Wajapani wanawezaje kutunza magari namna hii?

Pita darajani mkuu
 
Ndio maana nnapita darajani, japokuwa siku hizi hamna hizi purukushani,
 
Pamoja na miundombinu ya barabara za Japan kuwa bora, lakini pia Wajapani hutumia sana usafiri wa umma (public transport) ambao uko more advanced na kasi. Ambapo wengi hutumia gari binafsi kwa siku chache katika mwezi.
 
Kwa utaratibu wa kijapani, gari ni lazima kufanyiwa service/check up kila baada ya miaka 2.
Pili, gari kama hiyo umiliki wake ni wa mtu mmoja tu, tena Bibi wa kijapani ambae safari zake ni supermarket na nyumbani!!

Tatu, miundo msingi kuanzia barabara na teknolojia vina mchango mkubwa sana ktk utunzaji wa gari.
 
Bonge ya gari. Na Mimi nilikuwa nalo twin cams 6 cylinder.
Mimi pia mkuu hii gari niliwahi kuimiliki, ilikuwa inafunguka hatari, yangu ilikuwa na engine ya 1G curve,6 cylinder, halafu ilikuwa na mziki mzito wa Kenwood hauhitaji hata kuwa na booster. Pia ilikuwa na system moja ukiwa unaondoka ikifika 30 kph milango inajilock, niliipenda sana kwakweli...
 
Wanaume hawaruhusiwi kuendesha au kumiliki gari?
Je mujito hunywa na wanaume TU?
 
Ni gari moja nzuri. Kama kiuchumi upo vizuri sio ya kuiacha kwani kidogo inakula mafuta. Lakini ni gari nzito ukiwa ndani ni kama vile upo kwenye V8.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…