Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Leo mbunge Waitara amewashukia naibu Waziri maliasili na Waziri wa ardhi na kuwalaumu kumtegea mabomu njiani. Waitara amesema wahusika wameenda jimboni kwake na kudai wamemshirikisha eneo la mipaka na kuwahamisha watu bonde la mto Msimbazi.
Waitara amewataka mawaziri wa Maliasili na Ardhi waende mkoa wa Mara kwani hawawezi kwenda peke yao na kuwapa wananchi wake taarifa za uongo, Waitara amesisitiza watagombana.
Mwisho amesema amewekewa bomu ambalo hatakubali kulipuka peke yake bali watalipuka wote.
Kuhusu ripoti ya Jaffo, amesema walishaandikiana sana na mgodi lakini ripoti ya Jaffo imeharibu hali ya hewa.
Akimjibu, Naibu spika wa Bunge, Mussa Zungu amenena
Mussa Zungu: Asante mheshimiwa Waitara lakini wewe ulikuwa naibu Waziri wa mazingira na ulikuwa unakwenda kwenye migodi wala wabunge wenzio huwaambii, na umemaliza ukaenda huko uchukuzi, unaenda huko unakagua lakini huwaambii lakini hoja yako ni ya msingi.
Kwa mawaziri mkienda huko muambizane lakini habari ndio hiyo.