Waislamu wazindua program 2010



Huna Lolote Tumaini...Mnajichanganya tu! Yani hiyo report huwezi kuilinganisha na ile ya katoliki hata tone, yao ilikua ya kitaalam na kisomi zaidi, yani ilikua ngumu kujua wanamtaka mtu wa dini yao...it was so general tofauti na nyie yani ipo live and direct kwamba mnataka kiongozi wa dini yenu, mi nawaambia ubaguzi utawamaliza na hali ya kuendeleza vinyongo ambazo nyie ndio mlitafsiri kipotofu hakutawafikisha popote.

Kitendo cha kusema "awe mtu ambae atachunguza mauaji kwenye maandamano yale yakusema YESU si mungu" that means hamjatambua kwamba mlifanya kosa kuzungumzia dini ya watu wengine, yani mnaona mlichofanya ni haki. sasa tutawaaminije itapotokea pande nyingine(eg christians) watapofanyiwa uonevu, kutukanwa, kuchomewa makanisa yao na daily insults ambazo huwa tunazisikia, je huyo kiongozi mnaemtaka atasimama wapi? kwa maelezo mafupi tu inaonyesha dini nyingine hazitakua na haki...hata huyo kiongozi wenu amesema muongozo unafanya kazi, eti ukiangalia 90% ya waliochaguliwa huko kusini ni watu walioushika vizuri muongozo, tht prove huo muongozo unaonekana kufanya kazi kwa sababu waliochaguliwa ni waislam....

GOD PLS FORGIVE US BECAUSE WE DONT KNOW WHAT WE ARE DOING!
 

Tuusome marangapi barubaru....haiitaji digrii kujua mlichoandika huko ni ubaguzi...af kitendo cha kulenga wakristo wakati nchi hii inawatu wa dini zaidi ya hizo mbili siwaelewi kabisa.
 
kama kuna muislamu anaepuuza maimamu wa kiislamu basi huyo amepotea,kwa kipimo cha matashi ya nafsi yako ndo unamuona kaelimika!
 
Nafikiri issue hapa ni kwamba kabla dola (dola yetu haina dini) haijaingilia kati jambo hili, wasomi walioko huko kwenye vyombo vyetu vya dini ama imani mbalimbali zilizopo nchini wakae chini na kujadili ni kwa namna gani hii miongozo inayoibuka kutoka kila kundi la dini inaweza ikawa harmonized to lead Tanzanians (categorically their worshippers) to a right path of electing their national leader(s) who in turn (national leaders) will serve for national interests as shall be opposed to some group interests which might be the current fuel for such prolifirating miongozo.

Ukiwa na mtazamo mpana zaidi utabaini kuwa ipo haja ya serikali hata watanzania kwa ujumla kuwa makini zaidi na miongozo hii kwani usijeshangaa hapo badae dhana ikapanuka zaidi hata rais itaepata madaraka kwa uwiano wa karibu zaidi na mantiki ya muongozo wa kikundi fulani cha dini akapewa pia mwongozo wa kupata mawaziri na watendaji wengine wa serikali. Hapa itapendeza zaidi kama hayo yametendeka kwa maslahi ya taifa na wala si kwa kuzingatia UDINI ambao kwa namna moja ama nyingine unaonekana kuanza kulalamikiwa na baadhi ya wananchi ndani ya serikali yetu. Hofu yangu nikwamba miongozo hiyo isijekuwa ni vivuli vya huo UDINI.

Lakini pia panaweza kutokea kundi fulani la dini kuunga mkono mwongozo uliotolewa na kundi jingine kama siyo kutaka marekebisho katika mwongozo huo. Hapa tutajikuta badae tunzaanzisha Ofisi ya Msajili wa Miongozo ya Dini Mbalimbali kama ilivyo kwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

Hata hivyo suluhu iliyokubwa zaidi kwa matatizo kama haya (yanayopelekea kuzaliwa miongozo)itakuwa ni kwa wale wenzetu waingiao madrakani kutenda kazi zao ama kufanya teuzi zao kwa kuzingatia maslahi ya taifa badala ya kuweka mbele viaina fulani vya upendeleo kwa makundi fulani ya dini, kabila ama ukanda. Tatizo ni je, viongozi wa aina hiyo tunao? au the beuatyful ones are not yet born? or the beautiful ones will be born but also might become poluted by, among other factors, miongozo?
 
Hivi inawezekana mzaramo kuwa mbunge kule Tarime, au mmakonde kuwa mbunge wa Biharamulo.

kama sasa mambo hayo hakuna basi ndio tunakwenda another stage.

Dhambi ya ubaguzi imeanza kutusurubu.
 
Wanajamvi mtanisamehe si mchango kwenye hii thread kwasababu haisaidii kujenga taifa letu bali kulibomoa kwa faida watu wachache wenye uelewa duni.
 
Hivi inawezekana mzaramo kuwa mbunge kule Tarime, au mmakonde kuwa mbunge wa Biharamulo.

kama sasa mambo hayo hakuna basi ndio tunakwenda another stage.

Dhambi ya ubaguzi imeanza kutusurubu.

Kwa hiyo kama tulivyoanza na shule za kidini basi unataka tufike mahali ambapo tugawane mitaa? Tuwe na maeneo tofauti ya waislamu, wakristu, wasio na dini, wahindu, mabuddha, n.k.? Halafu baadae hayo hayo maeneo yagawanye kwa ajili ya wasunni, washia, mabohora, wakatoliki, waluteri, waanglikana, majehova n.k? Patakalika kweli?

Amandla....
 
Mhhhh! wewe ukiacha kuingiza udini wako na sisi tutaacha lakini wewe unafikiri ukifanya insult kwa uislamu wenye dini zetu tutanyamaza..ikitaka kuheshimiwa jiheshimu
"YOU HIT ME ONCE, I HIT YOU TWICE" ............. Huu ndiyo msemo wa watu wenye kuishi kwa visasi............. Yeye saa zote anawaza JINO KWA JINO........... ngangari kwa ngunguri........... Yaani kwake hana muda wa kusamehe......... So long as mtu kamuanza basi atalipiza kwa kiasi kikubwa sana... simply because ameanzwa.............
 
Hii hoja naona inachangiwa sana na kuungwa mkono na watu walewale..... Kinachonishangaza ni kuwa watu hao hawaishi Tanzania, wao kazi yao ni kutupandikiza chuki na baada ya hapo nina uhakika hawataonekana tena wakati tumeshalikoroga.......... Kwa maana hiyo watatuacha tunalinywa wenyewe. Mtu kama Barubaru, kaja Tanzania kwa siku saba na kurudi huko anakoishi. Hivi unategemea mtu kama huyo tukijiingiza kwenye vita ya kidini atakuja tena..???? Nionacho ni kuwa atabaki huko aliko, na sana sana anatoa misaada ya mabomu kwa watakaokuwa upande wake, lakini distantly.

Tuacheni tunaojuwa hali halisi ya TZ tuichangie hoja hii. Hii habari ya kuifananisha TZ na nchi zinazoongozwa kiislamu muiache kabisa. Hatutumii sharia....bali sheria.

Ni wazi kabisa kwamba kinachoelezwa kwenye hiyo program ni kumchagua kiongozi ambaye ni MUISLAM anayebisha huyo hajaielewa hiyo program na ninamshauri akaisome tena.....

NINA UHAKIKA KUWA PAMOJA NA KWAMBA KINGUNGE ALIUPINGA WARAKA WA WAKATOLIKI, LAKINI AKIGOMBEA NAFASI YOYOTE WAISLAM HAWATAMPA KURA............. Sababu ni kuwa yeye si MUISLAM
 
 

Iko kazi kweli!

Unaji-contradict halafu unasema uongo bila aibu? Wapi katika waraka wa maaskofu waliposema kiongozi wao awe mkatoliki?

Amandla....
 

Kama wao si wanafiki, wasingepinga waraka wa Wakatoliki. Kimsingi, ukisoma nyaraka zote mbili utaona mmoja unahusu maslahi ya Watz wote na mwingine maslahi ya Waislamu. Na huu wa maslahi ya Waislamu ndio unaopigiwa debe kuwa ni sahihi! Hivi kweli Watanzania tuna akili timamu?
 

jamani,mbona kimya sana ndugu zangu........afu nadhani Sheikh Yahya anapingana na maoini yenu, tafadfhali tunaomba msimamo wenu pia,kama aliyotuambia Sheikh Yahya ni kweli..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…