Tatizo la mkataba wala halihusiani na dini ya kiislamu, tatizo limekuja hao wakosoaji wamelihusisha jambo la mkataba na dini ya raisi, uasili wake kuwa ni mzanzibari na hao wawekezaji ambao ni waarabu na ni waislamu, baada ya kushambuliwa dini ya kislamu ndiyo ukakuta waislamu wanarejesha mapigo. Kwa kweli waislamu kwenye mambo ya maendeleo ya kiserikali wala hawana shughuli nayo. Serikali na imekuwa ikiingia mikataba na nchi tofauti hujapata kusikia waislamu wametoa waraka, ila panapokuwa na uonevu, udhalilishwaji wa muislamu na dini kwa ujumla hapo waislamu hawana simile. Hayo mambo ya mkataba malizaneni wenyewe lakini msikashifu wala kuwatukana waislamu.Kama kuna kitu Waislamu tunapaswa kukifanya katika kuandika HISTORIA yetu na ikasomwa kila baada ya sala ni hii ya Ikulu ya Magogoni hapa Dar es salaam maana ni historia yetu na ni halali kwetu kufanya hivyo ila sio kwenye suala la Mkataba wa Bandari; huko tunahitaji kuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu mikataba ya kimataifa.
Tujisahihishe
Faida ya mkataba wewe si mwenye ujuzi nao pia, kama ulivyosema kuna wajuzi basi nawe waachiye wajuzi wayashughulikiye mambo yao, tusije nasi tukadhani mfano wako ni wale watakaoathirika na uwekezaji wa DPW. Swala la uchumi wa nchi si swala la dini fulani ni swala la wananchi wote, hata hao waarabu huko nyuma walikuwa hawana lolote lakini baada ya uwekezaji kutoka nchi na watu tofauti na rasilimali zao chahche walizonazo leo nao wamekuwa na ukwasi mkubwa wa kutaka kuendeleza na nchi nyingine kwa manufaa ya wote.
Elimu ya dini ya kislamu ni pana sana, kwenye uislamu kuna elimu ya sheria (asili ya neno ni sharia kwa kiarabu) ambayo ni pana sana kutokana na sheria hizo ndiyo leo unawaona waarabu wameendelea sana huko mashariki ya kati. Nchi kama UAE (Umoja wa Falme za Kiarabu) ambayo imepata uhuru 02-12-1971, nchi ndogo sana yenye kutegemea mafuta (na si falme zote zenye mafuta bali Abu Dhabi ndiyo yenye kuchimba sana mafuta) lakini wamepiga hatua kubwa sana kimaendeleo kuliko sisi nchi iliyopata uhuru 1961,