Waislam tunapaswa kuondokana na upofu wa dini la sivyo tutaonekana wote hatuna akili

Muslim schoolers catch emotions way too quickly about their religion and forget critical thinking and logic when facing critical issues.
They become pawns to use by those who want to change the agenda in their favour.
 
Kwa hali hii basi wacha tuheshimu uamuzi wa mahakama kwa hukumu yake kwa sasa kuwa mkataba unaweza kutekelezeka, kama waliyofungua shauri hawajaridhika wanaweza kukata rufaa.
Kusema CCM inawatumia masheikh na maimamu kwa nini tusiseme na CHADEMA nayo inawatumia maaskofu na wachungaji vibaya katika kuupinga mkataba?
Kwa kuwa hata wanaopinga mkataba wanatafuta vipengele vya kuufanya mkataba uwe batili si kwamba hawataki uwekezaji bali hawamtaki muwekezaji kwa kuwa ni mwaarabu na ni muislamu, tuwe wa kweli JokaKuu, hakuna cha zaidi ya hivyo. Tatizo sisi tulichonacho kwenye mioyo hatukizungumzi kwenye hadhira na tunachokizungumza si kile kilichopo kwenye mioyo yetu.
 
huwezi sema natakiwa kujifunza kiswahili,bali uandishi wa kiswahili.hata hivyo asante kwa historia ya uarabuni lakini.
TEC ni wawakilishi wa wakristo wa kikatoliki, waraka waliyoutoa wa kupinga uwekezaji wa DPW kwenye bandari zetu kwa kusema wao wanawawakilisha watanzania wengi wenye kuukataa uwekezaji huo, swali huo wingi wa wanaowakilshwa na TEC wamepimwaje?
wingi ule ule wa idadi inayoanzia hesabu ya 2.sample hii ndogo tu inafaa kusikilizwa kabisa hasa kwa kuzingatia hoja watakazojenga.maana wanawezakuwa wamejenga hoja zenye nguvu kuliko kundi kubwa zaidi ambao kwa makusudi wameamua kuwa kama ng’ombe.
Ikiwa TEC inawawakilisha wapinga mkataba na miongoni mwao wamefika kumshutumu raisi kwa imani yake na uasili wake kwa kusema kwa kuwa yeye ni mzanzibari na muislamu ndiyo maana anataka kuiuza nchi ya Tanganyika kwa waarabu,
nakumbukuka nikikuomba kuleta kipande hiki peke yake katika walaka,kama rejea ya ushahidi toka nimekunukuu kwa mara ya kwanza.
kwa muktadha huo ndiyo maana TEC inaingia kwenye shutuma hiyo. Ni kweli wachungaji wengi wana shahada za juu lakini kwa hili wamekosa hekima kabisa, taasisi ya kidini unaona kuna moto unawaka wewe unakwenda kumwagilia petroli!
kipi rahisi kusema,kwamba raiss ametanguliza uislam na uarabu asili ama ni mjinga hakuusoma na kuuelewa mkataba alioamua kuupitisha???
NOTE:siungi mkono raiss kuitwa mwarabu muislam wala kuitwa mjinga.
kasikikize hotuba ya askofu KKKT,ameeleza vyema kwamba hapo kabla walikaa na rais na kumsihi arekebishe baadhi ya vipengere,kwanini hakuchukua hatua hizi,anajua yeye,bunge lake,na mahakama yake.hivyo tamko la TEC ni katika kumkumbusha kwamba amekiuka kabisa maagizo yao wote kama taasisi za kidini.
Huo waraka hauna afya ya usalama kwa nchi kama yetu, hayo mambo wawaachiye vyama vya siasa vya upinzani vilishughulikie haya mambo ya kuipinga serikali,
hakuna sehemu TEC imeainisha inapinga serikali,sijui kama hata umesoma waraka ama nawewe unaungana uwakilishi na akina mwaipopo!!!!
TEC inapinga mkataba mbovu.
wao wabaki na kondoo wao katika kuimarisha imani za wafuasi wao.
kwakuwa wanasimamia kundi kubwa la kondoo wameamua kuchukua hatua zaidi katika hatma ya maisha ya kondoo hao sababu ni jukumu lao,tofauti na hao wengine ambao wamejipa kazi ya kushughulikia tende za ngamia wao pekee.
Baadhi ya masheikh wamekasirika si kwa sababu ya kupinga uwekazaji wa bandari bali jinsi upingaji ulivyowasilishwa na baadhi ya wanasiasa na viongozi wa dini ya kikristo kwenye mitandano na hata mikutano ya hadhara.
ni ujinga wao tu unawasumbua,hoja mezani ni mkataba mbovu wenye vipengere tatanishi,wanachotakiwa kujikita nacho ni kwanini mkataba huu ni muhimu na hatupaswi kuukosa kwa namna yoyote.
mikataba ya kitaifa na rasilimali za nchi huwa haifichwi kama chupi iliyotoboka,iko wazi,haihitaji watu wale night na perdiem kuichambua.
ndio maana watu wanawashangaa masheikh ni njaa zinawasumbua ama elimu ndio tatizo!!!
Waislamu kutokana na misingi ya sheria zao za dini, ndiyo zimewafanya kuwa na mikataba bora yenye kuwa na uaminifu, haki na uadilfu katika kutekeleza makubaliano yao.
ndio maana hatutaki majibu ya kihisia kama haya maana,dini na sharia za kiislam hazihusiki kabisa hapa,hata hao waarabu wasingeweka vipengere vya kitapeli na dhurma namna hiyo kama kweli Allah ni Mungu anayewasimamia waislam.
 
Muslim schoolers catch emotions way too quickly about their religion and forget critical thinking and logic when facing critical issues.
They become pawns to use by those who want to change the agenda in their favour.
Muslim scholars are very wise.
 
Cc adriz Mufti kuku The Infinity je haya ni ya kweli?
 
Wale wazungu wa kahama barick wanachota dhahabu kila siku lakin sijasikia tamko lolote la TEC
kundi la Watu kama Hawa ni ngumu sana kuwaelimisha, utatumia nguvu nyingi lakini Wana mawazo mgando kichwani
 
Huyo jamaa hana akili kazi yake kukopi na kupaste maandiko bila kuchunguza uhalisia,maandiko matakatifu sio gazeti kuna elimu ya kutafsiri na ufanyaji wake kazi hata bible kuna sehemu nyingi sana za utata ukisoma directly unaweza kusema Mungu wa bible hana msimamo ,katili nk na ukiwapa hivyo vifungu Wagalatia wanakuambia hauwezi kuelewa kama haujapitiwa na roho mtakatifu ,mara hapo haijamasnishwa hivyo nk.

Huyo jamaa ni moja wa wapuuzi na wajinga kuwahi kutokea hapa JF ni wakupuuzwa ,akiweza alete uzi kuwe na open discussion ya hayo maandiko yajadiliwe kisomi bila mihemko kisha ajione jnsi gani alivyo mjinga.
 
japo ni kweli haikua mahali pake hapa lakini anatakiwa aelekezwe sio kubezwa.

kule Youtube kuna mtu anaitwa christian prince,kila muislam anasema jamaa ni muongo na haelewi maandiko,cha ajabu hakuna muislam mwenye elimu anayethubutu kumpigia jamaa amuelekeze namna bora ya kuitafsiri Quran,wanapiga waislam layman wanatukana tu kwa hasira baasi wakati huo waislam wengi wanaacha uislam sababu yake.

na wanazuoni wa kiislam wanasema wazi kwamba sababu kubwa ya waislam hasa vijana kuacha kushikamana na uislam ni sababu ya maswali mengi kukosa majibu kutoka kwa wasomi.
 

..kuna wadini ambao ni Wakristo na Waislamu na wanapinga au kuunga mkono mkataba kwa kusukumwa na imani zao.

..mimi kwa maoni yangu nashauri watu wa aina hiyo wapuuzwe.


..lakini kuna wengi wengine ambao wameunga mkono au wamepinga kwa hoja ambazo zimesimama, na wamesukumwa na uzalendo wao kwa nchi yetu.

..mimi niko upande wa wanaopinga mkataba huu. Sababu za kuwapa Dpw bandari zote nchini hazijitoshelezi. Pia ni jambo la hatari sana na halitoi mwanya kwa sisi kuchomoka ikiwa tutakuja kushindwana na Dpw.

..Pia sikubaliani na maamuzi ya serikali yetu kubadili na kulegeza sheria ya ulinzi wa rasilimali ambayo tumetoka kuitunga majuzi tu mwaka 2017. Napinga sheria hiyo kubadilishwa ili kumpendezesha muwekezaji mmoja Dpw.

..Mwisho, nashauri serikali itoke na tamko la kuanza upya mchakato wa kumpata muwekezaji bandarini. Na Watanzania / Watanganyika tuamue tunataka muwekezaji ktk maeneo yapi, na kwa masharti yapi.
 
mkorinto bado unaandika walaka una tatizo gani? Hebu andika kiswahili kizuri.
Tutamshauri raisi siku nyingine akitaka kufanya mikataba ya uwekezaji itabidi awachukuwe hao wachungaji kwani inaonyesha wana utaalamu wa uandishi wa mikataba kuliko wataalamu wa serikali, yaani wamemshauri raisi baada ya kukataa ushauri wao imebidi waende madhabahuni kushitaki kwa waumini wao. Hata kama Yesu angelikuwepo angewaambia hao maaskofu kama alivyowaambia wafuasi wake "Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na yaliyo ya Mungu mpeni Mungu."
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2023-08-25 at 15.35.00.mp4
    11.4 MB
Taifa haliwezi kuendeshwa kwa kukurupuka, km vipi hao tec waendezao huko vatikani .
 
mkorinto bado unaandika walaka una tatizo gani? Hebu andika kiswahili kizuri.
ni kazi ngumu kuzingatia kanuni zote za uandishi katika mijadala,isimame kama waraka popote nilipoandika walaka.
Tutamshauri raisi siku nyingine akitaka kufanya mikataba ya uwekezaji itabidi awachukuwe hao wachungaji kwani inaonyesha wana utaalamu wa uandishi wa mikataba kuliko wataalamu wa serikali,
sio jambo la ajabu,cha msingi asiwepo atakayejishuku kuonewa wala kuachwa katika hilo.
yaani wamemshauri raisi baada ya kukataa ushauri wao imebidi waende madhabahuni kushitaki kwa waumini wao.
hata ukishauriwa usiuze nyumba na mkeo ili ukalewee chumbani ukakaidi,atatoka apige kelele nje ili watu wote wakushangae.ili madhara yakitokea asiyejumuishwa kwamba hakusimamia nafasi yake.
kama Yesu angelikuwepo angewaambia hao maaskofu kama alivyowaambia wafuasi wake "Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na yaliyo ya Mungu mpeni Mungu."
ndio maana wamesoma walaka tu wala hawajashinikiza rais kujiuzulu wala kuutupilia mbali mkataba huo.
 

Attachments

  • v09044g40000cig8gqrc77u6dqt9958g.mp4
    8.3 MB
JokaKuu upo sahihi kabisa na mtazamo wako, tuache ushabiki wa udini katika mambo yenye maslahi ya taifa, nina uhakika kwamba hoja kama unazozileta ndiyo zingekuwa hoja za msingi halisi wa kupinga huu mkataba, nina uhakika kwa asilimia mia tusingefika katika haya malumbano yasiyo na tija, kuwacha mada husika na kuanza kushambuliana kwenye mtazamo wa udini.
Sisi sote ni watanzania na nia yetu ni kuona nchi yetu inapiga hatua kimandeleo bila ya kujali imani zetu, kwani kuna wangapi walikuwa waislamu huko nyuma wakawa wakristo na kuna wangapi wakristo wamekuwa waislamu, mambo ya imani yabaki kwenye mioyo yetu.
Tanzania tumetoka mbali mpaka kufika hapa tulipo, na tuna safari ndefu mpaka tufike mahali ambapo kila mtanzania atafurahia maisha mazuri kwa utanzania wake. Ulimwengu upo kwenye vita vya kiuchumi, jana tumeona BRICS inavyozidi kukuwa, lazima tusome alama za nyakati. Sisi kama waafrika wengine ambao tumebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi lakini hatufaidki nazo, sidhani kama sababu ni viongozi wetu, na haiwezekani Afrika nzima hatujielwi. Tatizo lipo kwa hao wakoloni wa kisasa wanaondelea kutupelekesha.
Naomba kwanza kama watanzania tujifunze diplomasia ya kiuchumi, tusome sheria zetu tuangalie vipi tunaweza kuzirekebisha ili tuendane na wakati. Tatizo letu tunakosa elimu ya mambo ndiyo maana tunatumia muda mwingi kulumbana katika mambo yasiyo na tija, na kuna mataifa yanafurahia hivi tunavyofarakana.
Tuwe na forums zitakazojadili mambo ya msingi kielimu na si kimihemko.
Tanzania itajengwa na watanzania wenyewe na si vinginevyo.
 
Ewe kijana umejaribu kuelezea jambo kwa hoja ila embu rudi kwanza nyuma hili jambo lilipo anza na mpaka lilipofika umewasikia BAKWATA wakitoa neno lao au kuchangia

JE,umemsikia mufti Zuber au Balaza la ulamaa likitia neno

Unasema wew ni muislam sikatai,unaweza ukawa n kwel muslim ila wajina n sio vitendo
Naomba nikukumbushe kitu viongoz wa Dini waliungna na kutoa mapendokezo yao na wakapewa Ahad ya kuwa yatafanyiwa kaz

Je, TEC wao walishindwa nin kuwa na subra mpak hapo muda waliopewa

Je TEC kutoa walak na kusema kuwa watanzania hawautaki mkataba wa bandar ni haki kuwasemea wtz wote

Kama kwel TEC,walikuwa wanawasemea wtz ni kwel sisi sote ni wakatolik kwa maaan walaka umeenda kusomwa katika makanisa yao na sio kwa wasiokuwa wao

Tafuta nukuu za mwambusi,mbowe na yule mtumish wao na zunguka huko mitandaoni uone kila pande inapotoa hisia zao badala za hoja zen rudi hap unipe nukuu japo moja wa shekh wakat kuhusu bandar

Natoa rai kuwa sio muumini wa BAKWATA ila kweny hil naona wametumia hekima na busara kwa kukaa kimyaa mpka muda utakapo fika

Mwisho kabisa kwako wew mwandish Rudi kasome tena QURAN maana inaweza kuwa sio kwa ajili yako na hao walio tanguliza hisia zao,

Baadhi ya vipengele katik IGA kwa upande wa bandar vina matatizo na vimejadiliwa na mawaziri pamoja na wabunge ambao 95% sio waislamu na kuvipittisha kam ambavyo vilipitishwa huko nyuma na wasomi weny PhD
 
Kifo hakihusiani na dini, labda useme mtu akiwa kwenye dini yako hafi. Lakini ni dhahiri mtu mwenye pesa ama maisha mepesi kuliko mshika dini.
Nimpuuzi tu ndio anamatumani ya kuishi milele kunabwana mmoja alivuna sana mazao akayawaka ghalani alishindwa hats kuwasaidia wenyemahitaji kisha akasema mwaka huu sitopata njaa kabisa kumbe muda wakuishi ulikuwa umebaki ninusu saa tu kipi alipata kikubwa utambue mtu aishi kwa kipande chamkate Bali kwaneno lamungu ndio uzima wamilele were tafuta uzima wamuda
 
Sioni mahusiano yoyote ya haya uyasemayo na dini. Kwenye huo mfano wako hapo tatizo ni kutokushika dini ama kutojua kuna kifo? Sioni mahusiano yoyote kati ya kifo na dini.
 
Hili ndio tatizo letu tukijadiliana bandari tutaingiza uislam, uarabu, halafu kama ulivyofanya jamaa yangu 'Retired' character assasination kwa Mtume wetu, kinachonisikitisha ukatumalizia na cartoon yako kutaka kumtukana Prophet wetu kwa matusi yako ya picha why uende all the way kujitahidi kumchafua, unatakiwa usome kidogo tu kuelewa waliompinga kama wewe mabilion wameshakufa na wala hawatajwi wala kujulikana na yeye anaendelea kuongeza wanaomkubali na kumfuata na wako tayari kupoteza chochote kwa ajili yake, kwa sasa inafika mabillioni sijui mangapi, unafikiri ni coincidence au sisi watu mabilioni kuanzia wakati wake mpaka wakati huu hatuna akili za kupambanua, hatujasoma kama wewe au wengi wanavyojiaminisha, uje wewe na facts zako uchwala za pedophile syndrome tukuone genius, mimi ningekushauri soma kidogo jielimishe utanufaika na utabadilika kimtizamo, utapunguza sumu ya kuwapoteza wengine wasiojua kuuelewa ukweli na kuufuata, unaemtukana amewekwa among the top 100 influencial people na watu wa LEO, narudia sio wale waliomkubali 100 % na kumfuata wa 1400 waliokuwa wamejitolea kukukabili kwa lolote ukijitokeza tu kuwa tishio waliokuwa hawana hata electricity, google upate prove jina lake liko namba moja hakuna binaadam mwengine alio score zaidi, na waliomchagua position hio sio Waislam, hiyo pekee inaweza kukupa motisha kusoma Uislam na huyo Mtume uliomtukana ukamwelewa vizuri kuliko haya unayoandika ukawapoteza wengi, mimi sitetei habari ya bandari kuchukuliwa na waarabu NO, mimi ni mwarabu lakini siko kutetea kama Waarabu wenyewe wameshakuwa matajiri kwa hiyo kuikosa bandari yetu ikiwa hakuna maslahi mapana ya nchi na raia zake Watanzania than hakuna ulazima wa kupewa, tubaki na hoja za bandari itatusaidia au haitusaidii, ukiingiza uislam utajichanganya uislam hautaki watu wadhulumiwe kwa namna yoyote unayoijua wewe, ukiamini tofauti hiyo ni akili yako baki nayo mwenyewe, Huyo uliemtukana katufundisha kusimama na ukweli, na uaminifu, na haki, kutilia mkazo jambo hilo amesema ukija wewe na Uislam wako ukamdhulumu asie Muislam 'mimi kama Muhammad nakuwa wakili wake katika mizani', sasa wewe unae copy na kupaste muelewe huyu hapo ni Mtu wa namna gani, narudia soma ndugu yangu utanufaika, nakutumia link ya clip hiyo sikiliza majibu ya maswali ya Mama Aisha usiyoyajua utaelewa, siyo kama porojo la westerners wanaominisha wanafuata democracies na kuwapa watu haki zao kumbe wanapora rasilimali za nchi masikini na kuwaacha watu destitute omba omba.

View: https://youtu.be/G19zcrkUTEI?si=xfjsijvjgaXrqa7q
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…