Waitara aanza kuongea lugha ya watu

Waitara aanza kuongea lugha ya watu

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni.

Hizi ndiyo lugha ambazo serikali dhwalimu huzielewa.

Bila lugha hizi tutasubiri sana kwa madai yetu yote.

Kwani imekuwaje hatimaye Ruto na Gachagua kuongea lugha za kiutu kama hizi?

Viva wapambanaji wote viva!
 
Nina wasiwasi Waitara anaweza kufukuzwa uanachama wake wa CCM na hivyo kupoteza ubunge wake wa kubambia!
 
Nina wasiwasi Waitara anaweza kufukuzwa uanachama wake wa CCM na hivyo kupoteza ubunge wake wa kubambia!

Si walisema kuvunjika kwa koleo mjomba? Wengine wakasema ni heri kufa ukipigania haki kuliko kufa kwa malaria.
 
Nina wasiwasi Waitara anaweza kufukuzwa uanachama wake wa CCM na hivyo kupoteza ubunge wake wa kubambia!
Hana Cha kupoteza hapo maana 2025 chama kinarudi kwa wenyewe hawawezi mpitisha kura za maoni. So kaona afe na wananchi Ili akifukuzwa basi akienda Chadema au ACT alinde kura zake kuelekea 2025. It's a nice strategy Ili kumzidi kete Heche ila nachoona watagawa kura tu na Jimbo litabaki CCM!! Hapa wapinzani wawe makini sama yasijirudie ya 2010 tukagawana kura Tarime ikaenda CCM.
 
Nimeisikiliza hotuba yake na kukumbuka alipokuwa Rais wangu wa Serikali ya Wanafunzi UDSM almaarufu kama DARUSO 2005/2006. Ameongea kwa kujiamini sana. Ataweza anachokisema?
 
Michezo ya siasa imeanza, baada ya juzi kuongea huku akilia ili awaoneshe wapiga kura wake anaonewa, hapewi ushirikiano na idara nyingine za serikali, sasa ndio ameamua liwalo na liwe..
 
Michezo ya siasa imeanza, baada ya juzi kuongea huku akilia ili awaoneshe wapiga kura wake anaonewa, hapewi ushirikiano na idara nyingine za serikali, sasa ndio ameamua liwalo na liwe..

Kasema alikuwa anatoa sumu mwilini. Ila la msingi kujifunza lugha ya watu.
 
Huyu chapombe ameshajua kuwa mwisho wa ajira ya siasa kwake ni 2025 ndiyo maana ameamua kuwa roporopo liwawalo naliwe

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
Hakuna mwenye hatimiliki ya jimbo lolote hapa Tanganyika hata hao unadhania majimbo niyao,waweza kupoteza,au kufariki kabla ya mda,ni Mungu tu ndiye anayejua maisha ya mwanadamu, wewe baki tu chuki zako,kisa aliama Chadema.
 
Back
Top Bottom