Wajapani wanawezaje kutunza magari namna hii?

Wajapani wanawezaje kutunza magari namna hii?

Mkuu nakaa Kigamboni natumia pantoni mara kwa mara yaani kuna wamama wana ndoo za samaki wanapita nazo katikati ya magari wanagonga gari lako na zile ndoo bila kujali. Ukitaka siku yako iharibike muulize au mwambie apite vizuri. Bado wauza crisps hawajaweka matenga yao ya chuma juu ya bonnet, raia ataweka begi lake juu ya boot, bado kuna wale wabeba mabegi mgongoni kazi Yao ni kugonga na kugeuza side mirror. Ni balaa gari ina makovu balaa!
Pita darajani mkuu
 
Ndio maana nnapita darajani, japokuwa siku hizi hamna hizi purukushani,
 
View attachment 1659067

Wajapani wanawezaje kutunza gari na kubaki mpya kiasi hiki ikiwa na miaka 28. Japan ni nchi ya visiwa visiwa, hali ya hewa ya joto na wakati mwingine baridi Kali, upepo unavuma chumvi, vitu vinapata kutu.

Lakini magari ya Japan yana bodi imara sana haiathiriki na kutu ukilinganisha na magari ya Uingereza.
Hivi hii imekaaje?
Hata tu gari kuendelea kuwa mpya baada ya miaka 28 tangu itengenezwe.
Extrovert , RRONDO na Mshana Jr naomba maarifa yenu na wengine wote ambao sijawataja mwakaribishwa
Pamoja na miundombinu ya barabara za Japan kuwa bora, lakini pia Wajapani hutumia sana usafiri wa umma (public transport) ambao uko more advanced na kasi. Ambapo wengi hutumia gari binafsi kwa siku chache katika mwezi.
 
View attachment 1659067

Wajapani wanawezaje kutunza gari na kubaki mpya kiasi hiki ikiwa na miaka 28. Japan ni nchi ya visiwa visiwa, hali ya hewa ya joto na wakati mwingine baridi Kali, upepo unavuma chumvi, vitu vinapata kutu.

Lakini magari ya Japan yana bodi imara sana haiathiriki na kutu ukilinganisha na magari ya Uingereza.
Hivi hii imekaaje?
Hata tu gari kuendelea kuwa mpya baada ya miaka 28 tangu itengenezwe.
Extrovert , RRONDO na Mshana Jr naomba maarifa yenu na wengine wote ambao sijawataja mwakaribishwa
Kwa utaratibu wa kijapani, gari ni lazima kufanyiwa service/check up kila baada ya miaka 2.
Pili, gari kama hiyo umiliki wake ni wa mtu mmoja tu, tena Bibi wa kijapani ambae safari zake ni supermarket na nyumbani!!

Tatu, miundo msingi kuanzia barabara na teknolojia vina mchango mkubwa sana ktk utunzaji wa gari.
 
Bonge ya gari. Na Mimi nilikuwa nalo twin cams 6 cylinder.
Mimi pia mkuu hii gari niliwahi kuimiliki, ilikuwa inafunguka hatari, yangu ilikuwa na engine ya 1G curve,6 cylinder, halafu ilikuwa na mziki mzito wa Kenwood hauhitaji hata kuwa na booster. Pia ilikuwa na system moja ukiwa unaondoka ikifika 30 kph milango inajilock, niliipenda sana kwakweli...
 
Kwa utaratibu wa kijapni, gari ni lazima kufanyiwa service/check up kila baada ya miaka 2.
Pili, gari kama hiyo umiliki wake ni wa mtu mmoja tu, tena Bibi wa kijapani ambae safari zake ni supermarket na nyumbani!!

Tatu, miundo msingi kuanzia barabara na teknolojia vina mchango mkubwa sana ktk utunzajinwa gari.
Wanaume hawaruhusiwi kuendesha au kumiliki gari?
Je mujito hunywa na wanaume TU?
 
Mimi pia mkuu hii gari niliwahi kuimiliki,ilikuwa inafunguka hatari,yangu ilikuwa na engine ya 1G curve 6 cylinder,halafu ilikuwa na mziki mzito wa Kenwood hauhitaji hata kuwa na booster.Pia ilikuwa na system moja ukiwa unaondoka ikifika 30 kph milango inajilock,niliipenda sana kwakweli...
Ni gari moja nzuri. Kama kiuchumi upo vizuri sio ya kuiacha kwani kidogo inakula mafuta. Lakini ni gari nzito ukiwa ndani ni kama vile upo kwenye V8.
 
Back
Top Bottom