Wajameni!! Tatizo la Stars ni Kocha pamoja na Mapro!!

Naifahamu Carbo Verdè tangu wewe hujaja mjini Kutoka bush.....
 
Yani una taka kina ajibu ma kichuya wakacheze na kina ricardo na nuno? Hivi huijui cape verde ee? Ulitaka kumfunga cape verde kwenye uwanja wake wa nyumbani? Mimi nita fadhaika kama tuta shindwa kumfunga cape verde apa uwanja wa taifa io jumanne
Acha Soka la vijiweni kijana....unawa'overrate sana Cape Verde
 
Tulishawahi kupangwa nao kabla nadhani ilikuwa around 2009-10 tuliwafunga Dar 3-0 na kutoa nao sare ya 1-1 kwao mfungaji wetu kule alikuwa Kiggi Makassy
 
Acha Soka la vijiweni kijana....unawa'overrate sana Cape Verde
Ni kinini kina kufanya uweze ku underrate cape verde? Timu ya 63 kwa ubora duniani ipo nyumbani dhidi ya team 140 kwa ubora duniani... so una expect nn apo mzee? Apo ni sawa sawa na somalia ije uwanja wa taifa then eti mashabiki wa somalia wategemeee kutufunga sisi katika uwanja wa taifa
 
Huwa sipotezi hata sekunde moja kuangalia mechi yoyote inayo cheza Taifa stars. Ni afadhali huo muda nitumie kupigia puli tu!
 
Kama mpira tutaangalia viwango vya FiFa basi Ujerumani angetetea ubingwa wake....labda unaweza kuniambia kwanini Argentina alifungwa 3-0 na Croatia kwenye kombe la dunia.....je hapo hoja yako ya viwango vya FIFA si itakuwa haina mashiko sana!!!
 
Viwango vya fifa uwa vina onesha taswira na ndio maana sisi wa 140 tume fungwa na wa 63.. tena away
Kama mpira tutaangalia viwango vya FiFa basi Ujerumani angetetea ubingwa wake....labda unaweza kuniambia kwanini Argentina alifungwa 3-0 na Croatia kwenye kombe la dunia.....je hapo hoja yako ya viwango vya FIFA si itakuwa haina mashiko sana!!!
 
Tulichagua wenyewe kufungwa.makosa yameanzia kwa kocha kushindwa kupanga kikosi yakaenda hadi kwa wachezaji kujua wajipangeje kimajukumu uwanjani.Pamoja na kwamba cape verde wako vizuri ila bado mpira wao niwakawaida nasisi tungecheza vizuri tungepunguza idadi ya magoli au nasisi tusingetoka kapa.
 
Sijaona nafasi ya Ulimwengu pale T stars yaani inaonekana kama vile hawa wachezaji wanateuliwa bungeni na teuzi zao haziwezi kutenguliwa.

Wachezaji wale wale kila siku kwanini tusitafute wachezaji wengine tuachane na hawa waliokubuhu akili.
 
Kocha! kocha! Kocha!....aliingia na mawazo ya kulazimasha sare kwa kujaza mabeki
 
Sijaona nafasi ya Ulimwengu pale T stars yaani inaonekana kama vile hawa wachezaji wanateuliwa bungeni na teuzi zao haziwezi kutenguliwa.

Wachezaji wale wale kila siku kwanini tusitafute wachezaji wengine tuachane na hawa waliokubuhu akili.
Kuna watu wana mioyo ya uvumilivu aisee....yaani huyo Ulimwengu alivyo takataka ila bado kuna Club inamtegemea kama Forward wao na inamlipa Madolari.....kweli Wonders never end!!!
 
World Cup 2018 Argetina aliachwa Mauro Icardi top scorer Serie A, Germany aliachwa Leroy Sane sembuse Samata..Acha kukariri wewe Bashite...
Argentina unaifananisha na Tz una akili ww? Argentina kocha anaweza kuchagua vikosi hata vi3 na vyote vimeshiba .....unamtoa Samata unamweka nani? Mmeshazoea mpira wa magazetini kupamba wachezaji wakati viwango hamna
 
Amunike si kocha wa maana. Sijuwi ni mwendawazimu gani anayechagua makocha wa kufundisha Stars?
 
Iko wazi kabisa.. wachezaji ni mzigo!... Wanacheza Kama wanalazimishwa!.. Cape Verde wana kitu gani cha ajabu?? Ni kujtuma tuu
 
Sawa, alitolewa Mauro, akawekwa Messi, Aguero, Paulo Dyabala, walifika wapi Argetina na mpira gani walicheza? Ok, Akatolewa Sane akawekwa Muller na reus alicheza mpira gani Germany na aliishia wapi?Tumemuweka Sammata tumecheza nini na tumefika wapi? Tujitafakari tunakwama wapi.. Samata hataki kuumia kwa viposho vyetu halafu akasugue bench Genk..
 
Toa mudathir,Ulimwengu,Mwantika ,Kessy,Himid

Piga benchi Samatta,Msuva,manura


Ingiza Kichuya,Ajib,Nyoni ,Dirunga Ambokile
 


Hahahha, pole mkuu. Sasa mbona Okwi ni mfanyakazi wa Simba na anafanya mambo huko Uganda? Haitoshi kusema Samatta ni mfanyakazi wa Genk. Ila inakera sana aisee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…