nokwenumuya
JF-Expert Member
- Jun 29, 2019
- 820
- 2,896
WAITARA, NYAMHANGA WAIGAWA TARIME KWA MASLAHI YAO BINAFSI KISIASA
Mchakato huo wa ugawaji huanzia ngazi za chini, katika Wilaya/Halmashauri husika, kisha Mkoani na baadae mapendekezo hupelekwa TAMISEMI kwa ajili ya kuyathibitisha au kushauri panapowezekana.
Wilaya ya Tarime ina majimbo mawili, Jimbo la Tarime Mjini, na Jimbo la Tarime Vijijini. Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Wilaya ya Tarime iligawanywa katika Halmashauri mbili, ambapo Tarime Mjini ilipewa kata 8, na vijijini kata 26. Baadae ikaonekana Halmashauri ya Tarime Mjini kwanza imetengewa eneo dogo, pili kuna Wananchi kufuata huduma Nyamwaga (Makao Makuu ya Tarime Vijijini) ikaonekana ni mbali sana, na tatu haina vyanzo vya mapato, hivyo ikaonekana ni busara ugawaji wa kata ufanyike upya ili kuondoa Changamoto hizo zilizojitokeza baada ya ugawaji ambao haukuwa sahihi.
Mchakato ulianza na mwaka jana 2019 Halmashauri zote za Wilaya ya Tarime zikapendekeza kuwa kata 8 ziongezeke katika Halmashauri ya Tarime Mjini, ambazo ni Komaswa, Manga, Kiyole, Bumera, Mwema, Susuni, Sirari, na Regicheli. Halmashauri hizi zote mbili zinaongozwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Mapendekezo haya ambayo hayakushirikisha wananchi wa kata husika yaliibua malalamiko toka Tarafa ya INCHUGU, kwa sababu wananchi wa Tarafa hiyo hawakutaka igawanywe, walitaka ni kheri tarafa na kata zote ziende katika jimbo moja kuliko kugawanywa huku na huku, jambo ambalo walisema kimila halikubaliki, na walilalamikia hatua hiyo ya CHADEMA kutoa mapendekezo hayo bila kuwashirikisha wananchi na hasa WAZEE wa MILA.
Malalamiko hayo waliyapeleka TAMISEMI ili yafanyiwe kazi, wakiamini kuwa mapendekezo yao yatafanyiwa kazi ukizingatia kuwa Katibu Mkuu wa TAMISEMI, Injinia Joseph Nyamhanga, ni mtu wa Tarime hivyo anajua juu ya mila na ubaya wa kuigawa INCHUGU. Pili walimshirikisha Naibu Waziri, Mh. Mwita Waitara juu ya hilo. Waliamini uwepo wa hao unaweza kuwasaidia kwani wote bahati nzuri ni watu wa Tarime na hayo malalamiko wanayafahamu vizuri. Na hata wasingekuwa watu wa Tarime bado wangewaelimisha juu ya mila za kuigawanya INCHUGU.
Kinyume na matarajio ya kilio cha Wazee wa Tarafa ya INCHUGU, wawili hao wamekaa na kukubaliana kwenda kinyume kidogo na mapendekezo ya Mabaraza ya Madiwani baada ya kung’amua kuwa kama mapendekezo hayo yataachwa jinsi yalivyo yatawagonganisha wao katika uchaguzi Mkuu wa 2020, maana wote wana dhamira ya kwenda kugombea Ubunge katika majimbo hayo.
Mh. Mwita WAITARA, Naibu Waziri TAMISEMI, na INJINIA Joseph NYAMHANGA, Katibu Mkuu TAMISEMI wote walikuwa na dhamira ya kugombea Jimbo la Tarime Vijijini katika uchaguzi wa mwaka huu, 2020. Kwa kuwa wote wako TAMISEMI waliamua kwa kauli moja ni bora mmoja aende Tarime Mjini na mwingine aende Tarime Vijijini. Katika makubaliano hayo walikubaliana kuwa Mh. Waitara abaki Tarime Vijijini, na Injinia NYAMHANGA aende Tarime Mjini.
Changamoto ambayo waliiona kwa pamoja ni kuwa kata ya BINAGI, ambako ndipo anapotoka Injinia NYAMHANGA imependekezwa iendelee kubaki jimbo la Tarime Vijijini, hivyo itampa yeye changamoto kugombea mjini pasipo kuwepo na kata ambayo ndiko chimbuko la familia yake, hivyo wakaamua kuwa kwa namna yoyote lazima kata hiyo irudi jimbo la Tarime Mjini, bila kuzingatia mapendekezo wala ramani ya hiyo kata ilivyokaa.
Hivyo kinyume na taratibu za ugawaji, ambapo Katibu Mkuu huwa mtu wa mwisho katika mchakato huo, aliamua kuomba nyaraka za mapendekezo ya ugawaji wa Tarime, na kuamua kulifanyia kazi moja kwa moja bila kuwashirikisha watu wa chini yake, na akachora ramani mpya na kuiingiza kata ya Binagi katika jimbo la Tarime Mjini, ili aweze kuwa na nguvu katika kugombea jimbo hilo.
Jambo baya walilofanya ni kutoangalia maslahi ya umma wa wana INCHUGU, ambao walipendekeza tarafa hiyo isigawanywe bali iende ama Tarime Mjini yote, au Tarime Vijijini. Jambo ambalo sio tu kupuuza Wazee wa MILA wa tarafa hiyo, bali kuendeleza tabia waliyofanya madiwani wa CHADEMA wa kutoona umuhimu wa kuwashirikisha WAZEE katika mchakato wa ugawaji mpya wa mipaka ya kata na Jimbo hilo.
Baada ya kukamilisha mipango yao, wakakubaliana Mh. Waitara afanye ziara mwezi huu wa pili katika Wilaya ya Tarime, kwamba awakusanye wenyeviti wa vijiji na mitaa, atoe semina ya uongozi kama Naibu Waziri TAMISEMI ili kuwajengea uwezo katika ufanyaji wao wa kazi. Lakini ziara hiyo malengo yao ni kuendelea kuwa karibu na hao viongozi wa ngazi za chini ili kuwasaidia kufanikisha malengo yao(maana si mkakati wa nchi nzima), hivyo muda si mrefu mtamuona akienda Tarime kufanya ziara hiyo, labda abadilishe mbinu baada ya kuweka mipango yao wazi, lakini hadi sasa huo ndio mpango kazi ulio mezani kwao.
Baada ya kupata taarifa hii kwa mtu wa ndani wa Mh. Waitara, ambaye ni mkazi wa INCHUGU aishie Dar es Salaam, ambaye alijaribu kuwashauri kinyume basi nikaona bora kuiweka taarifa hii wazi huenda ikasaidia katika mchakato huo kuangaliwa upya, kwani kwa hali ilivyo hivi sasa Katibu Mkuu TAMISEMI, na Naibu Waziri tayari wamekwishazika mapendekezo ya wale Wazee wa INCHUGU ambao kimsingi wanawakilisha jamii nzima ya wakazi wa TARAFA hiyo.
Ni Mimi,
Venance Marwa
Mwana TARIME.
NOKWE AGHONGWE.
- Ni Naibu Waziri na Katibu Mkuu Wizara ya TAMISEMI.
- Dhamira ni kuwarahisishia mipango yao kugombea majimbo ya Tarime Mjini na Vijijini.
- Wagawanya Kata wakipuuza mapendekezo ya Mabaraza ya Madiwani.
- Washikilia msimamo wa kuigawa tarafa ya INCHUGU ulioasisiwa na CHADEMA.