Waislam na tatizo la ugaidi

Waislam na tatizo la ugaidi

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
KISA CHA ZAHAKI RASHID: KUTOKA MAUAJI YA MWEMBECHAI 1998 HADI MAUAJI YA STAKISHARI 2015

20140129_184842.jpg
Zahaki Rashidi

Ndugu msomaji,

Ili uweze kufaidikia na kisa cha Zahaki Rashid ni muhimu kwanza usome mwanzo wa matatizo yake mwaka wa 1998 baada ya kutokea mauaji ya Mwembechai yeye akiwa afisa wa polisi.

Tafadhali ingia hapa:

Mohamed Said: Sajenti Rashid Zahaki na Mauaji ya Mwembechai ya Ijumaa 13 Februari 1998

Zahaki, mtuhumiwa wa Stakishari anayeamini anafanyiwa visasi

- Alikuwa shuhuda muhimu wa Mauaji ya Mwembechai

Zahaki Rashidi Ngai si jina geni katika masikio ya Waislamu wengi hapa nchini. Yeye ni mmoja kati ya wanaharakati wachache ambao wametajwa sana na masheikh, vyombo vya habari na hata katika vitabu maarufu vilivyoandikwa na waataaluma wa Kiislamu.

Umaarufu wa Zahaki umetokana na kutajwa shuhuda muhimu wa tukio la mauaji ya Mwembe Chai na dhuluma mbalimbali ambazo Serikali imewatendea Waislamu.

Kwa mara ya kwanza, Zahaki alitoa ushuhuda wake kwa mwanahistoria maarufu Muhammedi Saidi. Alifanyiwa mahojiano maalum kuhusu ukweli wa mauaji ya Mwembe Chai. Hapo aliyasema yote aliyoyaiona na aliyoyaamini.

Baada ya hapo, ushuhuda huo ulichapishwa katika kitabu maarufu cha Prof. Hamza Njozi, kilichoitwa, ‘Muslim and state in Tanzania.'

Zahaki atajwa katika ujambazi

Akizungumza na gazeti la Imaan kabla ya kwenda polisi kuhoji kutajwa kwa jina lake katika taarifa zilizozagaa katika mitandao ya kijamii akitajwa kama miongoni mwa wahumiwa wa mauaji yaliyotokea kituo cha polisi Stakishari.

Alisema baada ya kupokea taarifa hizo za kuhusishwa na uhalifu huo, hatua ya kwanza aliyofanya ni kutaka kukutana na waandishi wa habari ili Waislamu wenzake wajue ukweli juu ya dhuluma ambayo jeshi la polisi linajaribu kumfanyia akiamini inatokana na historia yake ya kusema kweli kuhusu tukio la mauaji ya Mwembe Chai.

Alisema kinachotokea sasa ni matokeo ya chuki na kisasi cha muda mrefu kilichotokana na uamuzi wake ya kusema kweli katika tukio lile la mwaka 1998 ambalo lilipelekea kufukuzwa kazi ya polisi na kufedheheshwa baada ya kulikosoa jeshi hilo.

"Najua mtuhumiwa akishafika katika mikono ya polisi ni vigumu kukutana na waandishi wa habari na kuzungumza ukweli. Baada ya kuliona hilo nimeamua kukutana nanyi ili kuwaambia ukweli Waislamu wenzangu kuwa katika tukio hili mimi sihusiki hata kidogo na hata huyo anayetajwa kuwa kiongozi wa kundi simfahamu," alisema Zahaki.

Alisema kutokana na matukio ya Mwembe Chai, Jeshi la Polisi lilikasirishwa na limekuwa likimfuatilia kila hatua ili ipatikane nafasi ya kumpa kesi ili wampoteze ulimwenguni.

"Ndugu waandishi wa habari, mimi miaka yote nipo hapa nchini, nina wake wawili ambao naishi nao. Ajabu ni kwamba Jeshi la Polisi linadai mimi nimerejea kutoka Ethiopia. Huo ni uzushi ambao wanajaribu kuutumia ili nionekane muhalifu wakati ni uongo mtupu", alisema Zahaki.

Zahaki aliongeza: "Jeshi la polisi wawe wa kweli. Wafanye utafiti wao kwa makini badala ya kuvamia watu kwa kuwa shuku kwani hatua hiyo itafanya kukamatwa kwa watu ambao hawana hatia jambo ambalo halitamuathiri mtuhumiwa peke yake bali litaathiri maisha ya watoto, wake na wazazi wake".

"Mimi nilikuwa Sajenti katika kitengo cha ‘Crime Stoppers Unit' - Central Police. Tukio la Mwembe Chai lilivyotokea mimi nilikuwa ndio ‘in charge'. Nilitoa maelezo yangu kuhusu taarifa za tukio hilo lakini jeshi halikuridhika. Wamenifukuzwa kwa aibu na sasa wananishughulikia nje ya Jeshi la Polisi". Alilalamika Zahaki huku machozi yakimlenga lenga.

Ujumbe kwa Waislamu

Zahaki amewataka Waislamu wenzake kumuombea dua kwa mtihani huo ambao ameupata huku akiwahakikishia kuwa hajahusika katika uhalifu huo uliotekelezwa katika kituo cha Stakishari.

"Wa Llaah wa Billaahi sijahusika na uhalifu wa Stakishari, Mwenyezi Mungu anajua zaidi. Nitakwenda kuwahoji kwa nini wametaja jina langu na kulihusisha na mauaji yale, na pia kwa nini wanadanganya umma wa Watanzania kuwa mimi nimerejea kutoka Ethiopia wakati nipo hapa nchini? Wana ajenda gani ya siri" alisema Zahaki.

Aidha, Zahaki alisema anataka Waislamu wajue ukweli wote hata akiwa ameshikwa na Jeshi la Polisi ama kuuliwa katika mazingira ya kutatanisha, wajue kilichomuua ni chuki kutokana na kusema kweli katika kadhia ya Mwembe Chai.

Aibukia Jeshi la Polisi, akamatwa

Kama alivyoahidi kwa waandishi wa habari kuwa angekwenda kuhoji Jeshi la Polisi juu ya jina lake kuhusishwa na mauaji ya Stakishari, Zahaki kweli alifanya hivyo . Lakini taarifa ambayo Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam ilIitoa kwa waandishi wa habari ilisema mtuhumiwa huyo alijisalimisha.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema Mtuhumiwa Zahaki Ngai amejisalimisha kwa Jeshi la Polisi akiwa na wake zake wawili na kusema kuwa wale ambao bado hawajapatikana msako bado unaendelea.

Maneno hayo ya Kamishna Kova ni kama mwiba kwa Zahaki ambaye alishatangaza kuwa anaenda kuhoji kwa nini jina lake limetajwa na sio kujisalimisha. Kama alivyotabiri, inaonekana kama polisi wameendelea kupotosha umma.

Akizungumza na gazeti Imaan, Mwanasheria wa mtuhumiwa huyo alisema wanashangazwa na upotoshaji wa Kamanda Kova kwa umma wa Tanzania kwani Zahaki hakwenda kujisalimisha bali alikwenda kuuliza ukweli wa tetesi anazozisikia katika vyombo vya habari.

Kilindo alisema upotoshaji huo unakera na unaudhi kwani matamshi ya Kamishna wa polisi ni sawa na kuthibitisha kuwa ana uhakika Zahaki ni mhalifu na hivyo kupewa kesi hiyo wakati yeye hakuhusika na kadhia hiyo.

Katika tukio ambalo polisi wanadai Zahaki alihusika, majambazi kadhaa yalivamia kituo cha polisi cha Stakshari na kuua watu saba majira ya saa 5 usiku, Julai 12, 2015. Mpaka sasa tayari watuhumiwa tisa wanahojiwa kuhusiana na tukio hilo.

(Makala kwa hisani ya gazeti la Imaan Agosti 31 - Septemba 6, 2015)
 
Juzi yule kipofu Amon Mpanju kasema mbele ya Magufuli kuwa masheikh wa Uamsho ni magaidi....

Juzi akina Kova wameleta hadithi zao ila haya mambo mwisho wake si mzuri.
 
Duniani hamna haki .ukiwa mkweli unapotezwa. Mfano lowasa .leo hii wanamuona fisadi.histoshe mada zingine kama hizi tunaogopa kuchangia.Wanaweza na ww wakakuambia gaidi wakakupoteza .bhana siku nyingine usilete hizi mada Utachangia mwenyewe utasoma mwenyewe.
 
inakuwaje hata top cream ya nchi ikijaa waislam (rais+makamu wa rais+IGP+mkurugemzi wa TISS+RPC nk) bado waislam waseme wanaonewa? sijaelewa
 
Dua zangu na sala zangu ni ALLAH amfanyie wepesi kwenye kadhia hii, kwenye jambo la haki waislam, wakristo na dini nyegne na wasio na dini ni kuhakikisha kila mtu anapata haki yake kwa mujibu wa sheria, sote tuna haki ya kuishi kwa amani.
 
inakuwaje hata top cream ya nchi ikijaa waislam (rais+makamu wa rais+IGP+mkurugemzi wa TISS+RPC nk) bado waislam waseme wanaonewa? sijaelewa

Nafkiri nikueleweshe kidogo, uislamu na waislamu wanaofata haswa, maelezo ya uislam yanawataka hata wakiwa juu ya wasio waislamu watende haki kwa watu wote kwa waislam na wasio waislam. Hili unalosema sijui unadhihirisha nini/?
 
Mwenye kuamini Duniani tunapita Viongozi wanawahukumu watu wadogo (wanaowaongoza) lakini kuna Kiongozi wetu ataetuhukumu bila ya kuchagua cheo wala uwezo (mali)

naamini hii ni mitihani ukweli anajua mwenyewe na MWENYEZI MUNGU ila usimuombee mtu mabaya kama hajakufanyia ubaya

MWENYEZI MUNGU mkubwa na mwenye kutowa haki
 
inakuwaje hata top cream ya nchi ikijaa waislam (rais+makamu wa rais+IGP+mkurugemzi wa TISS+RPC nk) bado waislam waseme wanaonewa? sijaelewa

Tanga Kwetu,
Hapa si tatizo la vyeo bali tunazungumzia utekelezaji wa hii sheria ya ugaidi
kuwa kuna matatizo makubwa.

Ngoja nikupe mfano.

Mwaka wa 2003 walikamatwa watu kwa tuhuma za ugaidi ilhali si magaidi.
Hii ilikuwa mara tu baada ya sheria ya ugaidi kuridhiwa na rais.

Hawa walikuwa viongozi wa taaisi mbalimbali za Kiislam, taassisi ambazo
zikijishughulishana ujenzi wa misikiti, shule, madras, visima, nyumba za
mayatima na shughuli nyingine za kijamaa mfano wa hizo.

Baadae kwa kukosa ushahidi hawa Waislam waliachiwa.

Leo ni zaidi ya miaka 12 na hili tatizo bado linawakabili Waislam na hakuna
kesi hata moja ambayo ishasikilizwa na kutolewa hukumu.

Hili ndilo tunalololisema Waislam ili serikali ichukue hatua kuona kuwa haki
za msingi za raia wake zinalindwa.

Hili si swala la cheo na dini ya mshika dhamana.
 
Juzi yule kipofu Amon Mpanju kasema mbele ya Magufuli kuwa masheikh wa Uamsho ni magaidi....

Juzi akina Kova wameleta hadithi zao ila haya mambo mwisho wake si mzuri.

Lusungo,
Amon Mpanju hana alijualo masikini ya Mungu anajisemea tu.
Mdomo haumkatai bwana wake.

Sikuambii ukiingiza na kuwa kuna vyombo vya habari vinakurusha.

Sheikh Mselem bin Ali bingwa wa kutafsiri Qur'an hawezi hata kwa
mbali kuwa gaidi.
 
Waislam inabidi wabadilike na kuikataa CCM. CCM na viongozi wake imekuwa iki wanyanyasa na kuwatumia na pia kuwapa uoga kiasi kwamba wanaendelea kuikumbatia serikali hiyo hiyo inayo wanyanyasa na kutegemea kuwa ita badilika. CCM ni ile ile, ikataeni na chagueni mabadiliko.
 
Nafkiri nikueleweshe kidogo, uislamu na waislamu wanaofata haswa, maelezo ya uislam yanawataka hata wakiwa juu ya wasio waislamu watende haki kwa watu wote kwa waislam na wasio waislam. Hili unalosema sijui unadhihirisha nini/?

Kwa hiyo hapo Kova anatenda haki kwa watu wote kumbe!!
 
Kova hatendi haki kwake mwenyewe,polisi,wala taifa
Yeye kila siku maigizo tuu,ni nani aliyekutwa na hatia ya ugaidi mpaka sasa?
 
mungu amfanyie wepesi yeye pamoja na wale wote ambao wanashikiliwa bila hatia,

waislamu na wasiokuwa waislamu.......amiiiin
 
KISA CHA ZAHAKI RASHID: KUTOKA MAUAJI YA MWEMBECHAI 1998 HADI MAUAJI YA STAKISHARI 2015

20140129_184842.jpg
Zahaki Rashidi

Ndugu msomaji,

Ili uweze kufaidikia na kisa cha Zahaki Rashid ni muhimu kwanza usome mwanzo wa matatizo yake mwaka wa 1998 baada ya kutokea mauaji ya Mwembechai yeye akiwa afisa wa polisi.

Tafadhali ingia hapa:

Mohamed Said: Sajenti Rashid Zahaki na Mauaji ya Mwembechai ya Ijumaa 13 Februari 1998

Zahaki, mtuhumiwa wa Stakishari anayeamini anafanyiwa visasi

- Alikuwa shuhuda muhimu wa Mauaji ya Mwembechai

Zahaki Rashidi Ngai si jina geni katika masikio ya Waislamu wengi hapa nchini. Yeye ni mmoja kati ya wanaharakati wachache ambao wametajwa sana na masheikh, vyombo vya habari na hata katika vitabu maarufu vilivyoandikwa na waataaluma wa Kiislamu.

Umaarufu wa Zahaki umetokana na kutajwa shuhuda muhimu wa tukio la mauaji ya Mwembe Chai na dhuluma mbalimbali ambazo Serikali imewatendea Waislamu.

Kwa mara ya kwanza, Zahaki alitoa ushuhuda wake kwa mwanahistoria maarufu Muhammedi Saidi. Alifanyiwa mahojiano maalum kuhusu ukweli wa mauaji ya Mwembe Chai. Hapo aliyasema yote aliyoyaiona na aliyoyaamini.

Baada ya hapo, ushuhuda huo ulichapishwa katika kitabu maarufu cha Prof. Hamza Njozi, kilichoitwa, ‘Muslim and state in Tanzania.'

Zahaki atajwa katika ujambazi

Akizungumza na gazeti la Imaan kabla ya kwenda polisi kuhoji kutajwa kwa jina lake katika taarifa zilizozagaa katika mitandao ya kijamii akitajwa kama miongoni mwa wahumiwa wa mauaji yaliyotokea kituo cha polisi Stakishari.

Alisema baada ya kupokea taarifa hizo za kuhusishwa na uhalifu huo, hatua ya kwanza aliyofanya ni kutaka kukutana na waandishi wa habari ili Waislamu wenzake wajue ukweli juu ya dhuluma ambayo jeshi la polisi linajaribu kumfanyia akiamini inatokana na historia yake ya kusema kweli kuhusu tukio la mauaji ya Mwembe Chai.

Alisema kinachotokea sasa ni matokeo ya chuki na kisasi cha muda mrefu kilichotokana na uamuzi wake ya kusema kweli katika tukio lile la mwaka 1998 ambalo lilipelekea kufukuzwa kazi ya polisi na kufedheheshwa baada ya kulikosoa jeshi hilo.

"Najua mtuhumiwa akishafika katika mikono ya polisi ni vigumu kukutana na waandishi wa habari na kuzungumza ukweli. Baada ya kuliona hilo nimeamua kukutana nanyi ili kuwaambia ukweli Waislamu wenzangu kuwa katika tukio hili mimi sihusiki hata kidogo na hata huyo anayetajwa kuwa kiongozi wa kundi simfahamu," alisema Zahaki.

Alisema kutokana na matukio ya Mwembe Chai, Jeshi la Polisi lilikasirishwa na limekuwa likimfuatilia kila hatua ili ipatikane nafasi ya kumpa kesi ili wampoteze ulimwenguni.

"Ndugu waandishi wa habari, mimi miaka yote nipo hapa nchini, nina wake wawili ambao naishi nao. Ajabu ni kwamba Jeshi la Polisi linadai mimi nimerejea kutoka Ethiopia. Huo ni uzushi ambao wanajaribu kuutumia ili nionekane muhalifu wakati ni uongo mtupu", alisema Zahaki.

Zahaki aliongeza: "Jeshi la polisi wawe wa kweli. Wafanye utafiti wao kwa makini badala ya kuvamia watu kwa kuwa shuku kwani hatua hiyo itafanya kukamatwa kwa watu ambao hawana hatia jambo ambalo halitamuathiri mtuhumiwa peke yake bali litaathiri maisha ya watoto, wake na wazazi wake".

"Mimi nilikuwa Sajenti katika kitengo cha ‘Crime Stoppers Unit' - Central Police. Tukio la Mwembe Chai lilivyotokea mimi nilikuwa ndio ‘in charge'. Nilitoa maelezo yangu kuhusu taarifa za tukio hilo lakini jeshi halikuridhika. Wamenifukuzwa kwa aibu na sasa wananishughulikia nje ya Jeshi la Polisi". Alilalamika Zahaki huku machozi yakimlenga lenga.

Ujumbe kwa Waislamu

Zahaki amewataka Waislamu wenzake kumuombea dua kwa mtihani huo ambao ameupata huku akiwahakikishia kuwa hajahusika katika uhalifu huo uliotekelezwa katika kituo cha Stakishari.

"Wa Llaah wa Billaahi sijahusika na uhalifu wa Stakishari, Mwenyezi Mungu anajua zaidi. Nitakwenda kuwahoji kwa nini wametaja jina langu na kulihusisha na mauaji yale, na pia kwa nini wanadanganya umma wa Watanzania kuwa mimi nimerejea kutoka Ethiopia wakati nipo hapa nchini? Wana ajenda gani ya siri" alisema Zahaki.

Aidha, Zahaki alisema anataka Waislamu wajue ukweli wote hata akiwa ameshikwa na Jeshi la Polisi ama kuuliwa katika mazingira ya kutatanisha, wajue kilichomuua ni chuki kutokana na kusema kweli katika kadhia ya Mwembe Chai.

Aibukia Jeshi la Polisi, akamatwa

Kama alivyoahidi kwa waandishi wa habari kuwa angekwenda kuhoji Jeshi la Polisi juu ya jina lake kuhusishwa na mauaji ya Stakishari, Zahaki kweli alifanya hivyo . Lakini taarifa ambayo Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam ilIitoa kwa waandishi wa habari ilisema mtuhumiwa huyo alijisalimisha.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema Mtuhumiwa Zahaki Ngai amejisalimisha kwa Jeshi la Polisi akiwa na wake zake wawili na kusema kuwa wale ambao bado hawajapatikana msako bado unaendelea.

Maneno hayo ya Kamishna Kova ni kama mwiba kwa Zahaki ambaye alishatangaza kuwa anaenda kuhoji kwa nini jina lake limetajwa na sio kujisalimisha. Kama alivyotabiri, inaonekana kama polisi wameendelea kupotosha umma.

Akizungumza na gazeti Imaan, Mwanasheria wa mtuhumiwa huyo alisema wanashangazwa na upotoshaji wa Kamanda Kova kwa umma wa Tanzania kwani Zahaki hakwenda kujisalimisha bali alikwenda kuuliza ukweli wa tetesi anazozisikia katika vyombo vya habari.

Kilindo alisema upotoshaji huo unakera na unaudhi kwani matamshi ya Kamishna wa polisi ni sawa na kuthibitisha kuwa ana uhakika Zahaki ni mhalifu na hivyo kupewa kesi hiyo wakati yeye hakuhusika na kadhia hiyo.

Katika tukio ambalo polisi wanadai Zahaki alihusika, majambazi kadhaa yalivamia kituo cha polisi cha Stakshari na kuua watu saba majira ya saa 5 usiku, Julai 12, 2015. Mpaka sasa tayari watuhumiwa tisa wanahojiwa kuhusiana na tukio hilo.

(Makala kwa hisani ya gazeti la Imaan Agosti 31 - Septemba 6, 2015)
Kesi yake iliishia wapi mkuu?
 
Msakaa,
Hizi shutuma za ugaidi hakuna kesi ambayo ushahidi umethibitishwa na mtuhumiwa kuhukumiwa.

Sina taarifa zaidi za Zahaki ingawa nimeuliza sijapata jibu.
Yumkini katoweshwa duniani tayari.
 
Back
Top Bottom