Waisraeli kuua watoto kule Gaza na kuondoa matibabu bure kwa watoto chini ya miaka 5 siyo kitu sawa

Waisraeli kuua watoto kule Gaza na kuondoa matibabu bure kwa watoto chini ya miaka 5 siyo kitu sawa

Nsanzagee

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2023
Posts
2,209
Reaction score
4,769
Iko wapi huruma ya serikali kwa watoto kutoa matibabu bule kwa walio chini ya miaka mitano

Mbona tunawalaani wazayuni kushambulia na kuuwa watoto wa Gaza na huku tukiona sawa kutokuweka na kuendeleza sera ya matibabu bule kwa watoto wetu walio chini ya miaka mitano?

Panatofauti gani kati ya wazayuni wanaouwa watoto wa Gaza bila hatia na huku tukiondoa matibabu ya bule kwa watoto wetu?

Kipindi cha nyuma serikali ilikuwa na kauli mbiu na tena tulikuwa tukisikia viongozi wetu wakituhamasisha tuzae sana, kwani huduma za afya ya mjamzito na mtoto aliyechini ya miaka mutano, serikali itagharamia matibabu yake bule!

Je pesa za kugharamia matibabu hayo pesa zake ndio zimehamishiwa kwenye kulipa magoli ya simba na yanga inapocheza na wageni?

Jamani, mbona tunaingia kwenya laana?

Naishauri Wizara ya Afya, ilione hili, ni rahisi kusema kuzaa ni starehe, lakini hata anayesema naye alizaliwa!
 
Back
Top Bottom