Waitara: Mambo yalibadilika CHADEMA figisu, fitina na matumizi mabaya ya fedha

Waitara: Mambo yalibadilika CHADEMA figisu, fitina na matumizi mabaya ya fedha

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Akizungumza katika mahojiano na M & S Podcast yaliyorushwa Agosti 12, 2026, Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini, Mwita Waitara, amefunguka kuhusu mambo yaliyokuwa yakiendelea ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), akidai mambo yalibadilika chama kikajaa fitina, figisu, usaliti na matumizi mabaya ya fedha.

"Kwa hiyo tumeenda baadaye mambo yamebadilika ndani ya CHADEMA huku. Mambo mengi, fitina fitina, figisu figisu nyingi. Nikaona sasa siasa mimi nilikuwa nataka nifanye siasa ya upinzani halisi, ni kama sasa nafanya maigizo. Mambo yaliyokuwa yakitokea CCM unaona yanafanyika tena CHADEMA. Mambo ya kupendeleana, marafiki, ushoga ushoga mwingi, matumizi mabaya ya fedha na kusema fedha za kwa kificho, hakuna uwazi (transparency). Tumetenga hata akaunti maalum zile hazionekani..."

 
Alipokuwa CCM mbona hatukusikia hizi kelele za no transparency? Huku ni kutafuta kiki tu.
 
Back
Top Bottom