Waislamu washinda kesi dhidi ya serikali na BAKWATA leo 27/06/2025

Waislamu washinda kesi dhidi ya serikali na BAKWATA leo 27/06/2025

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,132
Reaction score
64,416
KAMATI YA KUTETEA HAKI ZA WAISLAMU TANZANIA

WAISLAMU WASHINDA KESI DHIDI YA SERIKALI NA BAKWATA LEO 27/06/2025.

“Natupilia mbali mapingamizi yote kwa sababu hayana mashiko”.

Hayo ni maneno ya (mmoja wa majaji kati ya majaji watatu), jaji Mbagwa wakati akisoma hukumu ya mapingamizi leo yaliyowekwa na Serikali na BAKWATA katika kesi dhidi yao iliyofunguliwa na Waislamu 12.
IMG-20250627-WA0025.jpg

Novemba 06, 2024, wawakilishi 12, wa Waislamu Tanzania walikwenda Mahakama Kuu ya Tanzania kufungua shauri la uvunjaji wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dhidi ya Waislamu wa Tanzania.

Katika shauri hilo Na. 27603/2024 waislamu wanapinga Serikali kulazimisha Waislamu wote Tanzania (na mali zao), kuwa chini ya chombo walichokiteuwa wao (serikali), (Bakwata), na kuwanyima haki mbalimbali za msingi zikiwemo za kiimani na maendeleo.
Katika shauri hilo, walioshtakiwa ni mamlaka tatu za serikali na Taasisi mbili za kidini:

1. Mwanasheria Mkuu wa Serikali, (Attorney general of Tanzania - AG).
2. Msajili wa Jumuiya, Wizara ya Mambo ya Ndani, (The Registrar of Societies, Ministry of Home Affairs).

3. Kabidhi Wasii Mkuu wa Serikali, (Registration Insolvency and Trusteeship Agency - RITA).
4. Mwingine ni Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA).
5. Aidha Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania (BARAZA KUU), wameunganishwa kwa sababu ya kuleta ufanisi katika shauri hilo.

Akisoma hukumu hiyo jaji Mbagwa alitangulia kusoma mapingamizi yaliyowekwa na serikali na BAKWATA. Katika mapingamizi hayo la kwanza serikali na Bakwata walidai Waislamu walioleta mashtaka hayo dhidi yao hawakuonesha ni kwa jinsi gani wanavyo athiriwa na maamuzi amabyo hutolewa na RITA, Msajili wa Mambo Ndani na Bakwata.

Pia, soma: Kesi ya Kikatiba dhidi ya Serikali na BAKWATA imetajwa leo 26.11.2024, Mahakama Kuu

Katika pingamizi la pili walidai walioleta mashtaka hawakua na uhalali wa kufungua shauri la kikatiba mahakamni bali walipashwa kupeleka malalamiko yao kwa waziri wa Mambo ya Ndani na Waziri wa Katiba na Sheria.

Akisoma hukumu hiyo jaji alisema hati ya mashtaka ya waleta mashtaka inaonesha wanavyo athirika na maamuzi hayo. Katika pingamizi la pili jaji alisema hoja za kisheria zilizowasilishwa na walioleta mashtaka zinathibitisha haki ya kufunguliwa kwa shauri la kikatiba. “…kwa hoja hizo natupilia mbali mapingamizi yote (yaliyowekwa na upande wa serikali na Bakwata) kwa sababu hayana mashiko” alisema jaji.

Baada ya kusoma hukumu hiyo iliyomchukua takriban dakika 50, jaji liamua shauri la msingi (uvunjwaji wa katiba dhidi ya Waislamu), lianze mchakato wake tarehe 04/07/2025, tarehe 14/07/2025, na tarehe 17/07/2025, jopo la majaji watatu (wakiongozwa na jaji Mkwizu), litaanza kusikiliza shauri hilo.
Wawakilishi wa Waislamu katika shauri hilo ni:
1. Sheikh Prof. Hamza Mustafa Njozi (Morogoro).
2. Sheikh Ponda Issa Ponda (Dar es Salaam).
3. Bi. Riziki Shahari Mngwali (Dar es Salaam).
4. Ustadhi Bakari Bakari Shingo (Dar es Salaam).
5. Ustadhi Juma Husein Kilaghai (Dar es Salaam).
6. Ustadi Abdallah Mohammed Saidi (Dar es Salaam).
7. Ustadhi Ibrahim Hussein Sherally (Mwanza).
8. Ustadhi Mussa Rafiki Marua (Dar es Salaam).
9. Ustadhi Abubakar Ibrahim Mngodo (Dar es Salaam).
10. Ustadhi Mustafa Mohammed Abeid (Dar es Salaam).

Aidha wawakilishi wawili wamefariki duni ambao ni Ustadhi Twalib Muhammad Twalib (kutoka Dodoma), na Sheikh Ayoub Salim Muinge (kutoka Morogoro). Ustadhi Twalib alifariki dunia tarehe 31.12.2024, na Sheikh Ayoub alifariki dunia tarehe 18.2.2025.
 
Ungeandika wameshinda Pingamizi la awali la Kesi Yao.
Hawajashinda Kesi Bado. Ninawatakia mafanikio though.
 
Back
Top Bottom