Waislamu wazindua program 2010

Ni bora wawe hawana Diploma kuliko kuwa na zile za St.. St,, ambazo zinakubeba toka Certificate mpaka PhD.



au zile za islamic, islamic .. islamic....! zinazomtoa mtu mwenye Phd mpaka certificate ya madrassa. ! HAHAHAHAHAHAHAH....!

THE LATE MO.
 
Tujiulize kati ya hao masheikh wanaopigania haki ya Waislam ni wangapi hata wana diploma kujua haki ya kataba ya nchi kutobadilishwa?

Usikashifu dini yetu wengi wamesoma wana certificate za MADRASA na ni walimu wazuri wa MADRASA
 
jamani jamani huu udini utatupeleka wapi? sifa za kiongozi bora ni kuwa muumini wa dini fulani tu na si dini nyingine? mimi nafikiri sifa kubwa ya kiongozi ni uzalendo. Tukianza kuchagua watu kwa misingi ya dini tutafika kweli?
 
Wakatoliki itawaudhi hiyo program. lakini nchi ni ya wote . You can fool some people some time But ou can't all the people all the time.

Hafif....fikra finyu sana....kwanini huisi wakatoliki ndo watakaochefuka na hii programu ya waislamu?Madhehebu mengine ya kikistru unayaweka wapi?Dini nyingine zikiwemo za asili zinafurahi hilo?Fikiri kwanza...acha hisia hisia...
 

Barubaru,
Hapa tatizo langu si CHADEMA. Ila kuingiza habari za dini kwenye kila mjadala. Kama ni dini kuna kitengo chake.

Kama mtu akija na kuichambua CHADEMA vizuri basi mie hainipi wasiwasi.

Kumbuka mie ni MPINZANI mkubwa wa Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Chadema mwaka huu. Nina imani Zitto alifanya makosa kugombea na Mbowe alifanya makosa kuanza siasa chafu kwa Zitto. Kama mambo yangelienda kwa uwazi na ukweli, hii aibu isingelikuwepo.
 
Mhhhh! wewe ukiacha kuingiza udini wako na sisi tutaacha lakini wewe unafikiri ukifanya insult kwa uislamu wenye dini zetu tutanyamaza..ikitaka kuheshimiwa jiheshimu
 
1. Nashukuru kwa majibu yako ndugu, lakini sijamtisha mtu yeyote zaidi ya kueleza ukweli wa mambo! Sijui kama umejiuliza kwamba shura ya maimamu inapotafuta kiongozi wa kitaifa kwenye misikiti pekee, huyo kiongozi atawaongoza akina nani?
2. Na wanaposema kwamba wanataka kiongozi ambaye hatahusisha uislamu na ugaidi, huyo kiongozi hatakuwa mwadilifu, in the first place, kwa sababu hatakuwa anasema ukweli, atakuwa MNAFIKI mkubwa! Soma maneno ya Quran kuhusu UGAIDI: "Mola wako Mlezi alipo wafunulia Malaika: Hakika Mimi ni pamoja nanyi, basi watieni nguvu walio amini. Nitatia woga katika nyoyo za walio kufuru. Basi wapigeni juu ya shingo na wapigeni kwenye kila ncha za vidole." (Quran 8:12).
3. Sasa hapa mimi nawatisha watu au marehemu Muhammad ndio anayetishia uhai wa watu wasio na hatia kupitia Quran? Kuwa na huruma na nafsi yako ambayo inakutaka useme ukweli siku zote!
 

Hoja yako imekaa KIDINI na ume-quote quran "out of context" yaani kutafsiri quran unatakiwa usome huo ujumbe (sura) in a "holistic manner" i.e. umetolewa wapi? kwa ajili ya nani? na wakati gani? ok. kwahiyo swala lako la maradhi yako ya udini wako sintajibu ok au weka kule kwenye dini ntakusaidia..
Kwakuwa ulikuwa na hoja moja tu yenye kuhitaji ufafanuzi

1. Kiongozi wa kitaifa kutafutwa misikitini pekee kiongozi huyo ataongoza kina nani? ...Hiyo si kweli shura inapeleka mwongozo kwa watanzania wote ni mikutano yake inafanyika kwenye public places all over the country...kwa hiyo ni kwa wananchi wote unaweza kuhudhuria ili uweze kupata historia sahihi ya nchi na matatizo ya msingi ya nchi hii nzuri...unlike waraka ambao husambazwa na kufundishwa kwenye jumuiya za kikatoliki na kufundishwa na mapadre huo ndio umekaa kibaguzi si kitaifa
 

1. Nilisema hii ni biashara na wewe kwa kuununua umedhihirisha. Hao wakatoliki wanaowakera hawakuuza waraka wao. Huu ni mpango wa ulaji wa watu wachache wanaojifanya ndiyo wawakilishi wa waislamu wote.
2. Kulikuwa na haja gani kutuambia kuwa simu unayoitumia ni ya dereva wako? Au ndiyo kutudhihirishia bado ile dhana ya utwana?
3.Nitakutakaje usifie Chadema au ukatoliki wakati mimi mwenyewe sijawahi kufanya hivyo? Wamisheni wote si wakatoliki kama ambavyo pengine unadhani.
4. Naam, Tumaini ana haki ya kuchangia kama mtu mwingine. Na vivyo hivyo ana haki ya kujibiwa kadri anavyoileta hoja yake.
5. Hoja yangu ni kuwa hii ni programu jina tu. Ni mpango ambao umeletwa kuendelea kuwagawa wamisheni na waislamu. Wakati huu unatamka wazi kuwa mgombea achaguliwe kutokana na ahadi zake kwa waislamu, huo wa wenzenu haukufanya hivyo. Hatari ya kuweka litmus test kama hii ni kuwa watajitokeza walaghai au wachochezi watakaoitumia kwa ajili ya ajenda zao.

Amandla.......
 

Kwa taarifa yako waliopinga waraka wa wakatoliki ni BAKWATA ambayo si waislam wote wanaifuata. Kina Ponda wamekuwa against BAKWATA kwa miaka mingi.
 
Wanasema tatizo kubwa ni udini na wana imply kuwa viongozi wakristo ndiyo mafisadi....Soma kwa makini...Ningependelea kuona mwongozo wa kitaifa zaidi.

Kusema kuna udini hakuna uhusiano na implication kwamba viongozi wakristo ndio mafisadi.

Ina maana mkristo akisema kuna udini ina maana anasema Waislamu ndio mafisadi? I dont think so.

Kama mtu anaamini mafisadi wengi ni waialamu ama wakristo ana uhuru wa kusema waziwazi. Kusema kuna tatizo la udini haiwezi kuwa na maana kwamba wasio dini ya msemaji ndio mafisadi.
 
Hii progamme ina agenda nyingi zilizojificha na kuna wanaofuata mkumbo tu bila kujua hasa ndani yaliyomo ni nini.

Kuna the so called wapigania uhuru wenye grievances za miaka mingi walioona hawakutendewa na kupewa heshima ya kutosha hasa na utawala wa awamu ya kwanza.Wameandika vitabu weeee wakaona havijawaletea matunda..sasa wanakuja na program.

Ngoja tuone hii nchi itafika wapi kwa ubiinafsi wa watu wachache wenye kutumia majority innocent ignorant poor and the down trodden!
 
Tunawatakia mafanikio mema
 
Asiyejua maana usimfunze maana. Tuacheni na program yetu ya mwongozo wa 2010.

Kwani kutoa mwongozo ni kosa kisheria?
Kutoa program ya mwongozo ni kosa kisheria?
Mbona DCI au hata mwanasheria mkuu hajasem lolote?

Sasa nyie wakristo kinawauma nini?
 

Kwani nyinyi mlipoulalamikia waraka wa wakatoliki ilikuwa ni kwa sababu wao walivunja sheria?

Sasa kwa nini mliileta hii habari humu kama hamkutaka wamisheni wachangie?

Kitu tuchoogopa wengine ni kuwa hicho mnachotaka kiwe kikitokea hatutawaona mstari wa mbele. Kazi hiyo mtawaachia hao wafuasi wenu ambao wengi hawana nafasi nzuri kama za kwenu.

Amandla......
 
Ni bora wawe hawana Diploma kuliko kuwa na zile za St.. St,, ambazo zinakubeba toka Certificate mpaka PhD.
kama ya Slaa. mimi siku zote humwita Slaa kwangu sio DR.
PIA JITAHIDI UPATE UJUMBE WA IJUMAA WA OKTOBA 24 KUTOKA MSIKITI WA IDRISA WENYE KICHWA CHA HABARI KAULI ZA SLAA NA ASKOFU KILAINI HAZINA NIA NJEMA NA WAISLAM.
AU SOMA GAZETI LA JAMBO LEO TOLEO 111 LA OKTOBA 19,2009 KUONESHA NIA MBAYA YA SLAA
 

Ubinafsi na udini ulianzia kwenye waraka wa Maaskofu tusije kusahau "source" tukaanza kurukia matokeo..source ni waraka!

Watu wengi tulishauri serikali iwakemee wakristo na udini wao pamaoja na agenda ya ubinafsi na ajenda zao zingine za siri wakakataa na wakristo wakaja juu kuutetea..

Wacha kulalamika usisahau source, niliwahi kusema nchi hii kutakuwa na vyama viwili "christian party ans islamic party at the end of the day..naamini tutafika huko wananchi watachagua kwa mrengo huo good move..
 

Arm-chair General mwingine!

Amandla......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…