Waislamu jifunzeni kutenganisha dini (religion) na ya kidunia (secularism)

[emoji706][emoji706][emoji706]
 
Kwa misimamo kama hii, vijana wa Kiislam wataendelea kupambana sana wafike Ulaya na USA. Hata siku moja hawawezi tamani kwenda Saudia, Afghanistan au Iran
 
We jamaa umeongea pumba sana sasa unavyotaka dada zetu na mama zetu watembee bila ya nguo ,mwanamke kila kiungo chake ni uchi sasa uislam umemtaftia stara ili aweze kujihifadhi kutokana na madhila na makero kutoka kwa watu wenye matamanio ya haraka ,,na ndio maana ubakaji kutamani wake za watu yote yamekuja baada ya dada zetu kua na uhuru kwenye mavazi ,,,kwa taarifa yko hakuna mwanamme anaevutiwa na mwanamke asiejihifadhi rijali yoyote anapenda mwanamke mwenye staha na
 
Uislamu haumlazimishi mtu kufanya jambo flani,katika uislamu hakuna kulazimishana. Bali Ni wewe tu ukiona maamrisho ya uislamu Ni sahihi unayafuata....mnakosea Sana kusema kwamba watu wanalazimishwa!

Uislamu ni mfumo mzima wa Maisha ya mwanadamu uliyo sahihi....kwa yule anayeona unafaa na atakae ufuata kiusahihi lazima maisha yake hapa Duniani yatakwenda na kufanikiwa kwa chochote anachokitaka atakipata.

Unataka kulazimisha waislamu wafuata Mila ambazo sio sahihi kwao ili iweje?

Mavazi ya kiislamu yanakuuma Nini?
Kila mmoja afuate anachokiamini tusipangiane.
 
Ndugu Girita hii issue ya kulazimisha tunaishuhudia Kila siku huko uarabun ambalo ndo chimbuko la uislamu. Tunaishuhudia Kila siku watoto wa kike huko uarabun wanauliwa na kukimbia family zao kisa kutaka kubadili dini.

Nchi kama Iran tumeshuhudia mauaji makubwa Kwa sababu ya mavazi Kwa wanawake. Je hao huko hawaujui uislamu?
 
huujui uislam.

hiki unachojaribu kuhalalisha ni kama kutaka kusem mtu anawezakuwa muislam halafu akafanya yale anayoyataka au anayojisikia,hata kama ni kinyume na uislam.

moja ya malengo ya uislam ni muislam kuufata wenyewe unavyoagiza,na ili hili litimie kwa urahisi ni mpaka tawala iwe chini ya sheria za kiislam,yaani sharia law.

kuishi nje ya mfumo wa sharia ni kushindwa kwa uislam maana moja kwa moja ni matundu katika kuuharibu uislam na waislam wenyewe.muislam anapoishi na mtu asiye muislam akatii sheria zisizo za kiislam hayas sio malengo ya uislam,ndio sababu hata zenj huwa wanafoka sana wanapoona kuna dalili za kuwatoa kwenye tamaduni zao za kidini.

uislam usio wa kulazimisha sio uislam wa Quran ni uislam wa kisasa.
 
Reforms ni jambo zuri kwa Dini yoyote ile kwa mfano unakuta wasichana badala ya kuvaa vazi la kuogelea wao wanaogelea na hijabu na mabaibui na mara nyingi yanawatega wakati wa kuogelea na kusababisha vifo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…