Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Wakuu
Wajasiliamali wa kada mbalimbali kutoka wilaya zote tano za Jiji la Dar es Salaam wamezungumza na waandishi wa habari leo, Desemba 24, kuhusu msimamo wao juu ya maandamano nchini.
Akizungumza kwa niaba ya viongozi wenzake, Seleman Said Bane, aliyejitambulisha kuwa ni mjasiliamali wa vifaa vya michezo kutoka Ilala, aliwasilisha tamko la umoja wao na kulifikisha kwa jamii kama msimamo wao kuhusu vurugu na machafuko ya Oktoba 29, 2025, pamoja na athari zake kwa ustawi wa Tanzania.
Wajasiliamali hao wanatambua kuwa matukio hayo hayakuwa maandamano halali, bali yalikuwa vurugu na machafuko. Wamesisitiza kuwa wao, kama wadau wengine katika jamii, wanakabiliwa na changamoto, madai, matamanio na mahitaji halali yanayopaswa kusikilizwa, kujadiliwa na kutatuliwa kwa njia za amani.
Hata hivyo, wamesema uzoefu wa Oktoba 29 umewafundisha kwa gharama kubwa kuwa vurugu, uvunjifu wa amani, uchomaji wa mali za umma na binafsi, kutukana viongozi wa Serikali, pamoja na aina zote za uchochezi, haviwezi kamwe kuleta suluhu ya changamoto za wananchi.