Waislamu watatu wahukumiwa kifungo cha maisha nchini India kwa kuchinja ng'ombe

Wakusoma 12

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2017
Posts
5,503
Reaction score
15,858
Mahakama moja katika mji wa Gandhinagar, jimbo la Gujarat nchini India, imewahukumu Waislamu watatu kifungo cha maisha jela kwa kosa la kuchinja ng'ombe.

Katika hukumu yake, mahakama ilirejelea maandiko matakatifu ya dini ya Kihindu, yakiwemo Manu Smriti na Vedas, kueleza umuhimu wa ng'ombe katika imani hiyo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Press Trust of India, Naibu Waziri Mkuu wa jimbo la Gujarat, Harish Singhvi, amepongeza uamuzi huo akisema unatuma ujumbe ulio wazi kuwa sheria za jimbo hilo hazitawasamehe wanaochinja ng'ombe.

Katika hukumu iliyotolewa Jumatatu, Jaji B.R. Rajput aliwaamuru washtakiwa hao kulipa faini ya rupia 300,000 za India, pamoja na adhabu ya kifungo cha maisha.

Mahakama ilisema katika uamuzi wake kuwa iwapo watu wanaotuhumiwa kwa makosa hayo hawataadhibiwa kwa mujibu wa sheria, ng'ombe anayeheshimiwa kama mtakatifu katika imani ya Kihindu, anayejulikana kama “Gau Mata”, huenda akatoweka duniani kadiri muda unavyopita.

Katika uamuzi mwingine, mahakama hiyo pia iliwaadhibu washtakiwa kwa kifungo cha miaka 10 jela na faini ya rupia 100,000 kila mmoja, chini ya Sheria ya Ulinzi wa Wanyama ya Gujarat ya mwaka 1954.

Hata hivyo, adhabu hizo zitatekelezwa kwa wakati mmoja.

Chanzo cha habari BBC
 
Sema jamii nyingi za Asia zina lugha ngumu sana wanazoelewana wao kwa wao kwenye mambo yao.
Kama kuna wale mke na mume kule Mecca walihukumiwa kifo,nadhani wameshanyongwa... Sasa kuna yule aliyekuwa anasambaza zile picha na video wale mke na mme wakiwa wana kiss msikitini, jamaa ni muhindi ambae anafanya kazi huko Saudia naye yupo jela hadi leo...

Hao wanajuana vyema.. 🤣 🤣
 
1000077065.jpg
 
muslims wana chokochoko sana, hakuna anayeweza ku-coexist na muslims, india kuna Christians wengi tu ukifika Goa state wanaishi (majority Christains) na wahindu vizuri kwa amani na respect, lkn muslms vs hindu ni vita, kwa nini? ...
Wenyewe kwa wenyewe wanatosha kukichafua. Pakistan ni waislamu wote ila Sunni na Shia wanauwana Kila siku.
 
Wahindu wanaabudu ng’ombe kama mungu
Ng'ombe nchini India ni mnyama anayeachwa hata barabarani wenyewe wakimkuta wanainama kama ishara ya kumuabudu

Zamani UK pia ilikuwa huruhusiwi kuchinja hata kuku mpaka upate kibali cha RSPCA, Royal Society for Prevention of Cruelty to Animals
 
Katika uamuzi mwingine, mahakama hiyo pia iliwaadhibu washtakiwa kwa kifungo cha miaka 10 jela na faini ya rupia 100,000 kila mmoja, chini ya Sheria ya Ulinzi wa Wanyama ya Gujarat ya mwaka 1954.

Hata hivyo, adhabu hizo zitatekelezwa kwa wakati mmoja.
Hapo ndio Ng'ombe wa Tanzania wanapoanza kuona bora wangezaliwa India tu ili wasiliwe nyama.
 
Katika uamuzi mwingine, mahakama hiyo pia iliwaadhibu washtakiwa kwa kifungo cha miaka 10 jela na faini ya rupia 100,000 kila mmoja, chini ya Sheria ya Ulinzi wa Wanyama ya Gujarat ya mwaka 1954.
Implication yake ni nini kwa hukumu ya awali
 
🤣 🤣 🤣 🤣
Hii dunia ina vituko..

Si wangechinja hata mbuzi... kama sheria za hilo jimbo zinasema wasichinje ng'ombe basi wamejitakia...
Ubishi usio na maana umewapoteza hii ni kujiona bora na watakatifu kuliko wengine..
Ukiona mtu anaabudu sisimizi muheshimu na sisimizi wake pita hivi..🚶‍♂️
 
Back
Top Bottom