Uko sahihi. Masheikh wapo kwenye majibizano ya kushindana, wakati maaskofu wanaweka mbele mustakbali wa Taiifa zima ndiyo maana huoni maaskofu wakiandika neno "sheikh", "uislamu", "waislamu" katika waraka wao.
Hao DP World wametimuliwa Djibouti nchi ya asilimia 98 waislamu tupu sembuse hapa kwetu!
Ishu hapa ni mkataba mbovu, siyo habari za uislamu wala Ukiristo
Mbona waislamu wa Uturuki wanajenga SGR maaskofu hawajatoa waraka?
Mbona Waislamu wa Misri wanajenga bwawa la Stieglers maaskofu hawajatoa waraka?
Qur'an inasema simamia haki na sema ukweli hata kama ukweli unakutandika wewe mwenyewe!
Usiposimamia haki na ukweli utaonekana kituko tu, bali yule asimamiaye ukweli atapata heshima!
Na ukweli haujalishi kausema paroko, askofu au imamu na sheikh!
Kwenye hili la bandari, maaskofu wapo katika ukweli na haki!