tuachane na hili.
 
Una mvurugiko wa kifikra bwashee
 
Akhiiy naweka sawa kidogo kuhusu hadithi inayosema fungeni mpate afya ni hadithi dhaifu Kwaiyo usiitumie apo ni makosa

Nawasilisha
 
1. Wapo watu wanajishindilia ila ni vyema kula kiasi

2. Hayo masaa 13 ambayo umefunga ndio masaa ya mishe, haijalishi umekula kiasi gani kabla kama umeamka umeenda kazini na kufanya shughuli zako za kila siku ile effect ya funga itakuja tu,

3. Pia funga si kula tu, tunafunga kufanya maovu pia
 
Hivyo ni kalenda ya kidemokrasia sana, maana katika kalenda yetu ya kawaida hatuwezi kufuata mwendo wa wakati moja kwa moja tunapaswa kuamini wataalamu.
with scientific evidence siyo kuwaamini from the vacuum! Uliyoyasema ndiy hayo ya zamani sasa tunatumia hii system kusoma mwaka
A year is the time Earth takes for one complete orbit around the sun and it is a little more than 365 days, plus nearly another quarter day

and this can be predicted precisely by modern science
 
Ni mawazo yako sikupingi ila usifosi.
It is not a matter of mawazo yangu, unaangalia kama kuna logic! Zamani Misri kubarehe kwa mtoto wa kuime kulihusishwa na kukoja damu at the age of puberty. Kumbe schistosomiasis infection at that age ndipo inapokuwa ime culminate na kutoa damu. Kwasababu hawakuwa na majibu ya science, basi wakasema mtoto amebalehe! SASA WANA MAJIBU YA SCIENCE KUWA HIYO NI DALILI ZA SCHISTOSOMIASIS

Egyptians have had a long history of symptoms caused by schistosomiasis, notably hematuria, which appeared classically in young boys and was once deemed to be a sign of puberty. It was in Egypt in 1851 that Theodore Bilharz discovered, in autopsy material that the causative agent of hematuria was schistosoma[2].
 
Nilishakwambia usinifosi chief hao wa Misri unaniletea mimi ili iweje kwani hiyi ndio reference yangu niliyo anza nayo.
 
Mkuu ila wewe na mimi tunapaswa KUAMINI habari hizo kuhusu mwaka na tarehe. Angalau Waislamu wanaweza kuona na kuhesabu wenyewe. Pamoja na hayo, mfumo wetu wa kalenda si kisayansi sana. Kuanza Mwaka kwenye Januari haifuati mantiki yoyote ila mapokeo ya utamaduni wa mbali sana, yaani Rumi (kabla ya kuzaliwa Kristo).
Pia tunaendelea kufuata mchana na usiku, ambayo ni tata ukitaka mfumo wa kisayansi ya kukadiria wakati.
Ila kimsingi ujumbe wangu: Wailsamu wakiangalia mwezi ni mtindo mojawapo wa kuhesabu wakati. Hakuna uhusiano na ushirikina au magic au imani potofu. Ina namna yake ya mantiki, ingawa si mtindo unaofaa kuratibu wakati kwa watu walio wengi duniani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…